Athari za Nyota katika Mahusiano ya Kimapenzi

Jack HD

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
737
1,000
Amani iwe juu yenu!!


Tuanzie hapa!!
Unajimu ama Astrolojia ni elimu juu ya uhusiano kati ya nyota na maisha ya binadamu duniani. Wanazuoni wa unajimu wanaeleza ya kwamba nyota zinaathiri maisha ya watu na matukio mbalimbali kwenye maisha yetu ya kila siku.

Tutakuwa washuhuda kusema kuna nyota nyingine kweli zinaendana kuliko nyota nyingine na watu wa nyota zenye mahusiano fulani wakiwa wapenzi ni rahisi kuwa na mapenzi ya kudumu kuliko wengine. Mara kadhaa tumeshasikia ule usemi mtu anakuambia "mimi na Fulani tunaelewana sana itakuwa tu nyota zetu zinaendana"

Kama nyota hizi zinauwezo wa kuathiri maisha ya watu, kwa hiyo tutakubaliana wote kuwa kuna umuhimu wa kuconsider nyota ya mtu kabla ya kuanza mahusiano ya kimapenzi. Katika maisha ya ndoa pia mara kadhaa watu wanapoanguka ama kufanikiwa kimaendeleo huweza kuhusishanisha na nyota ya mwenzi wake.

Sasa swali ni je, Kuna athari zozote zenye kuletwa na masuala ya nyota kwenye mahusiano ya kimapenzi? Kuna ulazima gani kufuatilia nyota ya mtu kabla hamjakuwa serious na mahusiano yenu? Nafasi ya nyota kwenye kuathiri maendeleo ya mahusiano ikoje?

Karibuni tujadili na tuelimishane.
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
6,691
2,000
Watu wa Asia wanatumia sana nyota kwenye mahusiano yao.Nasikia zina faida sana kama nyota zenu zitaendana na ni mbaya sana kama mtatofautiana nyota
 

APEFACE

JF-Expert Member
Oct 1, 2016
3,438
2,000
Angekuwepo Yahaya angetusaidia kwa hii ishu...nnavoskia nyota kuna zenye asili ya UDONGO,MAJI,UPEPO,NA MOTO eti upepo inaendana na moto alafu udongo inaendana na maji,
Moto-Kondoo,Simba,Mshale
Maji-Ng'e,Samaki,Kaa
Upepo-Mapacha,Mizani,Ndoo
Udongo-Ng'ombe,Mashuke,Mbuzi

1.Aries-March 21-April 19 (Punda/Kondoo)
2.Taurus-April 20-May 20 (Ng'ombe)
3.Gemin-May 21-June 20 (Mapacha)
4.Leo-July 23-August 22 (Simba)
5.Virgo-August 23-September 22 (Mashuke)
6.Libra-September 23-October 22 (Mizani)
7.Sagittarus-November 22-December 21 (Mshale)
8.Capricon-December 22-January 19 (Mbuzi)
9.Cancer-June 21-June 22 (Kaa)
10.Pisces-February 19-March 20 (Samaki)
11.Scorpion-Oct 23-November 21 (N'ge)
12.Aquarius January 20-February 18 (Ndoo)

wanaojua zaidi watusaidie.....................
 

Jack HD

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
737
1,000
Angekuwepo Yahaya angetusaidia kwa hii ishu...nnavoskia nyota kuna zenye asili ya UDONGO,MAJI,UPEPO,NA MOTO eti upepo inaendana na moto alafu udongo inaendana na maji,
Moto-Kondoo,Simba,Mshale
Maji-Ng'e,Samaki,Kaa
Upepo-Mapacha,Mizani,Ndoo
Udongo-Ng'ombe,Mashuke,Mbuzi

1.Aries-March 21-April 19 (Punda/Kondoo)
2.Taurus-April 20-May 20 (Ng'ombe)
3.Gemin-May 21-June 20 (Mapacha)
4.Leo-July 23-August 22 (Simba)
5.Virgo-August 23-September 22 (Mashuke)
6.Libra-September 23-October 22 (Mizani)
7.Sagittarus-November 22-December 21 (Mshale)
8.Capricon-December 22-January 19 (Mbuzi)
9.Cancer-June 21-June 22 (Kaa)
10.Pisces-February 19-March 20 (Samaki)
11.Scorpion-Oct 23-November 21 (N'ge)
12.Aquarius January 20-February 18 (Ndoo)

wanaojua zaidi watusaidie.....................
Umegusia juu juu mkuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom