Watoto watatu wafariki Kanisani Simiyu baada ya kulala kwenye hema lenye jiko la mkaa

Watoto watatu wafariki Kanisani Simiyu baada ya kulala kwenye hema lenye jiko la mkaa

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2013
Posts
14,698
Reaction score
7,907
Watoto watatu wa kike wakazi wa kijiji na kata ya Mkula, Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, wamefariki dunia wakiwa kwenye makambi ya Kanisa la Waadventisa Wasabato wilayani hapo

Chanzo cha tukio hilo kinadaiwa kuwa ni kukosa hewa baada ya kulala kwenye hema ambalo lina jiko la mkaa.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, anamringa Macha, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
 
Watoto watatu wa kike wakazi wa kijiji na kata ya Mkula,Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu,wamefariki dunia wakiwa kwenye makambi ya Kanisa la Waadventisa Wasabato wilayani hapo,chanzo la tukio hilo kinadaiwa kuwa ni kukosa hewa baada ya kulala kwenye hema ambalo lina jiko la mkaa.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Anamringa Macha,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Mkaa unaua haraka sana ukilala jiko linawaka. Hao waalim waangalizi walikuwa hawajui? Uzembe wa hali ya juu.
 
Unaweza usielewe inakuaje hadi leo watu wanaendelea kufa kwa uzembe huu ni sawa na wale wanaokula kasa kule Zanzibar!!

Wengi husema wajiegeshe watazima jiko wakitaka kulala na ndiyo inakuwa "niagieni niagieni".
 
Duh!,kwan kwenye makambi kila mtu anakuwa na jiko lake
Makambi ya Sasa hivi naona yameadvance.
Hata Wachungaji Wana Jiko lao na wapishi wao special.
Enzi nakua Kuna mke wa mjomba kwenye makambi ikitoka list ya wapishi wa vinono vya Wachungaji hakosi kwenye top 3.
Basi mimi nakuwa msabato pure kabisa maana ubwabwa hapo ni uhakika.

Makambi yakiisha usabato wangu unakuwa wa kuchaji 🤣🤣
 
Hao wasimamizi na waandaaji Kwa ujumla ni wapumbavu sana! Wamekatili maisha ya watoto kwa uzembe wa kutoweka mpangilio mzuri wa msosi kwenye hayo makambi, hawana tofauti kbs na mafuta ya mwamposa yaliyoangamiza makumi kule Moshi miaka ya nyuma kidogo! napendekeza serikali ya CCM iyapige marufuku hayo makambi..RIP WATOTO
 
Watoto watatu wa kike wakazi wa kijiji na kata ya Mkula,Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu,wamefariki dunia wakiwa kwenye makambi ya Kanisa la Waadventisa Wasabato wilayani hapo,chanzo la tukio hilo kinadaiwa kuwa ni kukosa hewa baada ya kulala kwenye hema ambalo lina jiko la mkaa.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Anamringa Macha,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Habari ya muda mrefu sana tangu Mwezi wa 8 katikati huko
 
Back
Top Bottom