AUDIO: Samuel Sitta azungumzia taarifa za kuhamishwa kwenye nyumba ya serikali

lil wayne

JF-Expert Member
Apr 15, 2016
992
904
Kumekuwa na taarifa ambazo zimeripotiwa na moja gazeti leo July 15 1016 likidai kuwa aliyekuwa spika wa bunge la tisa Samuel Sitta, kuondolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi baada ya serikali kugoma kulipia kodi ya pango. Samuel Sitta ameeleza usahihi wa taarifa hizo ambapo amesema……..


’Hakuna ukweli wowote kusema mimi nimeondolewa katika nyumba, ina maana gani kuwa katika nyumba wakati mimi sina cheo serikalini, tangu mwaka jana wakati naandaa makazi mengine nilikuwa najilipia pango mwenyewe baada ya hapo mimi nimehama mwenyewe hakuna suala la kuhamishwa‘


 
Kwamba ukweli ni amehama...sasa anachokanusha ni nin..nchi hii makambale wengi sana
 
6ba2c04c1226cc3f5b36910da2362267.jpg

Mzee yuko kazini..
 
Issue iko hivi mr Spika wa kupika katiba! Je uko kwenye hiyo nyumba au hauko? Hilo ndilo la msingi.
 
Safi sana Mzee Sitta umewashushua waliojenga kiwanda cha kupotosha kila aina ya taarifa. Kutwa nzima wanatunga uongo tu

Cc
Machadema.
 
Issue iko hivi mr Spika wa kupika katiba! Je uko kwenye hiyo nyumba au hauko? Hilo ndilo la msingi.
Amesema alikuwa anajilipia? Kwani serekali inafanya biashara? Si nyumba ya serekali hiyo au ni zile JPM aliuza wakazitengeneza sasa wanazikodisha kwa viongozi??
 
Kila mtu atavuna alichokipanda wacha ajifariji mzee wawatu ila inaonesha uzee huyu utakua nachangamoto nyingi zaidi
 
Hili zee kama limechanganyikiwa vile,si umehama sasa sijui anabisha nini.Sitta ulizoe vya kujonga nenda kaishi manzese uko
 
Waandishi wa kitanzania wengi wao hawajui kutofautisha habari na udaku, sijui wanasomea wapi!
 
Kichekesho! Kwamba miaka yote alikuwa bado hajaandaa makazi mpaka akose cheo ndo aanze kujipanga?
 
Back
Top Bottom