TheCrocodile
JF-Expert Member
- May 31, 2021
- 1,857
- 5,215
Kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Sefu Musa amefariki dunia baada ya kudaiwa kuuawa na askari watatu katika eneo la Ngorongoro mkoani Arusha, baada ya yeye na wenzake kutuhumiwa kuwa ni majangili.
Sefu alikuwa pamoja na Salim Hamisi maarufu Pachaa na Abdallah Nuru, wakitokea Arusha mjini kuelekea Babati mkoani Manyara kwa ajili ya kumzika mwenzao ambaye walikuwa wakifanya naye kazi ya kutengeneza magari maeneo ya Desemba jijini Arusha.
Watatu hao walikuwa wamepanda pikipiki moja na walipofika Makuyuni walipotea njia na kuelekea Karatu badala ya Babati. Waliendelea hadi Karatu mjini na kufika katika lango la kwanza la Ngorongoro lililokuwa likilindwa na askari watatu.
Baada ya kufika lango kuu la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro walibaini kuwa wamepotea njia na wakaamua kurejea. Inadaiwa walipofika katika lango la kwanza walikamatwa na askari hao na kutuhumiwa kuwa ni majangili, licha ya kueleza kuwa walikuwa wamepotea na walikuwa wakielekea Babati kwa ajili ya mazishi.
Kwa mujibu wa maelezo ya Abdallah Nuru, ambaye ndiye aliyenusurika, vijana hao waliamriwa kuvua nguo na kujigaragaza kwenye majani yaliyokuwa yakiwasha huku wakimwagiwa maji na askari hao, kabla ya kudaiwa kupigwa.
Katika tukio hilo, Sefu Musa alidaiwa kuzidiwa nguvu na kupoteza fahamu huku Salim Hamisi naye akizimia. Abdallah anadaiwa kupata majeraha mbalimbali lakini aliendelea kuwa na nguvu na kuwasaidia wenzake.
Baada ya hali kuwa mbaya, inadaiwa waliambiwa wavae nguo na kuondoka eneo hilo. Abdallah alitafuta bajaji na kuwapeleka wenzake katika Hospitali ya Lutheran Karatu.
Walipofika hospitalini, Sefu alikutwa amefariki dunia huku Salim akiwa katika hali mbaya na kupewa huduma ya oksijeni iliyomsaidia kurejea kwenye fahamu. Anaendelea kupatiwa matibabu.
Abdallah Nuru ndiye aliyenusurika na kufanikiwa kuwasaidia wenzake hadi hospitalini licha ya yeye mwenyewe kupata majeraha. Mwili wa Sefu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha alipigiwa simu kwa ajili ya kupata ufafanuzi kuhusu taarifa hii, lakini simu yake iliita bila kupokelewa.