Feedback
JF-Expert Member
- Mar 14, 2011
- 7,988
- 4,507
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Arusha (Katoliki) Mhashamu Josephat Lebulu amesema ushiriki wa wanafunzi wa vyuo vikuu na shule za sekondari katika vyama vya siasa nchini ni hatari na kuwataka wanafunzi hao wazingatie masomo yaliyowapeleka vyuoni na katika shule hizo. Aliyasema hayo jana katika mahafali ya wahitimu 197 ambao ni madaktari, wauguzi na wataalamu wengine wa afya waliomaliza katika Chuo Kikuu cha Tiba cha KCMC cha Chuo Kikuu cha Tumaini.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi ya jumuiya ya vijana wa CCM (UVCCM), Ridhiwani Kikwete alikuwa mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kufungua shina la wakereketwa Ofisi ya Chama Njoro wilayani Moshi na kukabidhi kadi za wanachama wapya wa UVCCM na CCM zaidi ya 220 katika vyuo vikuu mbalimbali kikiwemo cha kumbukumbu ya Askofu Stephano (SMMUCO) Kampasi ya Moshi, aliwataka wasomi kufungua matawi ya vyama katika vyuo vyao, lakini pia kutumia fursa mbalimbali zinazoibuliwa ili kujipatia ajira ndani na nje ya nchi.
Kaazi kweli kweli viongozi wetu wataasa hadi wachoke wajue vijana tumedata.
Source: HabariLeo.