Askofu mwingine adakwa na unga

Mkuu utakuta mtu ana waumini kumi na hata wasaidizi hana lakini anajiita Askofu. Uaskofu umeingiliwa


Maaskofu wote wangechunguzwa kama wanavyo chunguzwa viongozi kubaini biashara zao na vyanzo vya utajiri wao
 
Mkuu,

Mwakasege ameingiaje hapa? Yeye sio na ajiiti Askofu na wala hana Kanisa. Yeye ni Mwalimu tu!!!! Please usitafuta kuwachafua watu bila sababu za msingi!!!!!

Tiba

Mkuu usifanye kuegemea upande mmoja bali mtake akuwekee vielelezo vya kuwatuhumu hawa watu
 
acha watu watafute hela, iwe haram au halali mbaya kushikwa tu.
 
Mkuu nimeona jina la Morine Amatus. Hii siyo ile habari ya mtoto wa Amatus Liyumba aliyekamatwa kule Lindi na mzigo? Mbona hii imekuja kama habari nyingine tena mpya?
Lindi ni kituo cha usambazaji madawa ya kulevya?

Huyo askofu hakukimbia aliachwa tu atokomee zake. Katika hali hiyo ya usiku polisi watakuwaje wazembe kiasi hicho hadi mtu akimbie. Ina maana waliisimamisha hiyo gari kichwa kichwa? Jamaa wangekuwa na mashine si wangewamaliza polisi wetu hao? Kuna vimelea vya ufisadi hapa.


Kazi kutuletea mijibwa uwanjani tukienda kucheki soka......huko yanakotakiwa majibwa haya kunapwaya
 
MORIS Charles hujitambulisha kwa jina la Yusuph Mohamed Lutengwe.



Kwanini mnang'ang'ania kuwa huyu bwana anajiita askofu ili hali anatumia majina mawili moja la kikiristo na jingine la kiislam?Je haiwezekani kuwa Yusuf Mohamed Lutengwe ndio huyo anaejiita Morris Charles hivyo akawa ni shekh na sio askofu?
 
Kwanini mnang'ang'ania kuwa huyu bwana anajiita askofu ili hali anatumia majina mawili moja la kikiristo na jingine la kiislam?Je haiwezekani kuwa Yusuf Mohamed Lutengwe ndio huyo anaejiita Morris Charles hivyo akawa ni shekh na sio askofu?

Mkuu hawa wandundu huwa hawaaminiki. Unaweza kukuta ni Sheikh huko Sudan ya Kusini na ni Askofu hapa Tanzania!
 
hajakimbia huyo ni mchongo wa mkubwa huo..kweli vita ya madawa hatutaiweza kamwe

Hata mie siliamini hilo
eti kirahisi rahisi tu wanasema jamaa alikimbilia pasipo eleweka,sasa huo mtego wao waliuka wa nini? mimi nadhani walipo weka mtego walitambua kabisa kuwa ni lazima kuna mtu atachomoka hiyo possiblity kama polisi lazima waijue,sasa ilikuwaje jamaa achomoke kirahisi?
 
Duu mkuu umenifanya nicheke sana, yaani unakuta mtu upande mmoja sheikh upande mwingine Askofu, huu ni full usanii, basi dini zimeshaingiliwa.....

Mkuu hawa wandundu huwa hawaaminiki. Unaweza kukuta ni Sheikh huko Sudan ya Kusini na ni Askofu hapa Tanzania!
 
Da nashindwa kuelewa na uyo nabii frola mbona simwelewi manake jinsi alivyo jichuna!!!!!!!!!!aya siku za mwisho kutakua na manabii wa uongo ngoja tuone.
 
Tatizo kubwa sio hawa watu kujiita majina mbalimbali; Tatizo kubwa ni ruksa iliyotolewa na AZIMIO LA ZANZIBAR kuhusu Uhuru wa kuabudu ndio DINI mbalimbali za watu pekee zikaanzishwa kama NGO's za kujineemesha.

Tatizo ndio hilo; ni kuangoalia hizo sheria zilizoanzishwa na kizidhibiti; hizo DINI uchwara zitaondoka
Unakumbuka kuna DINI Moja ilimpekekea Rais Kikwete Sanduku la Pesa Ikulu? Hiyo DINI haina hata Benki? kutoa Cheki? na Rais akapokea, kama msaada wa waliaoadhirika na Mafuriko Dar.
 


Waliokamatwa wametajwa kuwa ni pamoja na
Ismail Adamu (28), Hamad Said (27), Morine Amatus (22) na Pendo Mohammed Chausi (67) ambaye ni mwenye nyumba yalipokamatwa madawa hayo. Tayari watu hao wamepandishwa kizimbani.




Nimevutiwa na washirika wa huyo "askofu Yusuph Mohamed Lutengwe."
 
Propaganda za kidini, mbaya sana.! Ili kuipa nguvu ile notion kwamba 'viongozi wa dini' -here reffered of christian religion ni wauza unga, Mbaya sana
 
najipa assignment nimpate nabii flora!duu anavutia naanza kwenda kanisani kwake mbezi
 
Back
Top Bottom