ATM nyingi nchini hazifai - Waziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ATM nyingi nchini hazifai - Waziri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Msindima, Oct 9, 2009.

 1. M

  Msindima JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  9th October 2009


  Na Richard Makore  [​IMG]
  Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Jeremiah Sumari.  Serikali imesema mashine nyingi za kutolea fedha benki (ATM), ni mbovu kwa kuwa huingizwa nchini kutoka nje baada ya kuonekana huko hazifai.
  Imesema hatua hiyo inasababisha kuwepo wimbi la watu kuiba fedha za wenzao kupitia mashine hizo bila wenyewe kujua.

  Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Jeremiah Sumari, alipokuwa akijibu maswali ya wabunge katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi.
  Sumari alisema kuwepo kwa mashine hizo ni hatari kwa usalama wa fedha za wananchi.

  Alifafanua kuwa kuna nchi moja ambayo hakuitaja iliwahi kuhamisha mashine zake zilizokuwa mbovu na kuzipeleka nchi nyingine na kwamba tukio hilo linaonyesha kuwa hata hapa nchini ziliingizwa.
  Alishazishauri benki kuchukua tahadhari ili kuepusha wimbi la wizi kupitia ATM.

  Hivi karibuni, Jeshi la Polisi liliwakamata raia wawili wa Bulgaria kwa tuhuma za kuiba kiasi cha Sh. milioni 70 jijini Dar es Salaam kupitia mashine hizo bila kutumia kadi. Wameufunguliwa mashitaka kortini.

  Mbali na matukio ya wizi, baadhi ya ATM zimekuwa zikilalamikiwa na wateja wa benki kutokana na kuharibika mara kwa mara na wakati mwingine kutokuwa na mtandao, hivyo kuwasababishia usumbufu wa kutopata huduma.

  Akizungumzia Benki ya Posta Tanzania ambayo serikali inamiliki asilimia 81 ya hisa, alikiri kuwa inahitajika sheria itakayoibadilisha kuwa kampuni ili iweze kufanya kazi kwa kushindana.
  Sumari alikuwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliokuwa wakijadili utendaji wa benki hiyo.

  Uongozi wa benki hiyo uliwaeleza wabunge kuwa unakabiliwa tatizo la mtaji mdogo, jambo ambalo linawafanya washindwe kufikia malengo waliyojiwekea.
  Wakichangia katika kikao hicho baadhi ya wabunge walisema bila sheria kufanyiwa marekebisho itakuwa vigumu benki hiyo kuweza kufanikisha malengo yake.

  Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Abdallah Kigoda, alishauri mabadiliko hayo yafanyike haraka na serikali iache kutumia neno "ipo kwenye mchakato" kwani hali hiyo inakatisha tamaa.

  Alisema neno mchakato halina mwisho na halisemi ni lini kazi husika au itaanza kufanyika, kauli ambayo iliungwa mkono na wabunge wengi.
  Kwa upande wake mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed, alisema wananchi wamechoshwa na neno "mchakato" ambalo serikali inapenda kulitumia kwa kuwa halionyeshi ni lini itafanya kile inachokusudia kukifanya.

  Aliishauri serikali kuuza hisa zake zote za Benki ya Posta na kujitoa katika biashara.
  Aidha, aliutaka uongozi wa Benki ya Posta kuacha kulalamika badala yake ufanye kazi kwa kushindana na watu wengine.
  Vikao vya kamati hiyo vinaendelea leo katika ofisi ndogo ya Bunge, jijini Dar es Salaam.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu naye asituzingue hapa na majibu yake ya hovyo hovyo kwani zinapoingizwa si ni serikali hii hii inayozikagua au
   
 3. E

  EMMANUEL SHOMBE Member

  #3
  Oct 9, 2009
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nani alaumiwe kati ya mwananchi, na huyo waziri, au MABENKI?
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Everybody has witnessed this in our banks!Siku ukiwa na shida kubwa kabisa unakuta hazifanyi kazi, japokuwa most of times huwa ni network issue!Baadhi ya watu tumelazimika kuwa na akaunti mabenki mbalimbali ili at least ikikwama ya siaradibii, unakimbilia eniembii! lol!
   
 5. JS

  JS JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2009
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  wao wenyewe hawakagui hizo mashine zinapoingizwa nchini ni uwizi kila mahali halafu eti wako kwenye mchakato!!!
   
 6. M

  Msindima JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hivi hiyo michakato yao huwa haikamiliki hata siku moja?
   
 7. M

  Msindima JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mwananchi kwa nini alaumiwe? kwanza alishazoea kwenda kupanga foleni na kuchukua pesa zake,haya mambo ya ATM ni wao wenyewe ndo wamewaletea wananchi.

  hata waziri sidhani kama lawama zinamwangukia maana unaweza kuta yeye ameingia kwenye hiyo wizara akakuta tayari ATM zilishaingia na si ajabu hata ukimwuliza zilianza kuingia lini wala hajui.

  kwa mabenki sijui labda tunaweza kulaumu kwa sababu yawezekana yenyewe ndo yalitoa mapendekezo kwa serikali ili yaweze kwenda na technolgy na kupunguza zile foleni za enzi zile.
   
 8. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,876
  Likes Received: 23,503
  Trophy Points: 280
  Mi ndio maana fweza zangu nazisunda chini ya pillow, nikijisikia kupiga ulabu au kusarandia mechi za mchangani najisevia kilaini. Hamna service charge wala nini. Mtakoma na mabenki yenu uchwara.
   
 9. M

  Msindima JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  hata mimi nashangaa wanaagiza wenyewe,wanazikagua wenyewe halafu leo anatwambia kuwa hazifai? kwa nini hawakusema hazifai kabla?
   
 10. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wanao agiza ATM sio Bank ni kampuni ambazo zimeshinda tender, tyhen wana instal, kama ATM zimechoka ukakuta na server kimeo hapo kazi ipo.
   
 11. M

  Msindima JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Chriss acha kutudanganya unataka kutwambia wewe unakaa na pesa zote nyumbani? hili nakukatalia siku hizi hakuna mtu anaeweka pesa nyumbani maana kuna mambo mengi wezi wanaweza kuingia na kuzikomba si hivyo tu nyumba inaweza kuwaka moto sasa kama ziko nyumbani baada ya majanga hayo itakuwaje?
   
 12. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,876
  Likes Received: 23,503
  Trophy Points: 280
  Lol! Ahsante mkuu, nilishasahau. Ntaweka hela benki, sehemu ya usalama. Hahahaha. Nakumbuka ulisema watu wa benki wanapaswa kula matikiti kwa wingi kwa kuwa nguvu za kiume ziko kaputi!
   
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,876
  Likes Received: 23,503
  Trophy Points: 280
  Karibu lunch binamu. Inaelekea unanijua sana, ahsante.
   
 14. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #14
  Oct 9, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hii issue ni serious! ndio maana hakuna aliyebisha, alibisha Burn nikamuelewesha nae akaelewa, BANK NOMA JAMANI DU!
   
 15. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #15
  Oct 9, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,876
  Likes Received: 23,503
  Trophy Points: 280
  Itabidi nimfanyie mpango wife apate kazi benki sehemu ya usalama. Huko aliko mijamaa itakuwa inanimegea.
   
 16. M

  Msindima JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Asante sana,sikujui ki-hivyo.
   
 17. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #17
  Oct 9, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,876
  Likes Received: 23,503
  Trophy Points: 280
  Umeanza uchoyo kama kawaida yako. Kitu kizuri tumia na nduguyo.
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  TZ kweli ni shamba la bibi! Bila kuitaja benki husika lakini nahisi hawa watakuja baina ya NBC au NMB, nawahisi zaidi hawa makaburu wa NBC.

  Sasa waziri mzima kuishia tu kusema kuwa 'wanaingiza ATM mbovu' bila kusema ni hatua ipi inachukuliwa, inatuma meseji gani kwa hao waleta bidhaa hafifu, wateja na wadau wengine kwa ujumla? Waziri anasubiri nani achukue hatua za kuwawaijibisha wahusika?
   
 19. M

  Msindima JF-Expert Member

  #19
  Oct 9, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135

  EEee yameshakuwa hayo tena.
   
 20. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #20
  Oct 9, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,876
  Likes Received: 23,503
  Trophy Points: 280
  Usiogope. Mambo ya kawaida tu. Kwahiyo? NiPM basi kama vipi.
   
Loading...