ATCL: Dom-Kigoma-Dar?

ATCL: Dom-Kigoma-Dar?

Ila ticket ya ATCL ipo valid kwa 6 months (ukiangalia bei utaona fastjet bei nafuu lakini hakuna cancellation na hata kama wataruhusu itabidi uongezee kulingana na bei ya siku hiyo.
Unakaa na tiketi miezi 6 ya nn? unawaachia airline hela miezi 6 (mambo ya dharura unayapigia hesabu?) anyway bado Fastjet anaongoza TZ. Pamoja na figisu figisu za hapa na pale.
 
Mkuu mwaka jana December shirika la ndege ATCL lilifuta safari zote za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga kwa amri kutoka juu kwa sababu mbili kubwa:
1) Kuwapa wakati mgumu wakazi na wageni waliopanga kutembelea maeneo hayo kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka.
2) Serikali haikupenda kabisa mtu anayeitwa LOWASSA kupanda ndege zake.

Safari za Kilimanjaro zimeanza tena
Akili zako zinakutosha kunywea maji tu
 
Unakaa na tiketi miezi 6 ya nn? unawaachia airline hela miezi 6 (mambo ya dharura unayapigia hesabu?) anyway bado Fastjet anaongoza TZ. Pamoja na figisu figisu za hapa na pale.
Operation ya fastjet ni tofauti na ya precision air na ATCL, unatakiwa ujiulize kwanini yeye bei zake zio chini alafu hawa wengine wapo juu lakini wana survive, ukijiuliza hapo ndio utapata jibu (walikuja Community airline, wakaja 540 na sasa Fastjet), ukibahatisha ticket ya 79000 ujue kuna wengine wamelipa 300,000, na mara nyingi wanaolipa 79,000 si wateja hasa wa huu usafiri (fanya uchunguzi akikosa hiyo anapanda bus)
 
Wana JF,
Naomba msaada kwa wenye kujua taratibu za ndege/aviation, nilitaka kukwea pipa toka Dodoma to Dar sasa nimechek ATCL naona nauli 165,000/= (one-way) lakini tunatoka Dodoma to Kigoma kisha ndo tunakuja Dar...KWA UTARATIBU ufuatao;

(Reporting time 05:30am) DEPARTURE TIME (Dodoma) 07:30am
ARRIVAL TIME (Dar) 11:40am
NAULI = 165,000/=???
*** Kwa utaratibu huu si bora niweke mafuta kwenye Ki-ESCUDO changu nitoke Dodoma saa 10 alfajiri by saa 3 asubuhi nipo dar? ATC hebu fanyeni namna kutuvutia wana-Dodoma tukwee hiyo Kitu.
Mmh basi kwa nauli hiyo ni rahisi sana kwa atakaetaka kwenda kigoma akapandie dodoma manake nauli yake ni zaidi ya 600000. Haha
 
ATCL wameanza kufanya Biashara kumfurahisha bwana yule hii inaonyesha Dodoma hamna abiria wengi na ndio maana wanataka wakawaunganishe na wale wa Kigoma,Biashara ya airline ngumu siyo kuwa na ndege tu.
Muda si mrefu wataanza kuomba ruzuku serikalini,kaagiza mindege mingine minne, ataipaki kwa kukosa abiria
 
Fastjet inaboa sana na hawako organized
Of course ana bei nafuu, ila kwa msafiri wa ndege mzoefu lazima atawaona chenga fastjet, sema tu wadau wengi wanamwona mwokozi kwa kuwa hawajapata fursa ya kulinganisha na sehemu nyingine. Mie wale huwa nawapenda kama bei ipo chini ya 150,000 pamoja na mzigo lakini zaidi ya hapo napanda mangalangala yetu (precision air na ATCL)
 
Operation ya fastjet ni tofauti na ya precision air na ATCL, unatakiwa ujiulize kwanini yeye bei zake zio chini alafu hawa wengine wapo juu lakini wana survive, ukijiuliza hapo ndio utapata jibu (walikuja Community airline, wakaja 540 na sasa Fastjet), ukibahatisha ticket ya 79000 ujue kuna wengine wamelipa 300,000, na mara nyingi wanaolipa 79,000 si wateja hasa wa huu usafiri (fanya uchunguzi akikosa hiyo anapanda bus)
Mkuu unataka kumaanisha nini,f
 
Watanzania wenzangu tujifunze kuangalia taarifa kama ziko sahihi kabla hatujaunga kuiponda mali yetu. Nimejaribu kwenda ATCL booking web na nimekutana na hii DOM-DSM direct flight. Yawezekana OP ni mgeni katika anga. Ila huwa kuna direct-flight na connected flight na kwa sababu ATCL bado ina ndege chache sidhani kama wanaweza kuwa na same route direct and connected. Nadhani (my guess) kuwa watakuwa wana siku ya direct na ya connected.

So kama ulikuwa na nia ya kusafiri na mabawa ya Kilimanjaro nimekusaidia kutafuta direct flight ya karibuni.
Nikutakie Safari njema na ahsante kwa kuchagua kusafiri na Air Tanzania (in that flight attendant's voice) 😉

Screen Shot 2017-03-15 at 9.33.20 AM.png
 
Kwanini abiria wa Dodoma wasisubiri ikitoka kigoma ndio wapande kuja Dar?? ATCL wamezingatia nini haswa??
 
Mkuu unataka kumaanisha nini,f
Namaanisha huu usafiri wa Fastjet (wa vigezo na masharti), mara nyingi tunautumia kutokana na timing ya zile ticket zetu flani zile za 79,000 au 101,000 (of course ni nzuri hata mie huwa ninazivia hizi na wengi wa wananchi wakikosa wanarudi kwenye usafiri wetu wa kawaida uliotukuza), kama angalau mara moja mtu aliwahi kutumia hizo option nyingine yaani Precisionair na ATCL ambao operation yao ni tofauti na fastjet (nikimaanisha thamani ya ticket yaan just incase ndege imekatwa hatua gani inachukuliwa ku-rescue situation yaani haki za abiria zinazingatiwa ikiwa pamoja na kupewa ndege nyingine either ya kukodi au vipi na kama ni vinginevyo unapewa vocha ya malazi na hotel kwa next day kitu ambacho kwa fastjet hakipo, ndo nikasema kama price ya fastjet ikiwa zaidi ya 150,000 yaani inakaribiana na hawa wengine kwa mie huwa naona bora kuchukua hawa wengine maana inakuwa hamna maana ya kununua ticket ya 187,000 (one way) alafu bado vigezo a masharti kibao wakati hizi zingine ambazo inajulikana kila kitu kimezingatiwa. Nina imani nikifanya hivi zitamfanya "kasuku" azidi kutoa bei ambazo ni affordable baada ya kuona ikipanda kidogo watu wanahama
 
Wana JF,
Naomba msaada kwa wenye kujua taratibu za ndege/aviation, nilitaka kukwea pipa toka Dodoma to Dar sasa nimechek ATCL naona nauli 165,000/= (one-way) lakini tunatoka Dodoma to Kigoma kisha ndo tunakuja Dar...KWA UTARATIBU ufuatao;

(Reporting time 05:30am) DEPARTURE TIME (Dodoma) 07:30am
ARRIVAL TIME (Dar) 11:40am
NAULI = 165,000/=???
*** Kwa utaratibu huu si bora niweke mafuta kwenye Ki-ESCUDO changu nitoke Dodoma saa 10 alfajiri by saa 3 asubuhi nipo dar? ATC hebu fanyeni namna kutuvutia wana-Dodoma tukwee hiyo Kitu.
Panda precision boss
 
Wamekaa zaidi kisiasa hivyo shirika lijiandae kuendelea kupata ruzuku ya umma kama wazee wa fake news!
 
Back
Top Bottom