Askofu mwingine adakwa na unga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu mwingine adakwa na unga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Mar 7, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  IGP Mwema.[​IMG]

  Nabii Flora
  Na Makongoro Oging'

  MORIS Charles anayejitambulisha kuwa ni askofu wa kanisa moja la kiroho jijini Dar es Salaam amedakwa na unga hivi karibu katika Kijiji cha Mchingambili, mkoani Lindi.

  Vyanzo vya habari vimeeleza kwamba Charles ambaye wakati fulani hujitambulisha kwa jina la Yusuph Mohamed Lutengwe alidakwa nyakati za usiku Januari 11, mwaka huu akiwa katika gari lake aina ya Toyota Land Cruiser (namba zinaifadhiwa ).

  Taarifa hizo zimedai kwamba kudakwa kwa mtu huyo kulifuatia habari zilizowafikia polisi mapema ambapo waliarifiwa na aina ya gari analotumia Charles kupokea ‘unga' au dawa za kulevya aina ya Heroine kilo 210 zenye thamani ya shilingi bilioni 9.4.

  MTEGO WA POLISI
  Imeelezwa kwamba siku ya tukio polisi waliweka mtego baada ya kupata taarifa ya kiongozi huyo kuwa atakuja katika kijiji hicho na gari lake la kifahari, wakapewa namba na raia wema.

  Habari zinasema ilipofika saa tano usiku waliliona gari kwa mbali na lilipowakaribia, walilisimamisha lakini inadaiwa kuna mtu alichomoka ndani ya gari hilo na kutokomea gizani.

  Vyanzo hivyo vinadai kuwa jeshi la polisi halikumjua mtu huyo lakini baadaye wakaambiwa kuwa aliyekimbia ndiye huyo anayejiita Askofu Charles ambapo mtu mmoja aliyekuwa akiliendesha gari hilo alitiwa mbaroni.

  Habari hizo zilieleza kwamba muda huo huo watu aliokuwa akiwapokea wakiwa na madawa walikamatwa na polisi wa kikosi kazi.

  Waliokamatwa wametajwa kuwa ni pamoja na Ismail Adamu (28), Hamad Said (27), Morine Amatus (22) na Pendo Mohammed Chausi (67) ambaye ni mwenye nyumba yalipokamatwa madawa hayo. Tayari watu hao wamepandishwa kizimbani.

  Habari zinasema polisi walimfuatilia askofu huyo na kugundua kuwa anaishi Mikocheni, jijini Dar es Salaam na wakafanikiwa kukamata mali nyingine ambazo ni magari mawili ya kifahari aina ya Porsche Cayenne na Jeep Wrangler.

  Hata hivyo, imeelezwa kuwa askofu huyo amefanikiwa kuwakimbia polisi na ametorokea nje ya nchi Januari 15, mwaka huu.

  Vyanzo hivyo vya habari vimedai kwamba kiongozi huyo wa dini huwa ana hati mbili za kusafiria, moja anatumia jina la Kiislam na huitumia anapotembelea nchi za Kiislam na nyingine yenye jina la Kikristo.

  Uchunguzi wetu umebaini kuwa hata magari anayotumia, usajili wake una utata kwani tulipofuatilia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) anayedaiwa kumiliki gari hilo Toyota Land Cruiser lililokamatwa na polisi ni Rashida Abushir Jumanne na aliuziwa na huyo kiongozi Januari 16, mwaka huu.

  Afisa mmoja wa TRA alisema mmiliki wa kwanza wa gari hilo ni Makame .O. Juma na kumbukumbu zao zinaonyesha kwamba Juni 9, 20011 aliliuza kwa kiongozi huyo anayejulikana pia kwa jina la Lutengwe.

  UTATA WA GARI
  Kinachoshangaza ni kwamba Lutengwe alikimbia nchini Januari 15, mwaka huu, iweje auze gari kwa Abushiri Januari 16, mwaka huu wakati gari hilo tangu likamatwe Januari 11, mwaka huu bado lipo polisi hadi sasa?

  Hata hivyo, mwandishi wa habari hii akiwa TRA alipata namba ya simu ya Abushiri, alipopigiwa alipokea mtu ambaye alijitambulisha kuwa yupo Morogoro na alisema kwamba anamfahamu Abushiri ambaye anaishi Sinza jijini Dar es Salaam .

  Kijana aliyepokea simu aliwasiliana na Abushiri alimpa namba ya mwandishi na akapiga simu. Katika mahojiano alikana kwamba yeye hana gari aina ya Toyota Land Cruiser na hajawahi kulimiliki, akadai inawezekana jina lake na namba yake ya simu inatumika vibaya na wahalifu.

  Abushiri alipohojiwa zaidi na mwandishi sababu ya simu yake kumkabidhi mtu ambaye yuko Morogoro wakati yeye yupo Dar es Salaam alijitetea kuwa huyo ni mdogo wake, hivyo ameamua kumpa hiyo simu ili aitumie.

  Uchunguzi umebaini kwamba hata baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa na madawa ya kulevya, simu zao zimegundulika kuwa waliosajiliwa ni marehemu waliokufa kati ya miaka miwili na mitatu na wengine walikuwa wakiishi Morogoro.

  Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa alipoulizwa kuhusu kiongozi huyo alisema kwamba hayupo tayari kulizungumzia suala hilo kwa vile bado linachunguzwa.

  Hata hivyo, alikiri kwamba kuna mfanyabiashara mkubwa wa madawa ya kulevya aliyekimbilia nje ya chini na kwamba magari yake yanashikiliwa na jeshi la polisi.

  VIONGOZI WA MAKANISA
  Baadhi ya wachungaji wa makanisa waliozungumza na gazeti hili kufuatia kadhia hii ya dawa za kulevya nchini, wameitaka serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wafanyabiashara hiyo haramu.

  John Said wa Kanisa la Victorious la Ubungo External amesema kwamba sasa imefikia muda wa serikali na jamii kwa ujumla kupiga vita biashara hiyo na wanaokamatwa na dawa wachukuliwe hatua kali haraka.

  Nabii Flora Peter wa Kanisa la Huduma ya Maombezi lililopo Mbezi Beach, Dar es Salaam amesema kwamba wanaokamatwa na biashara hiyo wachukuliwe hatua mahakamani kwani wanaumiza nguvu kazi ya taifa kutokana na ukweli kwamba vijana wengi wanaangamia na dawa hizo.

  Mchungaji Timoth Mwankenja alisema:
  "Kunahitajika jitihada za pamoja kati ya raia na polisi ili kupambana na biashara hii haramu. Kanisa letu tumewahi kutoa elimu mitaani, kunahitajika ushirikiano katika vita hii. Kama kuna viongozi wa dini wanajihusisha wachukiliwe hatua kali."

  Mchungaji Alponce Mtemela wa Kanisa la Pentekoste lililopo Kawe, amesema kwamba dawa za kulevya ni janga la taifa kwani wanaohusika na biashara hiyo haramu ni matajiri na wanaweza kufanya chochote, hivyo ameiomba serikali kuchukua hatua kali.

  Mwanzoni mwa mwaka jana jeshi la polisi kitengo cha dawa za kulevya lilimkamata Askofu wa Kanisa la Lord Choose Chaersimatic Revived, aliyejulikana kwa jina la Chidi Okechuku.

  Okechuku alikamatwa maeneo ya Mbezi Beach katika nyumba aliyopanga na alikutwa na kilo 81 za Heroine na kwa sasa kesi yake ipo mahakama kuu.


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hawa Ma-Askofu ni wa Uongo walikuja wakati wa Azimio la Zanzibar waliruhuzu Uhuru wa dini' dini nyingi zikaingia zisizo za maana sasa tunapata shida

  Sasa hawa watu wanatuharibia nchi yetu ana Passport mbili Jina la kikristo na kiislamu what a joke na kakimbia nchi
   
 3. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Maisha ya watanzania yamekwua magumu sana.
  religion as an institution imeiingiliwa sana.
  Zamani ukiskia askofu, roho inandunda maana una imagine ya watu kama Pengo, Kilaini na wengine.
  Siku hizi ukisikia askofu, unaulizia kwanza wa kanisa gani?
  ndio chanzo cha mambo kama haya.
  Angalia majina ya askofu mwenyewe na jina la kanisa lake.
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimeona jina la Morine Amatus. Hii siyo ile habari ya mtoto wa Amatus Liyumba aliyekamatwa kule Lindi na mzigo? Mbona hii imekuja kama habari nyingine tena mpya?
  Lindi ni kituo cha usambazaji madawa ya kulevya?

  Huyo askofu hakukimbia aliachwa tu atokomee zake. Katika hali hiyo ya usiku polisi watakuwaje wazembe kiasi hicho hadi mtu akimbie. Ina maana waliisimamisha hiyo gari kichwa kichwa? Jamaa wangekuwa na mashine si wangewamaliza polisi wetu hao? Kuna vimelea vya ufisadi hapa.
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu utakuta mtu ana waumini kumi na hata wasaidizi hana lakini anajiita Askofu. Uaskofu umeingiliwa
   
 6. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hawa maaskofu hii ndiyo biashara yao kitambo! Ni swala la muda tu yule nyangumi mwenye wafuasi wengi atatiwa mbaroni!
   
 7. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Natamani hata Getrude Rwakatare, Gamanywa na Mwakasege nao walipuliwe. Mnadhani hizo international schools za Rwakatare ni matokeo ya pesa halali wananngu. Jipeni fursa mchunguze mtagundua mengi kiasi cha kutoamini. Wengine wamo kwenye ofisi kubwa za umma ambao huwalilia wawakamate wenzao. Uliza Amina Chifupa alipotaka wakamatwa alifanywa nini? Huu mtandao ni mkubwa hata hao Maaskufu si wauzaji wenyewe. Wenye mali wako serikalini wanangu.
   
 8. Wonder Woman

  Wonder Woman Senior Member

  #8
  Mar 7, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MORIS Charles hujitambulisha kwa jina la Yusuph Mohamed Lutengwe.


   
 9. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bwana awajua walio wake na kila aliitaye jina la Bwana auache uovu,naomba wadakwe wengi iwezekanavyo,Mungu hadhihakiwi,tutawatambua kwa matunda yao,bila kuwasahau wanaolawiti waumini wao,wezi wa sadaka,waliovunja ndoa za waumini wao,hawatakufa kabla ya kulipa uovu wao wote!
   
 10. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Sasa wakale wapi>
   
 11. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #11
  Mar 7, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ujinga tu.. Udini utaichinja serikali hii.. Mtu kujiita Sheick,Askof, au Padre unahakika gani kwamba anaifanya kazi inayotambulisha Wasifu Wa Jina.. Umesema Mtu aliyejitambulisha Kama askof Moris halafu tena unasema alitokomea gizani Na mkahisi ndiye askof.. Mbona taarifa zinajikanganya. .. Binafsi Mtu anayesema viongozi wa Dini anamkasirisha Mola.. Sisemi kwamba wanadamu hawa ni malaika flan but my take walah chezeeni Maaskof Hao ila siku matayosema Imam akamatwa Na madawa ya kulevya lazima mthibitishe ni wa msikiti gani wa wapi Na sehemu gani Na uimam Wa raajun ipi.. Msipothibitisha Mbona mtakiona. Serikali inayochafua Dini za watu Ina laana.. Fakathun.. Sio kila anayejiita Imam ni Imam.. Kujiita kila Mtu anaweza kujiita apendavyo.. Serikali isipokuwa makini Kwa hili itazidi kukabiliwa Na mikosi, mitihani dhoofukhal...
   
 12. S

  Skillionare JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Huyo si askofu ni msanii !
   
 13. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mmh, kazi bado ipo.
   
 14. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Mwakasege ameingiaje hapa? Yeye sio na ajiiti Askofu na wala hana Kanisa. Yeye ni Mwalimu tu!!!! Please usitafuta kuwachafua watu bila sababu za msingi!!!!!

  Tiba
   
 15. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  kwani unadhani hawa maaskofu hawana wanasiasa na vigogo nyuma yao?
   
 16. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  mwingine ana majina yote askofu mtume na nabii sijui vyote hivyo anatoa wapi?
   
 17. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #17
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  I like it
   
 18. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #18
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  je unaona ni vyema kulihadaa jina la bwana ili upate kula kwakuangamiza watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu?
   
 19. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #19
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo hapo unawatetea hawa maaskofu walokamatwa na haya madawa au unania gani? Embu funguka zaidi
   
 20. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #20
  Mar 7, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nabii flora acha kupaka mkorogo. Thamini kazi nzuri ya uumbaji iliyofanywa na mungu.
   
Loading...