chakufia nini
JF-Expert Member
- Apr 14, 2015
- 692
- 456
bwana mmoja nchini nepal aliyejulikana kwa jina la chowdhry katika jiji la kathmandu kabla ya umauti kumkuta alimwambia mkewe kuwa atakapokufa azikwe na pesa zake zote kwani alikuwa tajiri wa kutupwa na kwa madai yake alihangaika sana kuzipata fedha hizo hivyo basi alitaka kwenda nazo katika dunia ya pili.kwa kuwa mkewe alimpenda sana na hakutaka kuivunja ahadi hiyo,wakati wa mazishi,kabla ya kufukia kaburi aliwaomba watu wasubiri kidogo ili aweze kuweka zile fedha kaburini.watu walistaajabu kuona mjane yule akiweka kibox ndani ya jeneza.kwa shingo upande baada ya kuweka kibox kile watu wakaanza kufukia.
baada ya mazishi ilibidi watu wakamuulize mjane yule kwanini alifanya uamuzi ule wa kumzika mumewe na pesa zote kwenye lile box?ndipo akajibu kuwa hakuweza kuvunja ahadi aliyomuahidi mumewe hivyo basi alikwenda bank na kudeposit fedha zote za mumewe kisha akamuandikia cheki ya zile fedha zote na kuiweka ile cheki ndani ya kile kibox alichozikwa nacho.
big up sana kwa huyu mwana mama.kwani kafanya uamuzi wa busara sana.yaani mtu unakuwa na roho mbaya hata baada ya kufa?dah