nyamalagala
JF-Expert Member
- Jun 5, 2016
- 744
- 675
Amani iwe kwenu wana JF.
Baada ya kusogezwa mbele kwa muda wa kuanza field mwaka huu ambapo ilikuwa ianze tarehe 25/7 ikabidi ziongezwe mbele kwa wiki mbili kutokana na zoezi la uhakiki lililokwamisha ulipwaji wa hela ya field mwaka huu.Tarehe 9/8 ndio tarehe rasmi wanafunzi waliamriwa kuripoti kwenye vituo vya kufanyia field zao.
Kama utani vile watu wameripoti Siku ya jumanne ya wiki iliyopita na ilipofika jumamosi mchana baadhi wakapigiwa simu kuwa wanakuja kuasesiwa Siku ya jumatatu tarehe 15/8. Yaani wamekaa shuleni wiki moja tu lakini Leo wanaambiwa wakae tayari kuasesiwa.
Hayawi hayawi mwisho huwa,Leo jumatatu ni kweli wameasesiwa kama kawaida.Sasa kwa mtindo huu unampimaje mtu kama ameweza kumudu mafunzo kwa vitendo wakati amefika kituoni kwake jumanne kisha jumatano akapewa vipindi,alhamisi akaingia kutambulishwa kisha akapiga pindi kidogo na ijumaa hakuwa na kipindi kisha leo jumatatu unampima kama amemudu kile alichopaswa kukifanya?.
Je kwa hali hii tutafika tunakotaka kufika kweli!.Wakati mwingine taratibu za uendeshaji wa Elimu ndizo huchangia kuiporomosha kwani haiwezekani mtu atarajiwe kukaa field miezi miwili alafu umpime ndani ya wiki moja aliyokaa kituoni kwake.Wakuu mnalionaje hili.
Hawa vijana wametendewa haki kweli kuwapima kabla ya kumaliza walau hata wiki tatu.Naomba kuwasilisha na karibuni kwa michango yenu.