ATCL kujigamba kuhudumia wateja 60,000 kwa mwezi ni failure. Ni wazi kuwa ndege nane zilinunuliwa kwa cash bila kufanya tathimini yakinifu

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Hivi kwa akili za kawaida unaweza kujisifia kuhudumia watu 60,000 kati ya watu mil 60? Na wewe ukatoka kifua mbele kuwa uko vizuri! Kwamba eti soko lako limekua? Hii ni aibu kubwa.

Nilitegemea sababu hii nchi ipo uchumi wa kati basi mje na idadi ya watanzania mil 15 ambao wana uwezo wa kulipia tiketi ya laki 3 kutoka Mza kwenda Dar. Lakini taifa lina watu mil 60. Watu elfu 60 kwa kwa mwezi wanapanda ndege mnajisifu huu ni mdhaha.

Kwa kweli ni kuwa hii Atcl ya mr Matindi imefufuliwa kisiasa na wala sio kusaidia taifa kiuchumi. Maana kama unafufua shirika la ndege kwa kununua ndege nane cash lazima uhakikishe raia wako watapanda hizo ndege kwa bei nafuu. Ok je, soko la nje zitamudu?

Ni wazi kuwa kufanya maamuzi kwa kukurupuka hayafai. Leo hii tumenunua ndege,hatuwezi kuzipanda wala hakuna dalili za kuongeza pato la taifa.
 
Subiri tumalizie kutunga kitabu cha Historia ya Tanzania, Ndege nane lazima tuzitaje ndani watoto wetu wazijue kwanza hadi kule vijijini.

Uzalendo mbele kwa mbele kutambulisha raslimali za nchi
 
Abiria 60,000 ÷ ndege 8 = 7,500 kila ndege inabeba abiria 7,500 kwa mwezi.

7,500 ÷30 =250. Kila ndege inabeba abiria 250 kwa siku.

Analysis hii ndio itawaumbua. Hakuna ndege itakayobeba abiria 250 kwa siku kwa sababu hata hizi ndege zenye seats 72, mara nyingi hazina hata abiria 50 kwa safari moja. Na hapo hapo bado wanapambana na precisionair - hizi taarifa za kupika tu!!
 
Hivi kwa akili za kawaida unaweza kujisifia kuhudumia watu 60,000 kati ya watu mil 60? Na wewe ukatoka kifua mbele kuwa uko vizuri! Kwamba eti soko lako limekua? Hii ni aibu kubwa.

Nilitegemea sababu hii nchi ipo uchumi wa kati basi mje na idadi ya watanzania mil 15 ambao wana uwezo wa kulipia tiketi ya laki 3 kutoka Mza kwenda Dar. Lakini taifa lina watu mil 60. Watu elfu 60 kwa kwa mwezi wanapanda ndege mnajisifu huu ni mdhaha.

Kwa kweli ni kuwa hii Atcl ya mr Matindi imefufuliwa kisiasa na wala sio kusaidia taifa kiuchumi. Maana kama unafufua shirika la ndege kwa kununua ndege nane cash lazima uhakikishe raia wako watapanda hizo ndege kwa bei nafuu. Ok je, soko la nje zitamudu?

Ni wazi kuwa kufanya maamuzi kwa kukurupuka hayafai. Leo hii tumenunua ndege,hatuwezi kuzipanda wala hakuna dalili za kuongeza pato la taifa.
Cc; barafu
 
Twende tararibu...unataka abiria 15m kwa mwezi?

Scenario no 1 Kwa Mwezi abiria 15m

Hawa ni sawa na abiria 20,833 kwa saa 1 (15m / 30days*24hrs).

Kama una fleet ya boing 787 km zetu zenye seat configuration ya abiria 266 tutahitaji ndege 78 kwa wakati mmoja ziwe angani? Swali ni Je tunazo hizo Ndege? Je viwanja vyetu vinaweza kuhudumia hao abiria 20,833 kwa saa? Kumbuka abiria 20,833 km ni mabasi ya siti 60 ni mabasi 347 kwa Saa sidhani km hawa abiria hata pale Ubungo hawapo.

Scenario no 2 ya abiria 15m kwa Mwaka.
15m/(365days×24hrs)...sawa na abiria 1712 kwa saa or boeing 6 ziwe hewani kwa wakati mmoja...or Boing @2 hewani abiria 532( 266x2) + Airbus @2 abiria 264 (132x2) + Bombadier Dash 8-Q400 @4 abiria 280 (70x4) for a total of 1076...hapo kuna abiria 636 watakosa usafiri (1712-1072).

Hapa bila kuangalia factor kua Bombadier imatumia zaidi ya lisaa sehem km Mwanza.

Ktk Scenario zote mbili Wishes za mtoa mada haziwezi kufikiwa hata kama watanzania wana pesa still hatuna Miundo Mbinu wala Ndege za kutosha kuwasafirisha na watu wanapinga serikali kuongeza ndege.

Ushauri wangu next time mtoa mada kabla hujaandika uzi tafadhali fanya uchambuzi wa kutosha kuliko mkurupuko huu ulioufanya.
 
Mtoa post huna kitu kichwani ingefaa uje na takwimu za shirika kwa miaka 10 au mitano ilopita kisha ulinganishe na sasa kwa kuzingatia maelezo yake hapo utaeleweka Ila sio kila jambo ni baya

Watu elfu 60 kwa mweI ni idadi nzur kama kweli inafikia hapo

Cha kuzingatia hapa ni idadi ya ndege kisha tulinganishe na idadi ya abilia si ajabu ndege zikawa zinaelemewa

Siasa mnayoikimbilia ndo inawagharimu
 
Back
Top Bottom