ATCL Yasitisha Safari zake

ATCL Yasitisha Safari zake

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
1,710
Reaction score
3,685
Katika hali isiyotarajiwa Shirika la Ndege Tanzania(ATCL) lenye ndege aina ya Boeing 735 lililokuwa linafanya safari kati ya Dar-Mwanza via K'njaro na Dar-Hahaya(Comoro) limesitisha safari zake hivi leo Asubuhi. Habari nilizozipata kwa jamaa yangu aliyekuwa asafili na ndege hiyo leo asubuhi ni kuwa abiria wote wa ATCL waliokata ticket kwenda Mwanza "wamefaulishwa" ktk ndege ya 540.Com aina ya CRJ.

Kwa habari ya chini ya kapeti ni kuwa ATCL imeshindwa kulipa malipo ya kukodi kwa kampuni ya AEROVISTA ilipoikodi Ndege hiyo,kampuni husika imeizuia ndege yake kuruka mpaka hapo itakapolipwa malimbikizo ya madeni yote na ATCL. Hii inatokea siku moja baada ya Wizara ya Uchukuzi kuwasilisha Bajeti yake ktk Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
This thing was breathing on life support for a long time,now its about time it dies and saves us from all unnecessary outlays.
 
ATCL tunaipenda,tunaiheshimu sana ila madai ndio yapo juu ya uwezo...
 
ATCL tunaipenda,tunaiheshimu sana ila madai ndio yapo juu ya uwezo...
napenda sana kuiona nchi yangu ikiwa na flag bearer huko angani lakini ndio hivi tena!

Tunabaki kuleta visingizio kama ilivyo kawaida yetu na kuishia kusema 'hujuma' na mengineyo. Nimemuona Mzee Shirima juzi wakati wakifungua karakana ya ndege za PrecisionAir akimueleza kwa uzuri kabisa JK juu ya serikali kununua shares zao ili wapate nguvu zaidi. Alimpa mfano wa KQ kuwa sio kuwa inamilikiwa moja kwa moja na serikali bali wana shares tu lakini linasaidia kuongeza idadi kubwa ya watalii nchini Kenya.

Binafsi kwa mfumo wa serikali na utawala uliopo TZ kwa sasa sioni njia yoyote ya kuikwamua ATCL huku ikijiendesha bilia kuendeshwa na serikali. Na je, kama rais mwenyewe anakili hadharani kuwa serikali haina uwezo wa kuwaongezea mishahara walimu wanaolipwa Tsh. 200,000/- (sio US $200,000) kwa mwezi itaweza kuliendesha hili shirika!?

Serikali lazima ipange vipau mbele vyake kulingana na uwezo wa mapato ya nchi na siyo kuiga KUNYA KWA TEMBO!
 
Kama Serikali inaona kuna ugumu kwa wao kununua hisa Precision Air,basi Precision wanunue hisa katika ATCL tena wawe na majority shareholding.Sijui kigugumizi kiko kwa nani? Govt au precision?
 
Nakubaliana na Ileje 100%. Serikali iachane kabisa na biashara hii kwa sasa. Acheni Precision na wengine waendelee. Sioni ATCL inatusaidia nini. Is the flag too heavy to bear?
 
napenda sana kuiona nchi yangu ikiwa na flag bearer huko angani lakini ndio hivi tena!

Tunabaki kuleta visingizio kama ilivyo kawaida yetu na kuishia kusema 'hujuma' na mengineyo. Nimemuona Mzee Shirima juzi wakati wakifungua karakana ya ndege za PrecisionAir akimueleza kwa uzuri kabisa JK juu ya serikali kununua shares zao ili wapate nguvu zaidi. Alimpa mfano wa KQ kuwa sio kuwa inamilikiwa moja kwa moja na serikali bali wana shares tu lakini linasaidia kuongeza idadi kubwa ya watalii nchini Kenya.

Binafsi kwa mfumo wa serikali na utawala uliopo TZ kwa sasa sioni njia yoyote ya kuikwamua ATCL huku ikijiendesha bilia kuendeshwa na serikali. Na je, kama rais mwenyewe anakili hadharani kuwa serikali haina uwezo wa kuwaongezea mishahara walimu wanaolipwa Tsh. 200,000/- (sio US $200,000) kwa mwezi itaweza kuliendesha hili shirika!?

Omujubi!

Uko sahihi tatizo ni Serikali na haswa huyo Mwakyembe anaota ndoto ya kuwa na National Carrier . Yeye na Dhaifu is another bunch of nicompoops . Kenya hawana national carrier Kenye Airways inayorusha ndege karibu duniani kote ni a Private Company na serikali ya Kenya inazo hisa only 23% .

It's quite simple Serikali inunue hisa PA na kutumia hiyo opportunity. Huwezi kodisha ndege moja halafu ukategemea ikutoe. Tulikuwa na Air Tanzania ikauwawa na Watanzania na hakuna aliyepelekwa Mahakamani but the dream goes on and on.

Wakati Dhaifu anazindua Hanger ya PA alipewa hiyo offer na Shirima lakini akitokea Mwakyembe aka sema dhamira ya kufufua ATC iko pale pale. Nadhani Mwakyembe ni Mkristo na anajua from the bottom of his heartbeat that hakuna kitu kilichowahi kufa kikafufuka ila yasemekana Yesu Kristo alifufuka I can't dispute that kwani wengi wanaamini.

Kufufua ATC under CCM is an impossible mission kwani it's still the same level. Just like watu Fulani wanafikiria kufufua JKT?

Simple solution lets jump at the offer ya PA tununue hisa tusonge mbele! Hizi ngonjera za kuanzisha Chuo cha air hostess is another failed CCM conception.
 
Hao aerovista hawajui kuwa madai yao HAYATEKELEZEKI
 
Kwani ni lazima kila nchi iwe na shirika la ndege hata kama uwezo wa kumiliki ndege haina? Inakuwaje tunakodisha ndege kwa pesa zote hizo ilihali shirika linaoparate kwa hasara? Just imagine shirika lilipokuwa na ndege 2 lilikuwa na wafanyakazi 500. Ilipobaki moja likapunguza wafanyakazi an kubakia 300. Majuzi tumepata haka kakukodisha, shirika likatangaza ajira mpya! This is typical insane. Serikali iachane na habari ya ndege ilimradi za kuwasafirisha viongozi zipo so far niwatanzania wangapi wanatumia usafiri wa ndege? Nadhani Precision, fly 540, na mashirika mengine kama coastal, flylink, auricair yanatosha kusaidia kuwasafirisha watanzania na pesa ya kukodisha ndege ikatumiaka kurejesha na kuboresha reli na treni ya kati ambayo ndiyo inamsaada mkubwa kwa watanzania kuliko hiyo boeing ya kuazima inayotufilisi!
 
Ni upepo tu, utapita halafu mdeni wetu atasahau kiaina!
 
Katika hali isiyotarajiwa Shirika la Ndege Tanzania(ATCL) lenye ndege aina ya Boeing 735 lililokuwa linafanya safari kati ya Dar-Mwanza via K'njaro na Dar-Hahaya(Comoro) limesitisha safari zake hivi leo Asubuhi. Habari nilizozipata kwa jamaa yangu aliyekuwa asafili na ndege hiyo leo asubuhi ni kuwa abiria wote wa ATCL waliokata ticket kwenda Mwanza "wamefaulishwa" ktk ndege ya 540.Com aina ya CRJ.

Kwa habari ya chini ya kapeti ni kuwa ATCL imeshindwa kulipa malipo ya kukodi kwa kampuni ya AEROVISTA ilipoikodi Ndege hiyo,kampuni husika imeizuia ndege yake kuruka mpaka hapo itakapolipwa malimbikizo ya madeni yote na ATCL. Hii inatokea siku moja baada ya Wizara ya Uchukuzi kuwasilisha Bajeti yake ktk Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hapo kwenye red...chini ya kapeti tena...WEWE BENI...Hachawafilizike zao banaaaa
 
kwa serikali hii ATCL ni kama malaria ,,,kampeni nyingi wachache wanufaike
 
Kwani ni lazima kila nchi iwe na shirika la ndege hata kama uwezo wa kumiliki ndege haina?
Kwa mazingira haya ya ATCL hakuna ulazima hata kidogo wa kuwa na hiyo kitu. Tatizo ni kuwa viongozi wetu wanafanya mambo kwa kutafuta sifa zaidi na si kwa kuangalia faida na uhalisia wajambo lenyewe
 
naona hili swala haliko mahakamani hivyo linaruhusiwa kujadiliwa
mh spika naomba muongozo kama inaruhusiwa kujadilia sakata la atcl wakati bajeti aijapitshwa??
 
kwani ni lazima kila nchi iwe na shirika la ndege hata kama uwezo wa kumiliki ndege haina? Inakuwaje tunakodisha ndege kwa pesa zote hizo ilihali shirika linaoparate kwa hasara? Just imagine shirika lilipokuwa na ndege 2 lilikuwa na wafanyakazi 500. Ilipobaki moja likapunguza wafanyakazi an kubakia 300. Majuzi tumepata haka kakukodisha, shirika likatangaza ajira mpya! This is typical insane. Serikali iachane na habari ya ndege ilimradi za kuwasafirisha viongozi zipo so far niwatanzania wangapi wanatumia usafiri wa ndege? Nadhani precision, fly 540, na mashirika mengine kama coastal, flylink, auricair yanatosha kusaidia kuwasafirisha watanzania na pesa ya kukodisha ndege ikatumiaka kurejesha na kuboresha reli na treni ya kati ambayo ndiyo inamsaada mkubwa kwa watanzania kuliko hiyo boeing ya kuazima inayotufilisi!
escobar
umeniacha hoi siku naona alinitumia msg kaka mmoja kuniuliza hivi lazima nioe na mimi kaka??
Nikiangalia na hapo juu nasubiri mwongoozo wa kujibu kuptia kifungu cha jf no25 kipengele z/j
 
Back
Top Bottom