Askofu Ruwa`ichi: Nyie mapadre nani aliwakataza msioe?

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
137
Reaction score
156
Wakuu nyie mnaionaje hii?

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus Ruwa`ichi amesema upadre ni wito, akieleza kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakimuuliza kwa nini mapadre wa Kanisa Katoliki hawaruhusiwi kuoa. ‎

Akizungumzia suala hilo, amesema mara kwa mara amekuwa akipokea watu ofisini kwake wanaotaka kujua sababu za mapadre kutooa, huku akiwataka kutafakari maana ya wito wa upadre. ‎ ‎“Mara chache wanakuja watu ofisini kwangu wananiuliza kwa nini unawakataza mapadre wasioe. Nyie mapadre mpo hapa, nani aliyewakataza msioe? Kuwa padre siyo balaa au nongwa, upadre ni wito,” amesema. ‎ ‎

Kauli hiyo imeibua mjadala kuhusu wito wa upadre na utaratibu wa Kanisa Katoliki kuhusu useja wa mapadre. ‎

Lakini ukiifikiria hii kauli haimaanishi kuwa mapadre wanatakiwa kuoa, kwasababu upadre ni wito basi sadaka yao ni kuji commit wasioe. Maana askofu amesisitiza kuwa kila wito una sadaka yake, kwahivyo pengine wao kutooa ndio sadaka ya wito wao. Au nyie mnasemaje wenzangu?

Hebu wenye ujuzi kuhusu hili mtueleweshe hapa aisee.
 
Hujamwelew askofu, aliposema upadri ni wito anamaanisha kabla ya mtu kuweka nadhiri ya upadri alijua kabisa akiwa padri hataruhusiwa kuoa.
Iweje wakishapata daraja la upadri ndio waone umuhimu wa kuoa wakati hakuna mtu aliyewashikia fimbo kuwa mapadri.
Hapo wanaonyesha walitafuta ajira badala ya kumtumikia Mungu.
 
sahihi mkuu
 
Sio kwa ubaya,
Mtu unakataa kuoa kisa kumtumikia Mungu kweli?Hatya vipi nyie ambao hamjaoana.Je,wazazi wenu wasingeoana mgekuja kumtumikia huyo Mungu asiyetaka muoe.

Haya na wale masister mnazijua behind on the scene’s zao?

Je,Mungu yupo teyari kudanganywa kama ninyi navyofanya(kuzini)?
Kwa sababu binafsi hakuna mwanamume anayeweza kuishi siku 365 bila kulomba,uongo.
 
Ukimtumikia Mungu ndiyo imekatazwa usioe?, unaweza weka andiko la hilo katazo mkuu?, mwili ulio timamu lazima uwe na matamanio, Shahawa zinazalishwa kila leo zinatumika wapi?, au masista wapo kwa kazi hiyo? ndiyo maana wanapata maskandali kuwala vijana wanaofanya kazi huko Makanisani aisee.
 
Unaweza kumtumikia Mungu huku ukiwa umeoa mfano ukawa Kateksita muimbaji,muombaji etc. Kutumikia sio lazima wote tuwa mapadri/wachungaji,masista, wahubiri n.k. Kila mtu anaweza kumtumikia Mungu kwa nafasi yake na wote ni sawa. Padri si bora zaidi kuliko mtumishi asiye padri.
 
Mbona Elia hakuoa.
 
Sio kwa ubaya,
Mtu unakataa kuoa kisa kumtumikia Mungu kweli?Hatya vipi nyie ambao hamjaoana.Je,wazazi wenu wasingeoana mgekuja kumtumikia huyo Mungu asiyetaka muoe.

Haya na wale masister mnazijua behind on the scene’s zao?

Je,Mungu yupo teyari kudanganywa kama ninyi navyofanya(kuzini)?
Kwa sababu binafsi hakuna mwanamume anayeweza kuishi siku 365 bila kulomba,uongo.
Ukioa wewe inatosha,a married man is a weak man,kanisa linaelewa hiyo dhana.

Tutolee upuuzi wako.
 
A married man is a weak man, hasa kwenye tamaduni za Afrika. Unapigiwa simu mama mkwe anaumwa, halafu wewe ni padri unaona sadaka za waumini zinazengea hapo akaunti inasoma 100M,utaweza kujizuia kuiba sadaka ili mama mkwe akatibiwe??.
 
Umeona baba mkwe tu, Kwahiyo akiwa baba yako mzazi inakuwaje? Au usipooa hata Baba mzazi naye unakuwa huna?
 
Wakuu nyie mnaionaje hii?

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus Ruwa`ichi amesema upadre ni wito, akieleza kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakimuuliza kwa nini mapadre wa Kanisa Katoliki hawaruhusiwi kuoa. ‎

Akizungumzia suala hilo, amesema mara kwa mara amekuwa akipokea watu ofisini kwake wanaotaka kujua sababu za mapadre kutooa, huku akiwataka kutafakari maana ya wito wa upadre. ‎ ‎“Mara chache wanakuja watu ofisini kwangu wananiuliza kwa nini unawakataza mapadre wasioe. Nyie mapadre mpo hapa, nani aliyewakataza msioe? Kuwa padre siyo balaa au nongwa, upadre ni wito,” amesema. ‎ ‎

Kauli hiyo imeibua mjadala kuhusu wito wa upadre na utaratibu wa Kanisa Katoliki kuhusu useja wa mapadre. ‎

Lakini ukiifikiria hii kauli haimaanishi kuwa mapadre wanatakiwa kuoa, kwasababu upadre ni wito basi sadaka yao ni kuji commit wasioe. Maana askofu amesisitiza kuwa kila wito una sadaka yake, kwahivyo pengine wao kutooa ndio sadaka ya wito wao. Au nyie mnasemaje wenzangu?

Hebu wenye ujuzi kuhusu hili mtueleweshe hapa aisee.
View attachment 3696701
ukitaka upate siri za hawa kina Ruwaichi,ongea vizuri na masister wanaoishi nao parokiani,,😂😂,hawa jamaa giza likiingia ni balaa sana,
 
Unaweza kumtumikia Mungu huku ukiwa umeoa mfano ukawa Kateksita muimbaji,muombaji etc. Kutumikia sio lazima wote tuwa mapadri/wachungaji,masista, wahubiri n.k. Kila mtu anaweza kumtumikia Mungu kwa nafasi yake na wote ni sawa. Padri si bora zaidi kuliko mtumishi asiye padri.
paulo ndio alizuia watumikiaji kuoa(paulism)
 
Umeona baba mkwe tu, Kwahiyo akiwa baba yako mzazi inakuwaje? Au usipooa hata Baba mzazi naye unakuwa huna?
Akioa anakuwa na wazazi wanne wanamtegemea tofauti asipooa anakuwa na wazazi wawili tu. Halafu wazazi wake waliomzaa wanaweza kutibiwa na Kanisa maana wamemtoa sadaka mtoto wao kwa ajili ya Kanisa. Ila akishaoa mambo yanakuwa mengi, ndio maana makanisa ambayo wachungaji wanaoa hawana taasisi nyingi eg shule ,vyuo, hospital na zinazoendeshwa kwa weledi kama Katoliki. Mfano mzuri shule za masista zinafanya vizuri kwa sababu masista hawana familia wanaziangalia hizo shule 24/7.
 
Kwahiyo asipooa hata kaka na dada zake wa tumbo undugu unakatika?
 
Akioa anakuwa na wazazi wanne wanamtegemea tofauti asipooa anakuwa na wazazi wawili tu. Halafu wazazi wake waliomzaa wanaweza kutibiwa na Kanisa maana wamemtoa sadaka mtoto wao kwa ajili ya Kanisa. Ila akishaoa mambo yanakuwa mengi, ndio maana makanisa ambayo wachungaji wanaoa hawana taasisi nyingi eg shule ,vyuo, hospital na zinazoendeshwa kwa weledi kama Katoliki. Mfano mzuri shule za masista zinafanya vizuri kwa sababu masista hawana familia wanaziangalia hizo shule 24/7.
Kweli kabisa mkuu,padre anaruhusiwa pia kuacha upadre aende kuoa tena ndoa ya kanisani Wala Haina shida kabisa,iwapo atashindwa kutunza nadhiri alizoweka,na hii habar ya kuchit watu wanachit tu hata waliokwenye ndoa
 
Back
Top Bottom