No wonder... Miafrika Ndivyo Tulivyo.... Nyani Ngabu
Mambo ya maana hatusemi miaka mingapi jela, nani kavaa nini miaka 20 haya...
Hivi vazi la jeshi la Tanzania likoje? Mimi ninafahamu lile la kijani kilichoiva kwa Army, light blue kwa Air Force, na jeupe kwa Navy. Hata hivyo nguo za rangi hiyo siyo vazi la kijeshi mpaka ziwe na nembo ya JWTZ na bendera ya Tanzania pamoja na jina na cheo cha askari anayelivaa. Vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa majeshi ya nchi nyingine pia.
Vazi le kijeshi kivita ni lile la mabakamabaka likiwa na nembo ya jeshi, pamoja na bendera ya nchi na jina na cheo cha askari aliyelivaa; kwa mfano vazi la kivita la jeshi la Marekani ni kama ifuatavyo:
Nguo ya mabakamabaka bila kuwa na nembo ya jeshi, na bendera ya Taifa hata bila kuwa na jina wala cheo cha askari siyo uniform ya jeshi. Ni nguo inayoweza kutumika na mtu yeyote yule anayefanya shughuli za porini kama vile uwindaji na camping.
Angalia yanavyoweza kutumika:
Mgombea Urais wa Marekani kwa tiketi ya Democrat mwaka 2004 akiwinda ndege
Babu anamfundisha mtoto wake kuwinda swala
Watoto wakiwa Camping
Huyu waziri anaweza kuwa karopoka, au kama ninavyolifahamu jeshi letu huenda linataka kuhodhi aina fulani ya mavazi ikiwa ni pamoja na zile safety boots (MABUTI). Ngoja tuone shria hiyo itakuwaje
Mimi nionavyo ni kwamba bado sisi watu weusi tuna matatizo.
Kama ikiwezekana mavazi hayo yapigwe marufuku kuingizwa TZ. Ni juzijuzi nilikuwa nakifikiria kununua moja ya koti la baridi liuzwalo paundi za bibi karibu 60 na ni koti zuru kwelikweli.
Sasa sijui itakuwaje na hizi sheria za ajabuajabu!
RAIA yeyote atakayepatikana amevaa vazi la jeshi au linalofanana na vazi hilo atatumikia kwenda jela miaka 20.
Rai hiyo imetolewa mjini Dodoma Bungeni na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi wakati alipokuwa anafafanua juu ya kufuata sheria ya mavazi hayo kwa wananchi.
Mwinyi alisema kuwa kuanzia sasa mtu yeyote ambaye ni raia wa Tanzania atakayeonekana amevaa vazi la Jeshi la Wananchi wa Tanzania [JWTZ] kiholela ambaye hausiki kwa namna moja ama nyingine na vazi hilo atatumikia kifungo cha kwenda jela miaka 20.
Source: http://www.nifahamishe.com
...Pheeeewwww! ..."Raia" mtakoma!!! ...kama alivyovaa mjapani huyu, heri yao wenye "nondo" za Obama na Malkia...
.........kwi kwi kwi yaani Nyani akiingia bongo na mavazi yake ya mabaka mabaka mswano tu...........