Wakazi wa DAR kwa muda mrefu wamekua wakilalamikia Auctions mart ambao walikua wanafunga magari hovyo hovyo, na likifungwa tu ni rushwa 50,000 au gari inaenda yard unalipa 150,000.
Leo, nimesikia mkuu wa mkoa wa Dar amepiga marufuku hawa jamaa kufunga magari.
Ingawa umekuja umechelewa lakini huu ni moja kati ya uamuzi bora kabisa kuwahi kufanywa na viongozi wetu, i wish wangeenda a step further na kuchunguza nani alikua akifaidika na ile biashara haramu, na ikiwezekana waathirika, wao weza kuonyesha uthibitisho wa malipo, mimi mmoja wapo, warejeshewe pesa zao.
Hawa jamaa walifikia wakati wanafunga gari hata kama dereva yuko ndani ya gari, mimi siku nafungiwa jamaa alikua ananitaza, sijafika hatua tatu mbele naona jamaa wanafunga gari, yaani wananitizama wakati nasimama ili wafunge wapate pesa, walikua ni MWAMKINGA AUCTION MART