Australia rangi ya njano wametoa wapi?

BigBro

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
3,209
9,860
Naangalia kombe la Dunia la Wanawake hapa, michuano inayofanyika kwa ushirikiano wa nchi mbili ndugu, New Zealand na Australia. Mchezo wa kwanza New Zealand kashinda 1-0 dhidi ya Norway, sahizi ni Australia na Republic of Ireland.
Timu za taifa zinatumia jezi zenye rangi ya bendera yao, lakini Australia anatumia jezi ya njano wakati bendera yake inafanana na ya England na New Zealand. Hii rangi ya njano kaitoa wapi?

NB:
Hii ni michuano ya tisa tangu ilipoanzishwa mwaka 1991 na inafanyika kila baada ya miaka minne na mwaka huu timu imeongezeka kuwa 32.

Marekani kashinda mara nne na ndio bingwa mtetezi na ndo timu iliyobeba kombe hilo mara nyingi zaidi. Ujerumani mara mbili, Norway mara moja na Japan mara moja.
 
Jezi na benders wapi na wapi?

Yanga siku hizi wana jezi nyeusi na dark blue, bendera ya Yanga ni kijani na njano.
 
Back
Top Bottom