Assume: Muungano umevunjika


Mie ni mmoja ya wazanzibari ambao wanaamini Tanganyika inaweza kuendelea bila ya kutegemea Zanzibar, na vile vile Zanzibar inaweza kuendelea zaidi ya ilipo sasa bila ya kutegemea Tanganyika.

Nadhani mkuu umejikita na nadharia mbovu na kusahau lengo na madhumuni ya muungano.Lengo kuu kwa wakati huo lilozaa muungano ni shinikizo kutoka nje (vita baridi) na lile la kisiasa kwa upande wa Karume.

Mwenye akili timamu, hawezi hoji kama nchi mbili zinaweza kuishi kama majirani na kuendelea na shughuli zake bila ya tatizo lolote maana ilikuwa hivyo kwa takriban miaka yote kasoro hio 47 ya muungano.Hivyo masuala yako hayana mashiko.

Hoja ya msingi ya wananchi wanayojiuliza ni faida gani wameipata ndani ya miaka 47 ? Sioni faida yoyote, bado inaendelea kuwa faida kuu ya muungano ni ya kisiasa ambayo inanufaisha wachache. Ukihoji faida za muungano hata Kikwete atakwambia ni wa kipekee barani Afrika, amani na utulivu bla bla.....This is just not enough, ukizingatia mzanzibari analipa double tax ndani ya jamhuri!
 
Mada nzuri sana hii, asante Mkuu kwa changa moto. Mimi nahisi ukivunjika muungano sote tutakuwa na nchi za kuheshimiana na watu wa nchi mbili watakuwa na mapenzi zaidi kuliko hivi sasa. Na hao wabunge watarudi Zanzibar kuendesha nchi yao kama wazalendo wenziwao. Wasiogope.
Kama munavojua, Zanzibar tuko katika kuanzisha shirika letu la ndege na kadhalika. Usafiri utakuwa rahisi kwenu na kwetu pia. Tunatoka Zanzibar airport kwenda kimataifa. Yapo mengi lakini kwanza hii moja.
 

Acha Pumba ndugu yangu. Ni watu 50 kwenye milioni moja ama kweli tu Great thinkers!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…