MORIS Charles anayejitambulisha kuwa ni askofu wa kanisa moja la kiroho jijini Dar es Salaam amedakwa na unga hivi karibu katika Kijiji cha Mchingambili, mkoani Lindi.
Vyanzo vya habari vimeeleza kwamba Charles ambaye wakati fulani hujitambulisha kwa jina la Yusuph Mohamed Lutengwe alidakwa nyakati za usiku Januari 11, mwaka huu akiwa katika gari lake aina ya Toyota Land Cruiser (namba zinaifadhiwa ).
Taarifa hizo zimedai kwamba kudakwa kwa mtu huyo kulifuatia habari zilizowafikia polisi mapema ambapo waliarifiwa na aina ya gari analotumia Charles kupokea unga au dawa za kulevya aina ya Heroine kilo 210 zenye thamani ya shilingi bilioni 9.4.
MTEGO WA POLISI
Imeelezwa kwamba siku ya tukio polisi waliweka mtego baada ya kupata taarifa ya kiongozi huyo kuwa atakuja katika kijiji hicho na gari lake la kifahari, wakapewa namba na raia wema.
Habari zinasema ilipofika saa tano usiku waliliona gari kwa mbali na lilipowakaribia, walilisimamisha lakini inadaiwa kuna mtu alichomoka ndani ya gari hilo na kutokomea gizani.
Vyanzo hivyo vinadai kuwa jeshi la polisi halikumjua mtu huyo lakini baadaye wakaambiwa kuwa aliyekimbia ndiye huyo anayejiita Askofu Charles ambapo mtu mmoja aliyekuwa akiliendesha gari hilo alitiwa mbaroni.
Habari hizo zilieleza kwamba muda huo huo watu aliokuwa akiwapokea wakiwa na madawa walikamatwa na polisi wa kikosi kazi.
Waliokamatwa wametajwa kuwa ni pamoja na Ismail Adamu (28), Hamad Said (27), Morine Amatus (22) na Pendo Mohammed Chausi (67) ambaye ni mwenye nyumba yalipokamatwa madawa hayo. Tayari watu hao wamepandishwa kizimbani.
Habari zinasema polisi walimfuatilia askofu huyo na kugundua kuwa anaishi Mikocheni, jijini Dar es Salaam na wakafanikiwa kukamata mali nyingine ambazo ni magari mawili ya kifahari aina ya Porsche Cayenne na Jeep Wrangler.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa askofu huyo amefanikiwa kuwakimbia polisi na ametorokea nje ya nchi Januari 15, mwaka huu.
Vyanzo hivyo vya habari vimedai kwamba kiongozi huyo wa dini huwa ana hati mbili za kusafiria, moja anatumia jina la Kiislam na huitumia anapotembelea nchi za Kiislam na nyingine yenye jina la Kikristo.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa hata magari anayotumia, usajili wake una utata kwani tulipofuatilia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) anayedaiwa kumiliki gari hilo Toyota Land Cruiser lililokamatwa na polisi ni Rashida Abushir Jumanne na aliuziwa na huyo kiongozi Januari 16, mwaka huu.
Afisa mmoja wa TRA alisema mmiliki wa kwanza wa gari hilo ni Makame .O. Juma na kumbukumbu zao zinaonyesha kwamba Juni 9, 20011 aliliuza kwa kiongozi huyo anayejulikana pia kwa jina la Lutengwe.
UTATA WA GARI
Kinachoshangaza ni kwamba Lutengwe alikimbia nchini Januari 15, mwaka huu, iweje auze gari kwa Abushiri Januari 16, mwaka huu wakati gari hilo tangu likamatwe Januari 11, mwaka huu bado lipo polisi hadi sasa?
Hata hivyo, mwandishi wa habari hii akiwa TRA alipata namba ya simu ya Abushiri, alipopigiwa alipokea mtu ambaye alijitambulisha kuwa yupo Morogoro na alisema kwamba anamfahamu Abushiri ambaye anaishi Sinza jijini Dar es Salaam .
Kijana aliyepokea simu aliwasiliana na Abushiri alimpa namba ya mwandishi na akapiga simu. Katika mahojiano alikana kwamba yeye hana gari aina ya Toyota Land Cruiser na hajawahi kulimiliki, akadai inawezekana jina lake na namba yake ya simu inatumika vibaya na wahalifu.
Abushiri alipohojiwa zaidi na mwandishi sababu ya simu yake kumkabidhi mtu ambaye yuko Morogoro wakati yeye yupo Dar es Salaam alijitetea kuwa huyo ni mdogo wake, hivyo ameamua kumpa hiyo simu ili aitumie.
Uchunguzi umebaini kwamba hata baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa na madawa ya kulevya, simu zao zimegundulika kuwa waliosajiliwa ni marehemu waliokufa kati ya miaka miwili na mitatu na wengine walikuwa wakiishi Morogoro.
Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa alipoulizwa kuhusu kiongozi huyo alisema kwamba hayupo tayari kulizungumzia suala hilo kwa vile bado linachunguzwa.
Hata hivyo, alikiri kwamba kuna mfanyabiashara mkubwa wa madawa ya kulevya aliyekimbilia nje ya chini na kwamba magari yake yanashikiliwa na jeshi la polisi.
VIONGOZI WA MAKANISA
Baadhi ya wachungaji wa makanisa waliozungumza na gazeti hili kufuatia kadhia hii ya dawa za kulevya nchini, wameitaka serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wafanyabiashara hiyo haramu.
John Said wa Kanisa la Victorious la Ubungo External amesema kwamba sasa imefikia muda wa serikali na jamii kwa ujumla kupiga vita biashara hiyo na wanaokamatwa na dawa wachukuliwe hatua kali haraka.
Nabii Flora Peter wa Kanisa la Huduma ya Maombezi lililopo Mbezi Beach, Dar es Salaam amesema kwamba wanaokamatwa na biashara hiyo wachukuliwe hatua mahakamani kwani wanaumiza nguvu kazi ya taifa kutokana na ukweli kwamba vijana wengi wanaangamia na dawa hizo.
Mchungaji Timoth Mwankenja alisema:
Kunahitajika jitihada za pamoja kati ya raia na polisi ili kupambana na biashara hii haramu. Kanisa letu tumewahi kutoa elimu mitaani, kunahitajika ushirikiano katika vita hii. Kama kuna viongozi wa dini wanajihusisha wachukiliwe hatua kali.
Mchungaji Alponce Mtemela wa Kanisa la Pentekoste lililopo Kawe, amesema kwamba dawa za kulevya ni janga la taifa kwani wanaohusika na biashara hiyo haramu ni matajiri na wanaweza kufanya chochote, hivyo ameiomba serikali kuchukua hatua kali.
Mwanzoni mwa mwaka jana jeshi la polisi kitengo cha dawa za kulevya lilimkamata Askofu wa Kanisa la Lord Choose Chaersimatic Revived, aliyejulikana kwa jina la Chidi Okechuku.
Okechuku alikamatwa maeneo ya Mbezi Beach katika nyumba aliyopanga na alikutwa na kilo 81 za Heroine na kwa sasa kesi yake ipo mahakama kuu.
Nabii Flora na Nabii Mwingira wote kundi moja.Wanaruhusu Mavazi ya Kikahaba Kanisani.Mke wa Mwingira anavaa wigi na suluali inayo onyesha Equator.Nabii Flora Mukorogo ili kuvuta manabii wa Kiume.
Ku
Makanisa mengi yameshindwa nidhamu na maadili ya Mungu.Torati 22:5 Mavazi ya mwanamme kwa mwanamke ni Chukizo.Kubadili asili kwa maana ya kujichubua kuvaa mawigi,suluali kwa mwanamke ni chukizo.Mavazi ya kikahaba chazo cha ubakaji kanisani. Mavazi ya Kikahaba ni maandalizi ya zinaa.
Mali zote za viongozi wa dini zimesha hesabiwa na kuthaminishwa tangia mwaka 2009.Mali hizo ni pamoja na Nyumba viwanja,pesa Benk n.k.Mchakato huo umefanyika kwa viongozi wote ,wenye kuiongoza jamii.Itafika muda nchi ikipata Rais kama Kagame kila mtu atalia.Kila Askof atatangaza mali zake hadharani kama mwenzao alivyofanya hapo nyuma.Inatakiwa Kanisa lisipokee pesa kutoka kwenye chanzo kichafu ukiwemo madawa ya kulevya, ukahaba, ufusika, ulawiti,ujambazi,ufisadi.Mungu hawezi kupokea s adaka yoyote kutoka ktk mapato hayo.Ni bora kanisa likafanya tathimini ya waumini wana otoa Zaka ili kuepuka laana
Ya kumutukana Mungu.
Da nashindwa kuelewa na uyo nabii frola mbona simwelewi manake jinsi alivyo jichuna!!!!!!!!!!aya siku za mwisho kutakua na manabii wa uongo ngoja tuone.
Natamani hata Getrude Rwakatare, Gamanywa na Mwakasege nao walipuliwe. Mnadhani hizo international schools za Rwakatare ni matokeo ya pesa halali wananngu. Jipeni fursa mchunguze mtagundua mengi kiasi cha kutoamini. Wengine wamo kwenye ofisi kubwa za umma ambao huwalilia wawakamate wenzao. Uliza Amina Chifupa alipotaka wakamatwa alifanywa nini? Huu mtandao ni mkubwa hata hao Maaskufu si wauzaji wenyewe. Wenye mali wako serikalini wanangu.
Huu ni udaku tu hamna lolote hapo kwanza habari ndefu lakini imeshindwa kubainisha uaskofu wa huyo tapeli. Eti askofu wa kanisa moja!!!??? Lipi na liko mtaa gani? Kama mwandishi aliweza kufualia hadi kupiga simu morogoro alishindwaje kupata baadhi ya waumini wa kanisa hilo? Ili kupata tathmini yao juu ya Kiongozi wao wa kiroho ??? Hakuna sababu ya kumhoji Flora Peter na wachungaji wengine kabla ya waumini wa kanisa husika au kuthibitisha kwa namna yoyote ile uaskofu wa huyo mtu. Halafu angalia majina ya wahusika Karibia yote ni ya kiislam je huyu ni askofu wa msikiti au kanisa? Watu hapa wapo kwenye michakato ya kukashfu ukristo, wakristo wa kweli kueni makini hasa nyakati hizi za mwisho zilizo tabiriwa kujaa hatari. shika sana ulichonacho.......
nabii flora na nabii mwingira wote kundi moja.wanaruhusu mavazi ya kikahaba kanisani.mke wa mwingira anavaa wigi na suluali inayo onyesha equator.nabii flora mukorogo ili kuvuta manabii wa kiume.
Ku
Enzi za unabii zilishakwisha. Hivi huyu anayejiita Nabii Flora, unabii kapewa na nani? Au ndio haya mambo ya 'The Beast and false prophet (Revelations: 19:20)
Mkuu nimeona jina la Morine Amatus. Hii siyo ile habari ya mtoto wa Amatus Liyumba aliyekamatwa kule Lindi na mzigo? Mbona hii imekuja kama habari nyingine tena mpya?
Lindi ni kituo cha usambazaji madawa ya kulevya?
Huyo askofu hakukimbia aliachwa tu atokomee zake. Katika hali hiyo ya usiku polisi watakuwaje wazembe kiasi hicho hadi mtu akimbie. Ina maana waliisimamisha hiyo gari kichwa kichwa? Jamaa wangekuwa na mashine si wangewamaliza polisi wetu hao? Kuna vimelea vya ufisadi hapa.
Huyo askofu hakukimbia aliachwa tu atokomee zake. Katika hali hiyo ya usiku polisi watakuwaje wazembe kiasi hicho hadi mtu akimbie. Ina maana waliisimamisha hiyo gari kichwa kichwa? Jamaa wangekuwa na mashine si wangewamaliza polisi wetu hao? Kuna vimelea vya ufisadi hapa.
Good job policemen! They had no option. You would have done exactly the same if you are Tanzanian! Kumbe mlitaka wamsakizie nani akamue hiyo mihela? I tell you hakuna hakimu mwenye jeuri ya kumhukumu bilionea nchi hii, na hata kama mkakamavu mmoja angetokea yet hakuna jela ingempokea coz this is the story of our history. And we are not doing this because of poverty, hunger or ignorance but because of who we are: a nation in peril, divided, under a seriously corrupt system, with no liberty and freedom.
Enzi za unabii zilishakwisha. Hivi huyu anayejiita Nabii Flora, unabii kapewa na nani? Au ndio haya mambo ya 'The Beast and false prophet (Revelations: 19:20)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.