Aua mke kwa kuzaa mtoto wa kike | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aua mke kwa kuzaa mtoto wa kike

Discussion in 'International Forum' started by The Boss, Jan 2, 2010.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Amuua Mkewe Kwa Kumzalia Mtoto wa Kike
  [​IMG]
  Daniel Hicks mkewe na mtoto wake aliowauaWednesday, December 30, 2009 1:30 PM
  Mwanaume mmoja wa nchini Marekani ambaye alikuwa na shauku kubwa ya kuwa na mtoto wa kiume anatafutwa na polisi baada ya kumuua mkewe aliyejifungua mtoto wa kike.Daniel Hicks mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa Seattle, Washington nchini Marekani anatafutwa na polisi baada ya kumuua mkewe na mtoto wake mchanga wa kike mwenye umri wa miezi mitatu.

  Daniel alifanya mauaji hayo kwa kuwa alikuwa hajaridhia mkewe Jenifer Morgan mwenye umri wa miaka 28 kujifungua mtoto wake.

  Daniel alimwonya mkewe wakati wa ujauzito wake kuwa iwapo atajifungua mtoto wa kike basi atamkataa yeye na mtoto atakayejifungua.

  Miezi mitatu baada ya mkewe kujifungua mtoto wa kike, Daniel alishindwa kuzizuia hasira zake na kumuua mkewe pamoja na mtoto wake mchanga kabla ya kutoroka na kujificha sehemu isiyojulikana.

  Daniel alimuua mkewe kwa kumpiga risasi 12 na hakuwa na huruma hata kidogo kwa mtoto wake mchanga ambaye alimuua kwa kumtandika risasi 7.

  Daniel kabla ya kutoroka aliacha ujumbe akisema kuwa anasikitika yeye pia ana ugonjwa kama wa babu yake.

  Mnamo mwaka 1983 , Babu yake Daniel alimuua mkewe kwa kumpiga risasi kabla ya kujimaliza mwenyewe.

  Polisi wanaendelea kumtafuta Daniel.
   
 2. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi si mfagiliaji wa adhabu ya kifo, lakini kesi kama hii adhabu ya kifo ni lazima itumike.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mhhh.
   
Loading...