Askofu: Serikali ikaze uzi kwa mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu: Serikali ikaze uzi kwa mafisadi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Dec 27, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,476
  Likes Received: 5,716
  Trophy Points: 280
  Askofu: Serikali ikaze uzi kwa mafisadi
  John Nditi, Morogoro
  Daily News; Friday,December 26, 2008 @00:02  Kanisa Katoliki nchini limeitaka Serikali ya Awamu ya Nne kushika hatamu katika suala la kuongoza nchi kwa mujibu wa Katiba na mahakama kuhusika kikamilifu kusikiliza kesi za baadhi ya viongozi wanaotuhumiwa kuchota mamilioni ya fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na waliotumia madaraka yao vibaya.

  Mbali na kuitaka serikali na mahakama kusimamia wajibu wao, nao raia wametakiwa waheshimu uamuzi unaotolewa na mahakama katika masuala mbalimbali zikiwamo kesi nzito zinazoshughulikiwa kwa sasa.

  Kauli hiyo ilitolewa na Mhashamu Askofu Teresphori Mkude wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, juzi wakati wa mahubiri ya ibada ya mkesha wa Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika Kitaifa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Patris la mjini hapa.

  Alisema vitendo vya ufisadi vilivyoshamiri vimewafanya Watanzania kusherehekea Sikukuu ya Krismasi wakiwa katika mawazo mazito kuhusu hatima ya taifa lao kwa kuwa neno fedha ndio msingi na ufunguo wa maisha ambapo baadhi ya watu huzitafuta bila kuzingatia maadili mazuri.

  Alisema pamoja na mahakama kufanya kazi yake, serikali nayo inapaswa kushika hatamu katika suala la kuongoza nchi kwa mujibu wa Katiba na raia waheshimu uamuzi unaotolewa na mahakama katika masuala mbalimbali.

  “Inasikitisha kusikia wapo baadhi ya viongozi wa serikali kujipatia fedha nyingi wakiwa watumishi wa umma na iwapo ni kweli, wahusika walijifikiria hivyo hawakuzingatia upendo wa ndugu zao Watanzania na wala hawakuwathamini,” alisema Askofu Mkude. Alisema kwa mantiki hiyo, hivi sasa fedha imekuwa ikitumika kuwaletea vyeo baadhi ya viongozi wakati wa uchaguzi kwa kutofuata njia ya maadili ya uongozi.

  Alisema iwapo fedha hizo zilizochotwa na baadhi ya viongozi zingetumika kwa ajili ya kupunguza makali ya huduma za tiba katika hospitali na ujenzi wa zahanati, kuwalipia karo za shule wananchi masikini na zilizochakaa kukarabatiwa na kuboreshwa na kujengwa nyingine mpya vijijini. Kuhusu rushwa, alisema bado ni donda ndugu katika huduma nyingi kama za afya ambapo tiba ni ya kuchangia, lakini wananchi wanaendelea kudaiwa rushwa.
   
 2. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2008
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hawa wezi wa EPA waunganishwe katika shitaka la kupanga kwa pamoja kuhujumu uchumi wa Nchi DPP chukua ushauri huu ili tukate kabisa mizizi ya wezi hawa wanaotamba na fedha za wizi.
   
Loading...