Audio: Matapeli wa Mtandao

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,451
6,325
Juzi hapa nilipata SMS kwenye simu yangu ikitoka Tigo, ikinikumbusha kujisajili kwa alama za vidole ili niweze kupata gawio langu la Tigo Pesa.

After 5 minutes nikapigiwa simu na mtu ambaye alijitambulisha kama ni wakala wa Tigo na akaanza kunipa maelezo ya jinsi ya kupata gawio langu.

Ila baada ya muda nikahisi jamaa ni tapeli sababu maelezo ambayo alikuwa ananipa yalikuwa ya kutoa pesa kwenye simu yangu kwenda kwenye simu yake.

Nikaanza kumrecord na mazungumzo yakawa kama hivyo.

Sasa nikawa nawaza je hawa matapeli watakuwa ni wafanyakazi wa hii mitandao ya simu? Walijuaje kama nimetumiwa SMS na Tigo ya kuhusu gawio?

Tuwe makini jamani
 
Attachments

  • Call recording 255672771525_200211_131722.m4a
    10.9 MB · Views: 3
ingekuwa ni sauti ya mwanachadema ungekuta tcra washamkamata ila matapeli na wezi tcra kwao sio ishu, huyoo jamaa ataendelea tapeli watu wengi bila kukamatwa.

Wamkamate tapeli watapata wapi sifa kwa mkuu?
 
Huyo jamaa kuna siku alinipigia simu akaniuliza "samahani napiga simu kutoka Tigo nakuuliza iwapo laini yako imesajiliwa kwa alama za vidole"?
Nikamjibu ninyi si ndio wenye kufahamu nani amesajili nani bado. Au ni mtandao wa Tigo UPI huo? Jamaa akakata simu.
 
Hao jamaa ukiwashtukia wanakuporomoshea matusi.

Ukitaka uwaweze tumia simu yenye line ambayo haina hela kuingiza hizo namba anazokutajia, utajifunza mengi.
 
Juzi hapa nilipata SMS kwenye simu yangu ikitoka Tigo, ikinikumbusha kujisajili kwa alama za vidole ili niweze kupata gawio langu la Tigo Pesa.

After 5 minutes nikapigiwa simu na mtu ambaye alijitambulisha kama ni wakala wa Tigo na akaanza kunipa maelezo ya jinsi ya kupata gawio langu.

Ila baada ya muda nikahisi jamaa ni tapeli sababu maelezo ambayo alikuwa ananipa yalikuwa ya kutoa pesa kwenye simu yangu kwenda kwenye simu yake.

Nikaanza kumrecord na mazungumzo yakawa kama hivyo.

Sasa nikawa nawaza je hawa matapeli watakuwa ni wafanyakazi wa hii mitandao ya simu? Walijuaje kama nimetumiwa SMS na Tigo ya kuhusu gawio?

Tuwe makini jamani
Nimecheka .
 
Back
Top Bottom