Atheism: Imani nusu na robo


Mkuu unavyoongea ni kama vile una~assume jamaa assumptions zao zote ni za uongo, ila nikuulize kitu, una uhakika gani kua wenye imani ndio wako correct? kwa kifupi kila mtu anaamini anachokiamini ila ukweli ni kwamba hakuna mwenye 100% proof kua anachokiamini ndicho cha kweli.

Waislamu wanaamini kwa mtume, Wakristo wanaamini Yesu, Wahindi wapo wanaoamini ng'ombe, Wachina wapo wanaoamini Buddha, kuna dini zaidi ya 1000, na miungu zaidi ya 5000. Kila moja ya wafuasi wa hizi dini anaamini mungu wake ndiye wa kweli, anayeamini kwa Mungu moja yeye ana uhakika gani kua wa kwake ndiye wa kweli? Sanasana tunaongea lakini ukweli unabaki palepale, wengi tumeshika dini fulani kwa kua tumezaliwa na kukulia huko, ila ingekua mtu hufundishwi dini hadi ufikir umri labda miaka 18, leo hii dini ingeonekana kama story za The Avengers tu.

Cha muhimu ni kuheshimiana na kua tolerant, vitabu vingi vya dini vina mambo mazuri ndiyo, lakini vinayo mabaya pia, vipo vinavyoruhusu mauaji ya binadamu mwenzako, vingine vinaruhusu slavery, mambo ya kutoa kafara, ni vitu vya ajabu na watu watatafuta kila explanation kuziba huo ukweli ila ukweli uko palepale. Hivi vita hamtovimaliza, vilikuwepo zaidi ya miaka 2000 iliyopita, leo mnachofanya ni kurudia tu ila hamna kipya chochote, atakayekuja kuprove haya ni Mungu tu kama atajitokeza kweli au kama hatokuja kutokea milele then atakua hayupo ila hiyo milele sasa wengine hatutokuwepo by then kwa hiyo hatutojua, labda miaka 10,000 ijayo bado tu watakua wanamsubiri.
 
Mimi nimepractice atheism kwa miaka 2, nimeishi nao 24/7 katika kipindi chote hicho kwahiyo nilipoweka hii mada niliweka kwa maana kamili
 
Mimi nimepractice atheism kwa miaka 2, nimeishi nao 24/7 katika kipindi chote hicho kwahiyo nilipoweka hii mada niliweka kwa maana kamili

Hehehe mshana naweza kuchukulia serious kwenye mambo ya siasa ila tukija kwenye imani mimi hunidanganyi, wewe umepractice atheism 2 years, mara ulitoka kusema umesomea uchawi ukatudanganya na picha za harry potter, nimeona post zako nyingi tu ni pure fairy tales hazina ukweli wowote. U cannot prove anything, u-atheism wako unaongelea kuingia google na kutafuta anything related, nothing more
 
Aisee kwahiyo mtu akisomea kitu kimoja hawezi kusomea kingine? You can't be serious with what you just wrote...as a GT ulitakiwa kuniuliza nimesomea wapi lini na akina nani...ningebabaika kukujibu ndio ungekuja na blah blah kama hizi
Kumbuka hii sio mada yangu ya kwanza kuhusu atheism ngoja niitafute ile nyingine nikuwekee hapa hapa kisha unichagize kwa hoja na sio sifa binafsi tafadhali
 
GRAPH wewe ni Ze akili Kubwaz
 
Mimi ni mmojawapo wa wale tusioamini uwepo wa Mungu' ila nilikulia kwenye imani ya kikristo tena wale walokole wa kunena kwa lugha... baada ya kufika umri wa kujitambua,nikajikuta napenda tuu kuchunguza kila kitu kinachohusu dini... hiyo ikanifanya niufuatilie kwa karibu sana uislamu. Kiukweli kabisa ukisoma kwa umakini biblia na quran utagundua kwamba hakunaga MUNGU kabisa yaniii... Na hivi karibuni nikaifuatilia imani ya BUDDHA na hapo ndo nikagundua kwamba mabuddha ni watu wanaojitambua hapa duniani.
 
Umewahi kuona au kucomprehend ukubwa wa hizo sayari na namna zinavyozunguka kwenye njia zake, una evidence kwamba maji ya bahari yamekaa kwenye eneo mfano wa jagi in relation na nchi kavu na kwamba hakuna nguvu nyingine yoyote inayohitajika kuyazuia
Yaani we jamaa ni mgumu wa kuelewa sana, ukubwa wa hizo sayari kaangalie machapisho ya NASA...kumbe hujui hata bahari ni nini? na haya maswali yako yanahusiana vipi na mada?...kweli Africa ni dark continent.
 
Cha kushangaza sana ni kwamba itafika muda utarejea kwa huyu usiyemwamini sasa...mimi nimepractice mpaka satanism na kila imani miliyojaribu mwanzoni ilionekana nzuri na sahihi sana lakini kadiri unavyoenda deep ndio unavyozidi kukutana na mikanganyiko hasa kama unapenda kushughulisha akili
 
Sawa mkuu...ebu nipe maana ya neno Kilingeni..kabla ya kuanza mjadala,...Siyo neno la kipare kweli.
Mkutano/kusanyiko la watu wa kaliba fulani wanaokutana kwa jambo mahsusi sio siasa lakini
Hiki sio kipare ni kiswahili
 
Mkuu dini inafunga akili za watu na kuwatisha ili wasiwe wadadisi...hivyo kuwa chini ya kitu kisichokuwepo na kuwa watumwa kabisa....Ni vigumu sana kwa mtu mwenye uelewa mzuri na mdadisi akaendelea kuamini dini...Huyo Mungu ni wa namna gani mbona hajidhihirishi kwa watu wake na kumaliza malumbano?
 
Mkuu upo sawa kabisa.Kinachofanya watu wang'ang'anie dini zao ni kwa sababu mbili, kwanza walifundishwa wakiwa wadogo kabla akili yao haijashika vitu vingi...pili walipewa vitisho kwamba wasipofuata hizo dini wataingia motoni....Kuna watu waliishi wakiamini kuwa Yesu angerudi/kiama kingefika wakiwa hai lakini walikufa bila kuona chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…