Askofu: Siasa vyuoni hatari

Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,988
4,507
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Arusha (Katoliki) Mhashamu Josephat Lebulu amesema ushiriki wa wanafunzi wa vyuo vikuu na shule za sekondari katika vyama vya siasa nchini ni hatari na kuwataka wanafunzi hao wazingatie masomo yaliyowapeleka vyuoni na katika shule hizo. Aliyasema hayo jana katika mahafali ya wahitimu 197 ambao ni madaktari, wauguzi na wataalamu wengine wa afya waliomaliza katika Chuo Kikuu cha Tiba cha KCMC cha Chuo Kikuu cha Tumaini.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi ya jumuiya ya vijana wa CCM (UVCCM), Ridhiwani Kikwete alikuwa mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kufungua shina la wakereketwa Ofisi ya Chama Njoro wilayani Moshi na kukabidhi kadi za wanachama wapya wa UVCCM na CCM zaidi ya 220 katika vyuo vikuu mbalimbali kikiwemo cha kumbukumbu ya Askofu Stephano (SMMUCO) Kampasi ya Moshi, aliwataka wasomi kufungua matawi ya vyama katika vyuo vyao, lakini pia kutumia fursa mbalimbali zinazoibuliwa ili kujipatia ajira ndani na nje ya nchi.

Kaazi kweli kweli viongozi wetu wataasa hadi wachoke wajue vijana tumedata.

Source: HabariLeo.
 
akili ni nywele kila mtu ana zake waache waingize siasa vyuoni, watamaliza kichwani hamna kitu wanachojua siasa!!
 
hawa maskofu na mashehe wanatakia nini siasa, kazi yao ni kuhubiri dini mengi hayawahusu.
 
hawa maskofu na mashehe wanatakia nini siasa, kazi yao ni kuhubiri dini mengi hayawahusu.
Najua huna ujanja kwa vile Ridhwani anagawa kadi vyuoni otherwise ungekilaumu kile chama kinachowanyima usingizi.
 
Nakubaliana na hoja ya askofu . Wanafuzi wawe wanachama wa vyama lakini mambo ya kuanzisha matawi vyuoni ndo sawa sawa na ule mpango wa matawi ya chama fulani nje ya nchi.
 
Kumbe CCM na CHADEMA wote kundi moja?
Tatizo lako unaanzishaga ligi zisizo na kichwa wala miguu juzi ukaanzisha ligi ya lugha kwenye mada tofauti kabisa
kama hiyo ndiyo aina yako ya uchangiaji haina mashiko kwangu nakupotezea.
 
Nakubaliana na hoja ya askofu . Wanafuzi wawe wanachama wa vyama lakini mambo ya kuanzisha matawi vyuoni ndo sawa sawa na ule mpango wa matawi ya chama fulani nje ya nchi.
Unajua wanavyuo ni watu wazima kwa maana hiyo wanajua nini kilichowapeleka na
kuna baadhi ya vyuo vinafundisha somo la political science, kama chuo kimetenga darasa
kwa ajili hiyo vipi wanavyuo wakiwa na ofisi yao ku practise walichofundishwa.
 
Hatari huja pale wanapokua brain washed bila kutafakari wao wenyewe...
Kijana wa secondary let alone wa vyuo is old enough kua interested na mambo ya Siasa...
Bila hivyo ndio ile issue ya mtu alianza kua na interest ya Siasa at the age of 30
alafu anataka agombee uongozi wa Siasa at the age of 32/35 - anakua hajakomaa kisiasa...
 
Haya maneno aliosema Askofu, siasa vyuoni ni hatari, angesema Sheikh, CDM-kata-Jf, wangesema tatizo ni Shule tunashukuru Baba Askofu Josephat Lebulu, kasema ni msomi mzuri
 
Unajua wanavyuo ni watu wazima kwa maana hiyo wanajua nini kilichowapeleka nakuna baadhi ya vyuo vinafundisha somo la political science, kama chuo kimetenga darasakwa ajili hiyo vipi wanavyuo wakiwa na ofisi yao ku practise walichofundishwa.
Mkuu, nadhani ujamuelewa vizuri Baba Askofu Josephata Lebulu, ni msomi mzuri anachosema kakifanyia utafiti ajakukurupuka mimi nipo pamoja na Baba Askofu kwenye ili jambo la Siasa vyuoni ni Hatari
 
Mkuu, nadhani ujamuelewa vizuri Baba Askofu Josephata Lebulu, ni msomi mzuri anachosema kakifanyia utafiti ajakukurupuka mimi nipo pamoja na Baba Askofu kwenye ili jambo la Siasa vyuoni ni Hatari
Nafikiri Askofu alikuwa namwambia Ridhiwani amezidi sana.
 
Hiyo ya ridhiwani kugawa kadi 220 ni kanjanja palikuwa na mamluki kibao wengine ni vijana wa stendi walipewa mkwanja wakatia ndani huku wengine wakiwa ni wanachama wa Chadema.
CCM haina ubavu wa kuvuna watoto wa walala hoi mavyuoni.
 
Tatizo lako unaanzishaga ligi zisizo na kichwa wala miguu juzi ukaanzisha ligi ya lugha kwenye mada tofauti kabisa
kama hiyo ndiyo aina yako ya uchangiaji haina mashiko kwangu nakupotezea.

Mada tofauti kwa mujibu wa nani?

Wewe unaesema Askofu anamsema Ridhwan na CCM inashangaza kuwa umesahau kuwa Chadema nao wana matawi vyuoni.
 
hawa maskofu na mashehe wanatakia nini siasa, kazi yao ni kuhubiri dini mengi hayawahusu.

Kwahiyo wasubiri mambo yaharibike ndipo waseme? Watamhubiria nami kama sio sisi tunaoshiriki kwenye hizo siasa? Think Loud.
 
Quinine, usepende kuwa unafikiri, ebu msome vizuri Baba Askofu ujamuelewa!
Nimemwelewa sana kuwa Ridhiwani kazidi kuchochea wanavyuo, Baba Askofu anasema siasa vyuoni hazifai
yeye ndio kwanza anasema wazidi kufungua matawi vyuoni, kati ya mimi na wewe nani mnafiki.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi ya jumuiya ya vijana wa CCM (UVCCM), Ridhiwani Kikwete, aliwataka wasomi kufungua matawi zaidi ya vyama katika vyuo vyao
 
Back
Top Bottom