Athumani Idd'Chuji' na Haruna Moshi'Boban' kujitoa stars

Nidhamu ni kila kitu katika maisha.
Bila nidhamu, huna taifa, bila nidhamu huna familia,bila nidhamu hakuna maendeleo ya soka.
Yaliyotokea Abdijan ni jawabu la swali,kwanini mpaka sasa hatuna wachezaji wa kulipwa nchi za ulaya.
Tulifikiri kuwa, hii CHAN ingelikuwa break thru kwa Vijana wetu....!!!
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Tuliambiwa leo atakata mzizi wa fitina kilicho jili huko Ivory coast, Maximo kasema nini au kasema hata ongeza mkataba tena...
 
Last edited:
Bongo tutakuwa na mpira mpaka baada ya miaka 30 na kuendelea ila kwa sasa tuendeele kuwasindikiza wenzetu!!
 
tatizo bangi wakuu, hawa vijana, na wengine wapo ila maximo hajawagundua, wanapuliza balaa!!
 
Maximo anatakiwa kuwatambua wadau wa soka na kuhakikisha maslahi ya wadau yanatimia, sasa wachezaji ni wadau na wana maslahi pia cocher ni zaidi ya mwalimu sasa Maximo ana behave kama mwalimu wakati anapewa vinaja awacoach.

Si sahihi kusema mafanikio ya stars yanaletwa na Maximo, yeye ni mdau mmoja wapo katika kundi la wadau na hakubali na lawama pia. huyo Jk aliyemleta analaumiwa kila kukicha ndio itakuwa Maximo bwana, amebwagwa Big Phil wakati timu ni ya Tatu katika msimamo. Lakini wabongo tunaambiwa tulidhike na kufungwa, kudroo na kushinda game moja hata kama tuna mtazamo tofauti hii haipo mpira unanoga kama kuna wanao pinga, sio siasa kusema ndio mzee kila siku.

Kwa mazingira ya sasa Tanzania inastahili kuwa mbali zaidi ya ilipo, hata ushindi wenyewe sio predictable kama zilivyo timu za wenzetu. Ukilinganisha na majirani zetu sisi ndio tumewekeza zaidi katika timu ya taifa na hata ligi kuu, tunawazidi hata kenya katika matumizi wakati uchumi wetu ni mdogo lakini kiwango chetu ndio cha chini. tukisema mnalinganisha na miaka 18 iliyopita tena mnafunika hata historia kwamba mashindano yale ya mwaka 1982 ilikuwa CHAN ya ukweli sio hii ya wachezaji wa ndani.

Lakini mnakuwa wakali mkiambiwa bongo bado, si tunaona wakicheza sifa hazikutosha kutupeleka nusu fainali na Afrika mashariki ndio tumechezea kichapo hata cha wasomali. Pesa inayoenda stars ni nyingi kuliko kinachopatikana huko, uliza hata zambia wametumia ngapi ndio mjue Tanzania wanapiga hela na kugombana. Kama bangi wachezaji wengi wa kibongo wanakula jani na sio kigezo cha mwalimu kuchuniana na wachezaji kama vipi si awafukuze yeye si ndio kawaita anaogopa nini sasa.

Maelezo meeengi, point hakuna. Hujui hata unachotaka kueleza.
 
tatizo bangi wakuu, hawa vijana, na wengine wapo ila maximo hajawagundua, wanapuliza balaa!!

Siamini kama hilo nitatizo kiivyo mbona hata majuu wapo wanao bwia uganga na bado wana sakata soka sema wachezaji wetu wengi hawana malengo akisha fika msimbazi au jangwani basi anajiona kamaliza kazi...na uongozi nao ni tatizo hasa hizi timu mbili kubwa...na Akina ndolanga waliturudisha nyuma sana...lkn kwa pamoja tutafika tu......
 
MAXIMO alishasema mkataba ukiisha anaondoka suala lililopo ni kujadili nani ambye ana uwezo kuliko yeye atakaweza kumrithi lakini sidhani kama kuleta kocha mwingine ndio suluhisha ,soka la Tanzania tuna matatizo mengi sana hilo la kocha ni mojawapo
Kenya wana MARIGA,OLIECH wanacheza ulaya na kina AMBANI,MWALALA,OWINO,SUNGUTI wanacheza bongo,Uganda wana NSEREKO na OBUA wako ulaya .Sijui kama kuna mchezaji wa bongo anayecheza soka Kenya au Uganda

Kama umejaribu kufuatilia wachezaji wa Tanzania wanapokwenda kujaribiwa nje ya nchi hasa ulaya wanafeli katika maeneo matatu makubwa:

Kwanza, they are not athletic players, wapungufu wa stamina.

Pili, Ndani ya masaa 36, wanagundulika kuwa na uwezo mdogo wa kufuata maelekezo.

Tatu, wanaonekana kuwa hawako organized kama professional hasa pale wanapotakiwa waeleze malengo yao ndani ya miaka mitatu na mitano.

Haya yote hata kama unakipaji jopo linalopitisha wachezaji kwa ajili ya timu zao kubwa hawawezi ku-risk kumchukua mchezaji ambaye haeleweki.

Ili ku-attain hayo hapo juu ni lazima kwanza uwe na nidhani ya binafsi kwa maana ya kuwa na ratiba ya mazoezi binafsi, utaratibu wa mpangilio wa chakula, muda wa kupumzika, muda wa kusoma vitabu na majarida yahusuyo professional yenyewe nk

Pili, ni lazima uwe na nidhamu ya hali ya juu kwa coach (manager) kwani yeye ndiye aliyepewa dhamana nzima ya kuwaunganisha wachezaji waweze kucheza kitimu kwa mujibu wa programu alizozitayarisha na kuidhinishwa na bodi ya timu husika. Kitendo chochote cha utovu wa nidhamu, ikiwa ni pamoja na kutofuata maelekezo ya coach kinatosha kukuweka pembeni au benchi. (Refer kutokuelewana katika ya Mchezaji maarufu duniani David Bekham na Sir Alex Ferguson).

Tukirudi kwa wachezaji wetu, wengi wao malengo yao makubwa ni kucheza mpira Yanga au Simba. Na mara tu anapofanikiwa kuingia katika moja ya vilabu hivyo basi anaona amemalizana hakuna anayeweza kumwambia kitu from there. Na ikitokea kuonekana kuwa ni mchezaji muhimu kwenye kilabu hicho , hapo ndiyo usiseme, hajisikilizi hata yeye mwenyewe, atalewa sifa hadi mpira unamkimbia polepole. Siku atakayogundua kuwa yeye ni mchezaji mpira na muda unakuwa umekwisha mtupa mkono anazidi kuvuta bangi kwa hasira na kama gongo ipo karibu basi itamkoma. Kamaakishtukia hayo mawili basi si ajabu ukamwona ni dereva wa daladala au atokee msamaria amwajiri kama messenger.

Ni vema kuwa wachezaji wa soka wa Tanzania ambao wanaweza kuja kuwa professional na wazuri ni hawa vijana wanaofundishwa kucheza mpira wangali na umri mdogo kabisa na wala sio hawa wanaofundishwa wakiwa na umri mkubwa wa zaidi ya miaka 20. Hebu fikiria leo hii unamuingiza kijana wa miaka 20 darasani ajifunze kuandika na kusoma?

Ninaunga mkono kuwaondoa wale wote wasio kuwa na nidhamu katika timu ya Taifa, ni vizuri wakatoa nafasi kwa wale ambao wako tayari kumsikiliza mwalimu.
 
Mpaka sasa ni Maximo tu anayeongea na hatujamsikia Chuji na Boban upande wao. Actually mimi ningependelea hawa wawili wakae kimya kwani tunajua what happened in Ivory Coast.

Maximo kaitenga timu na hakumchezesha Chuji eti mpaka semi finals kwakuwa alikuwa majeruhi wiki 8. Wakati huohuo cheti cha daktari wa timu kimempa clean bill of health - Chuji anacho hicho cheti. Vilevile Chuji alikuwa na watu wamekuja kumuona live michezo yake na walivyotaka kumuhoji kuhusiana na maswala ya kucheza nje ndipo Maximo akapiga marufuku kuwa hakuna ruksa kuongea na wachezaji bila idhini yake kwanza. Chuji alienda kuomba idhini na Maximo akamtolea nje. Usiku huo hakulala vizuri kiasi kwamba asubuhi alichelewa kuamka na kukosa mazoezi na hapo Maximo akasema Chuji ana utovu wa nidhamu amesusia mazoezi. Wakati huohuo kwenye mazoezi watu wanakwambia Chuji alikuwa mnyama, yaani a beast in practice, akipiga zoezi mpaka watu wanashangaa kwa nini hapangwi?

Baada ya matukio hayo Chuji akawa anajifua sana mwenyewe beach na alisikika akisema yeye sasa anajifua kwa ajili ya timu yake ya Yanga ktk kombe la klabu bingwa Afrika na ndiko ataonekana na kutoka huko. Habari hizi zilipomfikia Maximo ndia ikawa mwisho wa wao kuzungumza, manake hata kusalimiana Maximo hasalimii wala kumjibu!

Maximo has a lot to answer to and the sad fact is that he is being given the benefit of the doubt in this issue. Chuji anaonekana mvuta bangi tu lakini wote tunaopenda mpira tunajua uwezo wake kimpira, Bangi ni nini bwana? It is not even a Performance Enhancing Drug but a "social" drug that is known for ruining ones potential in the long run - for short time relaxation it is da bomb! Peter Tosh said it best - some lawyers, doctors, politicians etc smoke it. Sasa iwe Chuji?!

My suggestion to Chuji and Boban: let sleeping dogs lie!. Muacheni Maximo asemeeee weeee lakini si July anakitoa zake? Kocha anayekuja si atachagua timu yake bwana na si atawaona mchezo wenu?

Stay cool, my brothers, stay cool!!!!
 
Hebu usituchekeshe hapa, wewe ni lazima utakuwa ni komandoo wa Yanga.

Ati unasema hao wavuta bangi wakae kimya wasiseme, then wewe ndiyo unawaongelea badala yao. Tafuta kazi ya kufanya na wala siyo kuongelea mambo yasiyokuwa na mbele wala wa nyuma.
 
Watu wengine bwana........Kaaazi kwelikweli!!!!

Your rambling ndi umeona ya maana kumbe hakuna kitu! Niliyoandika hayasemi ni kwa niaba ya nani bali ni maoni yangu tu na nimeshauri wakae kimya na wasizue mtafaruki mkubwa. Au mwenzangu inglishi not richabo because I sincerely began the sentence with "I suggest......" Ooooops, sorry, nimeanza na sentensi inayosema "Napendekeza....."

Kwa jinsi hiyo basi naona wameamua kukaa kimya (kama nilivyopendekeza??) - sasa nani mwenye mayai usoni mwake??? Wewe!!!
 
Hivi wale ambao wanataka Maximo aendele wanataka atupeleke wapi? tasks zote alizopewa ameshindwa kuleta matunda. Ngoja niwakumbushe, kazi ya kwanza ilikuwa ni kutupeleka CAN kule Ghana, Maximo akachemsha. Akapewa challenge iliyofanyika Dar mwaka 2008, Maximo akatota, tukampa challenge ya Uganda... pale hata nusu fainali tulifika kimazingaombwe... Ndipo akapeleka timu CHAN na kutuahidi ushindi.... hakuna tuliloambulia zaidi ya mgogoro na nyota wake.

Ushauri wangu ni kuwa kwakuwa mwenyewe anataka kujenga timu ya baadaye, basi na apewe timu ya Vijana U17. Ajenge Stamina huko, apambane na suala la nidhamu huko hadi wachezaji waive.

Huku kwenye mashindano tumpe Kocha mwingine mzuri anayeweza kutupatia ushindi.

Wale wanaobeza mafanikio ya makocha wazalendo mimi siwaelewi hata kidogo. Kombe la Challenge Bongo tumepata mwaka 1994 chini ya Mziray. Abdala Kibaden ndiye Kocha pekee aliyeiwezesha Simba kufika Fainali ya CAF mwaka 1993. Mafanikio haya hayajavunjwa hadi hii leo.

Huyu Maximo wenu kila siku Presha itakuwa inapanda, Presha inashuka!!
 
Watu wengine bwana........Kaaazi kwelikweli!!!!

Your rambling ndi umeona ya maana kumbe hakuna kitu! Niliyoandika hayasemi ni kwa niaba ya nani bali ni maoni yangu tu na nimeshauri wakae kimya na wasizue mtafaruki mkubwa. Au mwenzangu inglishi not richabo because I sincerely began the sentence with "I suggest......" Ooooops, sorry, nimeanza na sentensi inayosema "Napendekeza....."

Kwa jinsi hiyo basi naona wameamua kukaa kimya (kama nilivyopendekeza??) - sasa nani mwenye mayai usoni mwake??? Wewe!!!

Unaweza kurudi kwenye thread yako na kusoma ulichokiandika? au unataka kunishawishi uliyoyandika ndiyo yanayoeleza jinsi ulivyo? Kama hivyo ndivyo basi na iwe hivyo!
 
Back
Top Bottom