ATC igeni hata haya yaliyo mazuri toka kwa RwandAir

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,863
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
Moja kati ya nashirika yanayokuja juu kwa kasi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati ni RwandAir,hili ni shirika la ndege la Rwanda,lenye makao yake makuu jijini Kigali.
Licha ya ushindani mkubwa toka kwa nchi kama Kenya na Ethiopia kwa ukanda huu wa Mashariki,Kati na Pembe ya Afrika,bado RwandAir imejipambanunua kama mahindani wa kweli wa leo na kesho.Mpaka sasa shirika hili lina ndege kadhaa,ikiwemo Boeing 737-800,Boeing 737-700,CRJ-400 Next Generation,Dash-8,Boeing Dreamliner nk

Rwanda ni nchi ndogo sana,utalii wao unategemea sana sana uwepo wa sokwe,ziwa Kivu na baada ya mwaka 1994,Kigali Genocide Memorial Centre imekuwa kama sehemu ya Utalii(Hapa niliwahi kufika) lakini watalii wamekuwa wakimiminika na kutumia shirika lao la ndege la RwandAir.

Katika usafiri wa anga RwandAir sasa unapasua anga bila mchezo,wanafika Dsm mara mbili kwa siku na kulala,wanapita Kilimanjaro,sasa wame-extend wanaenda Dubai,J'burg na Lagos.Ili kuimalisha shirika lao na watu wao,Serikali ya Kigali imeingia mkataba na shirika la ndege la Ethiopia katika kitengo cha Ufundi(Techinical Dept).Katika kitengo hiki Wahandisi wa ndege toka Ethiopia wamemwagika Rwanda wakiwafundisha vijana wa Kinyarwanda ufundi wa ndege na maujanja yake,na baada ya muda wataachiwa shirika na wao kujiendesha huku wakiwa wamejitosheleza kwa kuwa na Cabin Crews kama Air hostess na Marubani,Wahandisi nk.Ndani ya miaka 10 ijayo RwandAir inaweza kuwa shirika kubwa zaidi hata ya Kenya Airways

Week hii RwandAir imeonyesha hadharani ndege yao mpya aina ya Airbus 333-200 iliyopewa jina la "Ubumwe".Wakati sisi tukiwa na ndege moja tena mbovu,wenzetu wanapaa juu.Nchi ambayo miaka 20 iliyopita tuliwapokea kama wakimbizi na watu wasio na makazi,leo wameanza kutupita hatua moja baada ya nyingine.Kweli hapa ATC ina la kujifunza.
 
Hii mada hapa niliileta hapa siku kadhaa zimepita,na leo yametimia.Rais kaomba wataalamu toka Rwanda kwenye sekta ya anga
 
Tuombee amani nchi. Mambo yatakwenda. Otherwise tutakuwa tunapiga mark time na magari ya washawasha na concentration yetu itakuwa huko. Tulipiga mark time kwa kuwaruhusu mafisadi kuchezea nchi.
 
Back
Top Bottom