Athumani Idd'Chuji' na Haruna Moshi'Boban' kujitoa stars | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Athumani Idd'Chuji' na Haruna Moshi'Boban' kujitoa stars

Discussion in 'Sports' started by Fidel80, Mar 3, 2009.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  VIUNGO wazoefu wa ushambuliaji wa timu ya soka ya taifa 'Taifa Stars', Athuman Idd 'Chuji' na Haruna Moshi �Boban� wamejitoa katika kikosi hicho kinachofundishwa na kocha Mbrazili, Marcio Maximo.

  Haruna kutoka Simba na Idd wa Yanga wamefikia hatua hiyo kutokana na kutoelewana na kocha huyo ambaye ameshindwa kuwapanga katika fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) ukiondoa Haruna ambaye alicheza mechi ya kwanza dhidi ya Senegal kwa dakika zisizozidi thelathini.

  Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata jijini hapa zinasema wachezaji hao wamejitoa Stars katika kipindi chote ambacho itakuwa chini ya Mbrazili huyo kwa madai kuwa amewadhalilisha baada ya kuwaweka benchi huku akitangaza kwa wananchi kuwa ni wagonjwa wakati ni wazima wa afya njema.

  "Chuji na Boban wanaonekana kama wakimbizi, wameamua kujitoa ingawa kuna wakati wamekuwa wakifikiria watu watawaelewa vibaya. Lakini jana (juzi Jumapili), wamekubaliana kuachana na Taifa Stars," alisema mchezaji wa karibu na wachezaji hao.

  "Wameona wakiendelea kuwa chini ya Maximo kamwe hawawezi kuisaidia Stars na yataendelea kuwa malumbano kwa kuwa tayari ameonyesha kinyongo dhidi yao na amekuwa hataki kuwachezesha lakini kila anapoulizwa na waandishi wa habari anazungusha maneno kibao bila ya kusema ukweli.

  "Boban na Chuji wamepanga kuwa wakifika Dar es Salaam walizungumzie suala hilo kwa undani, ndio maana unaona wamekuwa wakifanya mazoezi pekee yao baada ya Maximo kuwatenga. Unaona maisha yao kama juzi kawashusha kwenye basi tena mbele ya watu," alisema mchezaji huyo.

  Jumamosi usiku baada ya Stars kuwasili kwenye hoteli ya The President mjini Yaomossokro ikitokea Bouake ambako walimaliza mechi yao ya mwisho dhidi ya Zambia kwa sare ya bao 1-1, Maximo aliwataka wachezaji waliocheza na wale waliokuwa kwenye benchi kubaki kwenye basi.
  Bila ya kutaja majina alisema; �Wale waliocheza na waliokuwa kwenye benchi ndio wabaki kwenye basi tuzungumze."

  Hali hiyo iliwafanya Chuji na Boban wateremke kimya kimya na kupitiliza hadi vyumbani kwenda kujifungia. Lakini baada ya dakika 15, Maximo alifanya mkutano na waandishi wa habari na alipoulizwa sababu ya kuteremka wachezaji hao alisema kauli tofauti.

  "Unajua tumetoka sare, ambayo imetuathiri, huenda wachezaji wengine wana uchungu ndio maana wameshuka kwenye basi wanataka kujipumzisha, huwezi kuwakata na hakuna chochote kibaya," alijibu.

  Mwanaspoti iliwasaka Boban na Chuji kila mtu kwa wakati wake na kukiri kwamba walishushwa kwenye basi na Maximo. "Alisema waliocheza na waliokuwa kwenye benchi ndio wabaki kwenye basi, sisi tulikuwa jukwaani wakati wa mechi. Hakutaja majina lakini mtu mzima unaelewa huhitaji kusukumwa," alisema Boban na alipoulizwa suala la kujitoa kwenye timu alisema.

  "Nipo katika mazingira magumu sana, mimi huwa si mzungumzaji lakini wakati huu nitazungumza. Naomba unipe muda, kuna maamuzi ambayo nimefikia na nisingependa kuyaharakisha."

  Lakini kwa upande wa Chuji ambaye pia alikiri kuteremshwa kwenye basi, kuhusu suala la kujitoa alisema; "Uamuzi huo ni mzito, kama utakuwa umefikiwa unataka busara na ushauri. Lakini kuna ambacho nimefikia hata kama kuna ambao hawatapenda lakini sipendi kuendelea kuumia kama nilivyoishi huku Ivory Coast. Nitasema kila kitu baada ya kufika Dar es Salaam, ni vizuri kuyamaliza haya tukiwa nyumbani.

  "Unaniona niko huku, mimi ni kama askari ambaye nimekuja kutetea taifa langu. Lakini pamoja na kuwa na bunduki siruhusiwi kufyatua risasi wakati naona wenzangu wanashambuliwa. Inaniuma sana kweli, ila naomba uvumilie ikifika siku nitasema tu wacha nirudi nyumbani kwanza," alisema Chuji.

  Maximo alikataa katakata kwa mara nyingine kwamba kuna ugomvi ndani ya timu hiyo na kusisitiza kuwa suala la nidhamu anaendelea kulipa nafasi na yoyote ambaye hatataka kulifuata basi hatapata nafasi katika kikosi chake.

  Siku chache zilizopita alisema kikosi atakachochagua kwa mara nyingine kitajali damu mpya zaidi kwani amegundua majina hayana msaada.

  Bado chanzo cha tafrani la Maximo, Boban na Chuji hakijajulikana vizuri ingawa kila upande unaushutumu mwingine kwa kutokuwa na nidhamu au kuwa na dharau kwa upande mwingine.

  Wiki iliyopita Mbrazili huyo alitaka wachezaji hao warudishwe Dar es Salaam, lakini busara za Waziri, Seif Khatib ndio zilifanya wabaki baada ya kukataza mtu yoyote kurudishwa ingawa maamuzi ya mwisho ya kikao yalifikiwa kwamba kocha ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kama ataamua kuwapanga au kutowapanga uwanjani.

  Hii ni mara ya pili kwa Maximo kuingia kwenye tafrani kubwa na wachezaji mara ya kwanza ikiwa ni dhidi ya kipa Juma Kaseja ambaye amesusa kabisa kumuita katika kikosi chake huku akiwa hataki kutoa sababu za uhakika.

  Pamoja na ubora wake katika ufundishaji, moja ya kasoro kubwa ya kocha huyo imekuwa ni suala la kukasirika mara kwa mara na pia kuweka visasi kitu ambacho wadau wamekuwa wakimuasa kuachana navyo kwa faida ya kikosi chake.

  Habari za ndani zinasema kuwa Maximo amepanga kukivunja kikosi chake atakaporejea nchini na kwamba anataka kuunda kikosi kipya cha vijana wengi.
  Source;Mwanaspoti
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  WASIJE WAKALETA HABARI ZA 'MSEKWA'!........kustaafu uspika halafu mwishoni akaamua kurudi na kutetea kiti chake!

  Kwa hawa jamaa mi nahisi wameona ndo wanamalizikia kisoka!hawana namba za kudumu
   
 3. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Ataanza upya mara ngapi? Juzi tu alituambia Squad ya Stars ina wastani wa umri wa miaka 22 tu - saa vijana maana yake nini? Naona mambo yamemshinda. - huyu jamaa inaonekana ana personality problem pia (huko nyuma Kaseja na sasa akina Boban). Tumshukuru kwa alichofanya lakini nadhani imefika wakati sasa aonyeshwe mlango.
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hata ukiwa mwalimu mzuri lakini ushauriki unakuwa nothing.
  Ndio mwalimu ni mzuri lakini chuki binafsi dhidi ya baadhi ya wachezaji zinabomoa hatutafika mbele.Hawa wachezaji 2 ni wadhoefu na wamechangia kwa kiasi kikubwa kufika huko Ivory Coast leo hii kwa vile ameona amefika huko ana wadharau na kuto wachezesha na kutudanganya eti wanaumwa kumbe ana ugomvi nao.
  Huyu mwalimu tulisha sema hatufai mkataba ukiisha afungashe vilago arudi kwao huyu akienda London hatapewa hata timu ya daraja la 4 afundishe hapewi huyu.
   
 5. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mkuu inabidi ifikie watz tauchane na siasa za jangwni na msimbazi.......tuiongelee soka kitaalam zaidi......kumbuka timu kushinda hakuhitajikia mastaa wenye vipaji peke yake.....unakumbuka mwaka 2002 Scolari alimtema Romalio kwa kile hafai sio kiuchezaji ila hafai anaharibu timu..kinidhamu......

  ....badala yake akamchukua dogo wa PSG Ronaldo de Asis na mliona mambo yake.......hao boban kaseja nidhamu hakuna.....hawatufai timu ya taifa......

  ...Marcia kaitoa mbali timu yetu....mie nilishaisahau kabisa Stars sasa naweza hata kuvaa jezi ya stars mtaani......
   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...wakati umefika sasa wachezaji wa kiitanzania waache jeuri na majivuno eti tu kwakuwa wana majina makubwa...

  huyo CHUJI si ndiyo yule alokuwa kwenye sakata la Simba na Yanga? ...kuna kipindi wachezaji wanajiona wao ndio wao, kumbe maslahi ya taifa mbele kwanza, kama wanataka kuleta nyodo na majidai wakawafanyie wake zao nyumbani.

  Uwezo wenyewe kimpira hapo hapo Tanzania, kama wangekuwa mahodari si angalau ungesikia wanag'ara japo as pro's kwenye nchi (za kiafrika) mpira uloendelea.

  Watanzania tukitaka mafanikio, basi tuanze kuwalaani wachezaji kama hao kina Boban na Chuji kwa kuunda cohesive group within a National Team ili wapate preferrential treatment, ambayo kwa namna moja au nyingine inaua morale ya wachezaji wengine.

  Ujinga huu ndio uliokuwa unawaponza kina Mziray enzi hizo wanafundisha team zetu, ushikaji mbaya kwenye maslahi ya klabu na taifa...!
   
 7. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa ni biashara ya kuangalia mchezaji anataka nini basi kusingekuwa na kocha na isitoshe kocha ndio mwenye kujua nani ni nani na nani anafanya nini uwanja kwa uwezo wake kulingana na mchezo wenyewe unavyokwenda. Licha ya hivyo isitoshe anachonifurahisha Maximo akishaona mchezaji unatembea mabega juu anakumwaga tuuu. Sifa kwake ni kama hazina nafasi.
   
 8. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,270
  Likes Received: 4,247
  Trophy Points: 280
  Hao jamaa ndio wale ambao hawawezi kucheza bila kuvuta bangi
   
 9. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Sawa Mkuu, ni kweli ametutoa mbali. Ila issue ni kwamba kuna fighting talk in Taifa Stars dressing room na inaonekana yeye ndiye tatizo. Ni hulka yetu waTz kutopenda mabadiliko. Tusimng'ang'anie tu kama tunavyoing'ang'ania CCM ilivyotutoa mbali https://www.jamiiforums.com/images/smilies/confused.gif
  :confused:.
   
 10. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Mkuu, Bangi isiwe big issue. Wengi tu wanavuta/walivuta ktk umri huo - Michael Phelps, Obama etc.
   
 11. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mkuu nidhamu kwanza kocha kazi yake sio kufundisha mpira uwanjani tu....kama unafatilia wachezaji wa ulaya wakiharibu nje ya uwanja mtaani kwao au bar kocha akisikia anakula benchi......fuatilia Gerrad na Terry wakti fulani walilewa wakaharibu ile mbaya club.....

  .....kwenye michezo ipo sana Dikembe Mpolondo Mukamba Jean-Jacques Wamutombo aliwakiana na kocha wake na kumuambia "yeye he is 40yrs old......." kocha hakujali ni best brocker akamlima benchi......mkuu nidhamu kwanza....

  Unataka mabadiliko yepi mkuu stars zaidi ya haya yanaondelea.....yaani tatizo kamtosa kaseja ksia nidhamu ndio mnamuona hafai?....hivi mkuu unajua marcio kaijenga sana timu ki proffesional ndio maana hata wakina henry joseph wanaonekana na mawakala....

  ....anyway ukiambiwa uchague kocha mbadala wake utamchagua nani? sababu lazima uwe an suluhisho la kutomtaka Marcio Stars
   
 12. e

  edops New Member

  #12
  Mar 3, 2009
  Joined: Feb 16, 2008
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maximo siku siku zako zinahesabika stars.maana sasa imekua too much.baada ya kaseja sasa umeamia kwa boban na chuji. hakuna mtu hasiye jua tabia yako umekua mtu wa kuigawa stars sana ingawa stars inashinda simply coz of juhudi binafsi.
   
 13. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Loh .. jina kama sentensi!

  OK nakubaliana kuhusu nidhamu ya wachezaji. Ila makocha nao huwa wanakuwa evaluated na ikibainika kwamba wao ndiyo tatizo waonyeshwa milango. Mifano mingi tu

  Kuhusu kocha mbadala tunaweza kutumia procedure zile zile tulizotumia kumpata Maximo na tukampata kocha mzuri tu.
   
 14. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  sidhani......njia iliyotumika ndio imempata Marcia ambae humtaki......njia nyingine pls....na kocha mwingine unaweza kuanza sasa fulani anafaa kuwa kocha wetu.......anza sasa..
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Inatakiwa makosa wanayo fanya waachezaji yawe yanawekwa wazi.
  Kila mpenzi na shabiki wa soka ajue lakini hapa tunaona kama kuna harufu kauonevu flani hivi kutoka kwa kocha sasa hapo lazima tukomee si wadau wa soka....kwani hao akina Gerrard hawakuonywa na wakaonyeka?
   
 16. J

  James J Member

  #16
  Mar 3, 2009
  Joined: Jan 13, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mimi naona uwezo wa Maximo umefika kikomo hana jipya tena ni wakt mzuri wa kutafuta kocha mwingine ambaye atakuja na mbinu mpya,ni ukweli usiopingika kwamba Maximo anaigawa stars sana,kuna baadhi ya wachezaji anakumbatia ilihali uwezo wao mdogo compare to others players ambao maximo hawataki kabisa.NI VIZURI TUTAFUTE KOCHA KUTOKA ULAYA TUACHANE NA HAWA WA BRAZIL.
   
 17. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 135
  Tatizo hapa kwa vijana wetu inaonekana ni nidhamu, wamezoea panga pangua kwenye vilabu vyao ni lazima wacheze na wana jeuri ya kufanya kile wanachotaka bila kujali kocha anasema nini na huu ujinga ndio wanataka waundeleze kwenye timu ya taifa. Kuwa na kipaji cha mpira tu haitoshi kukufanya uwe mchezaji bora, nidhamu ni element kubwa sana kwa wachezaji waliofanikiwa duniani. Nidhamu ya Stam na Van Nielstroy ilipopungua kule Trafford walitimuliwa japokuwa viwango vyao bado vilikuwa juu, nidhamu ya Adriano iliposhuka kule San Siro aliozea bench.....bila nidhamu ni vigumu kwa mchezaji kufundishika na hakuna mwalimu ambaye atataka mchezaji ambaye hamuheshimu kwenye kikosi chake. Kuna tetesi kwamba hawa jamaa wao wanajiona ni 'mafaza' wa timu, mwalimu akiwapa maelekezo ya namna ya kucheza wao hawayafuati, wanataka wacheze 'kimtaani' kama wanavyojua wao, hata kama mimi ndo ningekuwa kocha nakumwaga hakyanani!
   
 18. Kireka1980

  Kireka1980 JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2009
  Joined: Mar 18, 2008
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  huyo Maximo kwa sapoti anayoipata na mwamko uliopo timu ilitakiwa ifanye vzr zaidi, sio kila siku kikosi kipya
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyu Maximo angekuwa anafanya kazi mazingira magumu kama makocha wa Majimaji,Polisi Dom,Simba,Yanga,Manyema sijui timu zingekuwaje?
   
 20. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 1,016
  Trophy Points: 280
  Maximo anatakiwa kuwatambua wadau wa soka na kuhakikisha maslahi ya wadau yanatimia, sasa wachezaji ni wadau na wana maslahi pia cocher ni zaidi ya mwalimu sasa Maximo ana behave kama mwalimu wakati anapewa vinaja awacoach.

  Si sahihi kusema mafanikio ya stars yanaletwa na Maximo, yeye ni mdau mmoja wapo katika kundi la wadau na hakubali na lawama pia. huyo Jk aliyemleta analaumiwa kila kukicha ndio itakuwa Maximo bwana, amebwagwa Big Phil wakati timu ni ya Tatu katika msimamo. Lakini wabongo tunaambiwa tulidhike na kufungwa, kudroo na kushinda game moja hata kama tuna mtazamo tofauti hii haipo mpira unanoga kama kuna wanao pinga, sio siasa kusema ndio mzee kila siku.

  Kwa mazingira ya sasa Tanzania inastahili kuwa mbali zaidi ya ilipo, hata ushindi wenyewe sio predictable kama zilivyo timu za wenzetu. Ukilinganisha na majirani zetu sisi ndio tumewekeza zaidi katika timu ya taifa na hata ligi kuu, tunawazidi hata kenya katika matumizi wakati uchumi wetu ni mdogo lakini kiwango chetu ndio cha chini. tukisema mnalinganisha na miaka 18 iliyopita tena mnafunika hata historia kwamba mashindano yale ya mwaka 1982 ilikuwa CHAN ya ukweli sio hii ya wachezaji wa ndani.

  Lakini mnakuwa wakali mkiambiwa bongo bado, si tunaona wakicheza sifa hazikutosha kutupeleka nusu fainali na Afrika mashariki ndio tumechezea kichapo hata cha wasomali. Pesa inayoenda stars ni nyingi kuliko kinachopatikana huko, uliza hata zambia wametumia ngapi ndio mjue Tanzania wanapiga hela na kugombana. Kama bangi wachezaji wengi wa kibongo wanakula jani na sio kigezo cha mwalimu kuchuniana na wachezaji kama vipi si awafukuze yeye si ndio kawaita anaogopa nini sasa.
   
Loading...