Aua mke kwa kumkata shoka mara tatu

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
MKAZI wa Kijiji cha kideleko Kata ya Kideleko wilayani Handeni Tanga, Amina Mbwego (35), ameuawa kwa kukatwa shoka shingoni na mumewe.

Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi, ambapo mume huyo aliyetajwa kuwa ni Josephu Wiliam (26) mkazi wa mkoani Dodoma, alimkata Amina mara tatu kwa shoka na kusababisha kifo chake papo hapo.

Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Coustantine Massawe, zilieleza kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Machi 6 mwaka huu katika Kijiji cha Kwaluwala, Kata ya Kang'ata wilayani Handeni.

Kamanda Massawe alisema kuwa amesikitishwa na matukio hayo ya mauaji ambayo chanzo chake ni mapenzi, akitaka wanandoa kuheshimu na kuwa waumini wa ndoa zao.

Mmoja wa ndugu wa marehemu ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alisema:"Yule jamaa ambaye kabila yake ni Mgogo amemfanyia unyama wa kutisha ndugu yetu, kabla ya kumuua alimlaza chini kifudifudi chumbali na kumcharanga mara tatu kwa shoka shingoni kama anapasua kuni. Baada ya kutimiza azma yake hiyo alitoroka kupitia dirishani."

Alisema kuwa baada ya William kukimbia kijijini, walikwenda kwa mganga wa jadi ili aweze kumzuia asiende mbali, ambapo baada ya kufanya hivyo asubuhi majira ya saa 2:30 asuhi walifanikiwa na asubuhi ya siku iliyofuata alionekana dukani katika kijiji cha Kideleko jirani na lilipotokea tukio akinunua sigara.

Ndugu huyo alisema kuwa baada ya William kuonekana alikamatwa na wanannchi na kupigwa kilichiosababisha apoteze fahamu kabla ya kuokolewa na polisi na kumfikisha katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni ambapo amelazwa akiwa mahututi.

Mmoja wa maofisa wandamizi wa polisi wilayani Handeni, alisema ambaye hata hivyio hakutaka kuandiwa jina kwa kuwa siyo msemaji wa polisi alieleza kuwa tukio hilo lilitokana na wivu wa kimapenzi, baada ya wawili hao kutoelewana katika mahusiano yao.[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]
[/FONT]
 
Huo wivu wa kupigana jamani,hivi wanawake hamna wivu? Na nyie muwapige waume zenu hata kwa mashoka maana hawana jema!
Wanakuja wamelewa wanaanzisha ugomvi,ukijihami ataanguka afe,ukizubaa utakufa wewe.
 
Na hiyo njia ya kwenda kumzuia mtuhumiwa kwa Kalumanzila...
Tumethubutu,tumeweza na Tunasonga mbele
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom