Mstahiki Mea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 5,581
- 10,110
Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Wende Luchagula (30) mkazi wa kijiji cha Milonji kata ya Lusewa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, anadaiwa amewaua watoto watatu wa mke mwenzie kwa kuwachinja na kitu chenye ncha kali shingoni kwa madai kuwa mumewe anampenda zaidi mke mdogo pamoja na watoto hao kitendo ambacho hakimpendezi.
Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea Julai 12, 2025 majira ya saa nane mchana huko katika kijiji cha Milonji kata ya Lusewa wilayani humo ambapo mtuhumiwa alivizia mumewe akiwa ametoka pamoja na mke mdogo kisha akatekeleza tukio hilo la mauaji.
Aidha watoto waliouawa na mama huyo wametajwa kwa majina yao kuwa ni Lugola Samweli (06), na mapacha ambao ni Kulwa Samweli na Doto Samweli wenye umri wa miezi (08).
Hata hivyo Jeshi la Polisi mkoa wa Ruvuma limethibitisha kumshikilia mwanamke huyo kwaajili ya taratibu za kisheria na uchunguzi zaidi.