Atlas Primary School - Madale, Dar

Kwani umeshikiwa bastola kwa watoto wako kusoma huko?
 
Ipo wapi? Mimi namuonea huruma mwanangu kumpeleka shule za mbali, afadhali ya hii anapitiwa saa 1.
Ipo karibu na bahari beach hotel,, ukipita chuo cha Jeshi (DEFENCE COLLEGE )
pale kunduchi
 
Nyie wazazi mabashite kweli. Hilo linawashindaje wakati shule ni private na mnatoa hela zenu.
Watu wanachoipendea hii shule ni Ufaulu na ada,
Kimkoa hua zinashindanaga kati ya Atlas ya Ubungo v/s Atlas ya Madale, zingine zinasubiri pemneni.
Pili ni ada kwani shule wakati shule hii ada ya Mwanafunzi wa chekechea haifikii Tshs 1.4mil, kwa shule ya Sunrise iliyoko pale Morocco eneo la makochi chekechea hiyo hiyo ni zaidi ya Tshs 4mil na zinalipwa in term of USD
 
Namtoa kabisa Atlas sitaki wanipe presha, Dereva unampigia anakupa majibu mepesi kabisa kama vile kaacha boga
Na chakushangaza dereva ndiyo anapanga kituo cha kumpitia mtoto,na darasa lina wanafunzi wengi mno.
 
Me mwanangu nishamtoaga nimempeleka bahari primary kitambo
Bahari shule nzuri sana, pia wanangu wanasoma bahari, sikutaka kabisa kuwapeleka atlas

Tatizo letu wazazi hatufanyi maandalizi mapema ya kuwatafutia watoto wetu shule, huwa tunafuata mkumbo na maandalizi ya zima moto, wakati tunataka watoto wasome shule nzuri

Lazima tuwatendee haki, kuanzia mazingira mpaka elimu
 
Hili tatizo lipo mno..sio Atlas ya madale tu hata ya Ubungo watoto wanapakatana wengine wanasimama.Ilitulazimu kuwaamisha watoto Hazina tu maana walikua wanasimama kutokea Kinondoni hadi Ubungo.Ila kwa taaluma wanajidahidi usafir ndo wanakosea mno.Wajirekebishe kwa hili.
 
Sasa mkuu haya maoni yako si ungeyatoa moja kwa moja kwa management ya shule?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…