Atakayesoma sheria chuo kikuu hatapewa mkopo - serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Atakayesoma sheria chuo kikuu hatapewa mkopo - serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwakiluma, Jun 1, 2012.

 1. Mwakiluma

  Mwakiluma Senior Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  (serikali yawakaanga wanafunzi wanaotarajia kujiunga vyuo vikuu);
  hii sasa imedhihirika wazi kwamba serikali haina haja tena ya kusomesha watu wake...katika waraka wa tcu(taasisi ya vyuo vikuu) kwenda kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga vyuo vikuu mwaka huu(soma chini waraka huo) imeorodhesha wazi fani ambazo hazitapewa mkopo tena, mbali na sheria zimo fani pia za uchumi zote(economics), sociologia , political scence na zingine. Napata taabu kuwa serikali imeridhika nini na kiwango cha watu wake waliosoma mpaka kuamua kutosemesha tena wanafunzi vyuo vikuu. Nchi zote duniani zinaweka mkazo katika kusomesha watu wake lakini kwa tanzania usomi si chochote. Serikali inaamini ikiwasomesha watu wake wataamka na kuona jinsi serikali inavyotafuna rasilimali za nchi hii. Je iwapo tutaacha kuwasomesha wanasheria na wana uchumi tutakuwa na taifa la namna gani. Nani atasimamia utiaji saini wa mikataba makini na nani pia atasimamia uchumi wa nchi hii. "kweli serikali ya tanzania ni kichwa cha mwenda wazimu).

  View attachment Admissions Guidebook for 2012-2013.pdf
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unategemea tusome dude lote hilo. Kata kipande husika kiweke hapa na anayetaka habari kamili aingie huko kwenye handbook.
   
 3. J

  Jadi JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,402
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  imedhihirika waliosomeshwa hawajui sheria na wanaboronga tu,wauchumi hawaimplement walichosoma,wanajipanga kuja kivingine
   
 4. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ukali wa kina Tundu Lisu, Halima Mdee na Mnyika unawaumiza sasa. Poleni sana. Vyuo vibuni course mpya ya B.A Ed (Law).
   
 5. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,864
  Likes Received: 1,148
  Trophy Points: 280
  Acheni kuionea TCU na serikali. Miaka ya Nyerere kulikuwa na kipaumbele cha kusomesha wataalam na ilikuwa ni Kilimo, Udaktari anzia wa rural medical aid, nursing, vertinary officers, ualimu na hata tuliomaliza shule nyakati hizo hatukujua elimu nyingine zaidi ya hizo fani. hata hviyo wanasheria, wahasibu,wanauchumi na wengineo nao walikuwepo na walisoma. Mimi naona nia ya TCU ni nzuri tu kupambanua kozi zipi zina kipaumbele cha mkopo ili watu wakasome tujazie mapengo kwenye fani hizo. hawajasema fani zingine hazitapewa mkopo ila wakishawapa mkopo wenye kusoma fani zilizoainishwa wengine watapewa tu. Kumbuka pamoja na hao TCU kuanisha kozi hizo mkopo ni ''Subject to means testing'' kipimo cha kuangalia kama wewe ni maskini wa kutosha kupewa mkopo. Mfano YATIMA, WALEMAVU, UMEFIWA NA MZAZI MMOJA.
   
 6. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,864
  Likes Received: 1,148
  Trophy Points: 280
  wa kuwalaumu ni Bodi ya mikopo. fomu zao hazina maelezo mengi kwa muombaji kuna open na closed questions. ukishajaza una submit na huwezi tena kuEdit na kufuta ulichojaza mwanzo. wanasema eti wanaangalia muombaji alisoma shule gani za kulipia au za serikali. wanasahau kwamba kuna watu maskini wanauza nyanya, samaki, ubuyu, maandazi ili wagharimie elimu ya sekondari ya watoto wao. halafu pia hawajui kuna single parency ya watoto waliotelekezwa na baba zao wakasomeshwa tu na mama zao ambao wamejitolea muhanga ili kuwafikisha watoto wao sekondari. Bodi walitakiwa wataoe uwanja mpana wa Single Parency na si kukimbilia tu ni wale waliofiwa na mzazi mmoja. Mimi mwanangu amesoma Private kwa mkopo wa kazini baada ya kutochaguliwa darasa la saba na alitelekezwa na baba yake tangu utoto. Ninaamini kwa vile kasoma Private sekondari zote na amejaza fomu zenye Priority hatapewa mkopo kwa hiyo Means testing ya Bodi ya Mikopo.
   
 7. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,601
  Likes Received: 2,458
  Trophy Points: 280
  "Mimi naona nia ya
  TCU ni nzuri tu kupambanua
  kozi zipi zina kipaumbele cha
  mkopo ili watu wakasome
  tujazie mapengo kwenye fani
  hizo. hawajasema fani zingine
  hazitapewa mkopo ila
  wakishawapa mkopo wenye
  kusoma fani zilizoainishwa
  wengine watapewa tu."

  Katika nchi kama Tanzania kusema kwamba eti kozi flani ndo zipewe kipaumbele ni ujuha tena usiofaa kabisa..
  Hebu fikiria nchi hii imepiga hatua kimaendeleo kwa kiwango cha kutoa kimpaumbele cha kusomesha watu wake kwa vipaumbele, mi nadhani si sahihi hata kidogo.
  Bado tunahitaji wanataaluma wengi zaidi ya hawa tulio nao.
   
 8. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ni sawa tu wanasheria wamezidi
   
 9. e

  ebrah JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2012
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Fedha zote quchney! Kina Mkulo wamekula wakajiuzulu, now hata Hela ya dawa hawana MSD Wanawadai na wanashindwa kuhirndesha"
  Sembuse elumu, tena inayowafanya washindwe kuongoza kwa qmani
   
 10. leroy

  leroy JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 840
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  Afadhali tubaki wachache tutese kwenye labour market.
  Vijana someni Ufundi, Ualimu na Udaktari, Hizi ndizo fani za msingi kwa maendeleo.

   
 11. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  ni afadhali we umemwambia. Watu wanachangisha harusi mpaka m20 kula kuku waliokuziwa arv.!! Lazima mtie akili na kuanzisha harambee za kuchangia watu wakasome.. By the way,kilichoishinda heslb ni kushindwa kuchambua nani anafaa jupewa mkopo na nani hafai. Hata hivyo mkijazana huko mtawasumbua kina riz
   
 12. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Chagua chadema 2015 ujinga kama huu hawataruhusu kabisa,hatuna wanasheria hatuna wachumi hatuna watu wa jamii ma-activist hili taifa litakuaje? Hv nani ni waziri wa elimu ya juu? Bado yupo tu anaangalia huu ujinga?
   
 13. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  kuna vyuo vina Bsc economics,khaa! Ujanja huo waliundua,mkopo hakuna.
   
 14. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ninaamini hujaelewa kabisa hiyo sehemu inayosema serikali haitatoa mkopo kwa fani hizo. Nasisitiza naamini hujaelewa!
   
 15. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Wanasheria wako wengi mtaani, wacha wapunguzwe. Tunawahitaji madaktari, na wanasayansi wengine. Anayetaka sheria atajisomesha, mbona watu wanajisomesha master na phd.
   
 16. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,081
  Likes Received: 6,542
  Trophy Points: 280
  Hela za kusomeshea wameshaziweka
  kwenye mifuko yao.

  CDM watarekebisha haya mambo
  ni mateso ya muda tu, vijana kaza buti.
   
 17. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Wtz ndo tukome.....tuliambiwa tuchague cdm free education tukabisha eti haiwezekani.........tutajiju......
   
Loading...