Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,277
Jamaa huyo alikuwa amenunua nyumba katika gorofa 40 ya jengo hilo Chongqing, aliamua aifanyie ukarabati ili imfae zaidi
Ripoti zinasema ufunguo aliopewa ulikuwa wa nyumba tofauti na ile aliyonunua, lakini yeye mwenyewe hakufahamu
Alipopewa ufunguo hakupoteza muda kwani alianza mara moja kufanya ukarabati wa mamilioni ya pesa, lakini baadaye ndipo wasimamizi wa jengo hilo wakamwambia anakarabati nyumba ya wenyewe
Imesemekana kulikuwa na nyumba nane katika gorofa hilo lakini ni nyumba nne pekee ambazo zilikuwa zimeuzwa, waliotoa maoni kuhusu habari hizo walipendekeza apewe hiyo nyumba kwa vile tayari ametumia pesa nyingi kuikarabati, huku wengine wakilaumu wasimamizi.