Athari ya Madawa ya Kulevya ni Kubwa Sana

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,373
6,084
Tatizo la madawa ya kulevya hapa nchini ni kubwa sana kuliko watu wengi mnavyofikilia. Tanzania na ukanda wa Afrika mashariki ndio imekuwa ndio vituo vikubwa vya kupitiza na kusafirisha madawa ya kulevya kwenda sehemu mbalimbali duniani.

Nampongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar Makonda kwa vita hivi ingalau kwasasa inagusa watumiaji tu. Leo magereza mbalimbali duniania kuna vijana wa,kitanzania wamefungwa na wengi wao ni wasafirishaji serikali ingetuma maofisa kutoka muungano wa vitengo mbalimbali hapa nchini waende kutembelea wafungwa hao,kupata maelezo ya nani ndio wadhamini wao katika biashara ya madawa ya kulevya.

Wafanyabiashara wa madawa ya kulevya wanajulikana na hata mali wanazomiliki zinajulikana kwani mtu hawezi kuwa hana biashara lakini ana gari la milioni 300. Serikali ya Marekani kupitia kitengo chake cha kupambana na madawa ya kulevya (US Drug Enforcement Administration ) imeamua kutoa msaada kwa nchi ambazo zimeamua kupambana na wafanyabiashara wa madawa hayo, hivi majuzi huko nchini Kenya imewatia nguvuni vijana wa Akasha ambao walikuwa ndio wafanyabiashara maarufu,nchini humo na kuwapeleka Marekani ili wafunguliwe mashitaka ya kufanya biashara hiyo na wanategemewa kufungwa maisha. Na serikali ya Mexico baada ya kusumbuliwa na mfanyabiashara maarufu wa Madawa hayo ya kulevya Joaquin Guzman waliamua kumpeleka Marekani ili ashitakiwe huko, huyu jamaa kwa ushawishi wa pesa zake alitoroka jela mara mbili.

Serikali inatakiwa kuungwa mkono kwenye vita hivi kwani tusipoangalia tutakuwa na vijana wengi kwenye majela nchi mbalimbali na vijana wetu hapa nchini watazidi kutumia madawa hayo ya kulevya ambapo watazidi kudhurika. Rais wa Philippines Duterte ametangaza vita dhidi ya madawa ya kulevya kama janga la kitaifa.
 
Back
Top Bottom