Askofu Mwanamapinduzi adaiwa kukimbia nchi

Ndugu Watanzania!
Kwa moyo mzito ninapenda kuwajulisha kuwa Askofu Maximilian Machumu maarufu kwa jina la Mwanampinduzi amelazimika kuikimbia nchi kuokoa maisha yake! Ameomba mimi nifikishe ujumbe huu kwa viongozi wengine waliotajwa katika waraka wake pamoja na ninyi nyote!

Kwa kuwa ni Askofu, taarifa za kukimbia kwake haziwezi kufichwa. Mara kadhaa ametujulisha juu ya hali yake lakini imefikia mahali na sisi tumeona inafaa aweze kuondoka kwa muda!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 5 Septemba 2025; saa 5:20 usiku

TAARIFA KWA UMMA JUU YA KUONDOKA KWANGU NCHINI TANZANIA!

Wapendwa
Askofu Emmaus Mwamakula, Askofu Benson Bagonza, Askofu William Mwamalanga, Padre Charles Kitima, Maaskofu, Wachungaji na Waumini wote;

Mhe. John Heche Makamu (Mwenyekiti wa CHADEMA), Mhe. John Mnyika (Katibu Mkuu wa CHADEMA), Dkt. Willbroad Slaa, Wakili Boniphace Mwabukusi (Rais wa TLS), Wakili Anna Henga (Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)), Wakili Onesmo Olengurumwa (Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC))' Watetezi wa haki za binadamu na Watanzania wote.

Nilipokea taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika kuwa usalama wangu uko hatarini, tunatafutwa tutekwe na kuuawa mimi na Askofu Gwajima. Mimi nimeshuhudia baadhi ya matukio kadhaa yanayotishia usalama wangu kama ifuatavyo:

Nimenusurika kutekwa mara kadhaa kwenye mazingira tofauti tofauti wakati wa sakata la kufungiwa kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima, ambapo mimi ndiye Naibu Katibu Mkuu wa Kanisa hilo.

Nimetafutwa mara nyingi na watu nisiowajua na kunusurika kupigwa risasi wakati wa ibada kwenye kumbi ambazo waumini wa Kanisa letu wanakusanyika kufanya Ibada. Na nililazimika kutoshiriki ibada pamoja na waumini kwa wiki kadhaa sasa.

Mara nyingi nimefuatiliwa na kukimbizwa na magari mbalimbali katika mazingira tata. Lakini pia, watu kadhaa wasiofahamika wamefika nyumbani kwangu na kuniulizia kwa walinzi wa nyumbani.

Kufuatiwa matukio haya yote pamoja na taarifa hizi siwezi kupuuza jambo hili, kwani baadhi ya ninaowafahamu waliwahi pia kupewa taarifa za kutekwa kama hizi. Baadaye walikuja kutekwa na hawajaonekana hadi leo wakiwemo Mdude Nyagali, Deusdedith Soka na Juma Kaswahili. Hawa wote nimekuwa nao kwenye harakati mbalimbali za kupigania haki nchini.

Baada ya Mhe. Tundu Lissu ambaye nimekuwa naye Ngorongoro kupigania haki za Wamasai kupewa kesi ya uhaini, mashaka na wasiwasi vimeongezeka kwangu pia hasa baada ya watu wasiojulikana kuanza kunifuatilia kila mara.

Kwa muda sasa nimeonekana kuwa ni tishio kutokana na harakati zangu za muda mrefu za kisiasa, kutetea haki za binadamu, kushiriki kwenye masuala ya CHADEMA na masuala mbalimbali ya nchi yetu Tanzania, kupitia maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:

KUFANYA HARAKATI ZA KUTETEA HAKI ZA BINADAMU KUPITIA JUKWAA LA SAUTI YA WATANZANIA

Kupitia jukwaa hili nimeshiriki kwenye masuala mbalimbali kama kupinga mkataba wa bandari wa DP World, kutetea haki za Wamasai wa Ngorongoro, kupinga utekaji na kutetea haki za binadamu nchini. Haya yote yalifanyika kwa njia ya Makala za video, makongamano, mahojiano na taasisi za haki kama LHRC kupitia Haki TV, Watetezi TV na vyombo vingi vya habari nchini, kushiriki mijadala ya haki nchini kupitia Club House na space mbalimbali.

KUFANYA SHUGHURI ZA KISIASA KUPITIA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

Kupitia chama cha CHADEMA ambapo mimi ni mwanachama wa muda mrefu, na Mwenyekiti wa Wilaya ya Itilima, nilishiriki katika shughuli mbalimbali za chama; ikiwemo maandamano yaliyoandaliwa na chama nchi nzima katika awamu zote kudai Katiba Mpya. Nimeshiriki ziara mbalimbali za kampeni ya mikutano ya “No Reforsm No Election” ambayo inaendelea mpaka sasa nchi nzima. Lakini pia, nimekuwa nikihudhuria kwenye kesi ya Mwenyekiti wa Chama Mhe. Tundu Lissu, Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

KUTETEA HAKI NA UHURU WA KUABUDU NA KUPINGA UBAGUZI WA KIDINI

Nimekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki na uhuru wa kuabudu nchini, ikiwemo kupinga kulifungiwa kwa Kanisa la Mch. Mwakipesile Mbarikiwa (Mbeya), kupinga na kukemea vikali kuvamiwa na kupigwa kwa Padri Charles Kitima, kupinga kufutiwa kwa usajili wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima ambalo limefungwa kwa sababu ya kukemea utekaji nchini, suala ambalo dunia nzima imeshuhudia msuguano mkali kati ya polisi na waumini wa Gwajima, na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Albert Msando.

Kutokana na ushiriki wangu wa moja kwa moja kwenye maeneo hayo makubwa matatu, nahisi ndio sababu ya mimi kutafutwa ili nitekwe. Kwa hiyo nimelazimika kuchukua tahadhari zote ikiwemo kuondoka nchini sababu za usalama.

Nimechukua uamuzi huu baada ya kutafakari sana ikiwemo kushauriana na familia pamoja na watumishi wa Mungu kadhaa na maombi. Mungu aliyeniondoa kwenu kwa kitambo, basi huyu Mungu atanileta tena kwenu kwa wakati wake. Nitaendelea kuwaombea na kushirikiana na ninyi kwa kadiri mazingira yatakayoruhusu!

Askofu Maximillian Machumu Kadutu (Mwanamapinduzi)
Naibu Katibu Mkuu wa Kanisa la GCTC (Ufufuo na Uzima)
Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Itilima, Simiyu
Moderator - Sauti ya Watanzania

5 Septemba 2025; Uhamishoni.
Toka vijiwe vyao vifungwe na wakose sadaka watakimbia mmoja mmoja
Hapo ndio unajua walikuwa wachungaji wa Mshahara
 
hii hatari sana its a partial win kwa serikali na ccm --- """ wao wanapakukimbilia mimi na wewe tutakimbilia wapi """ - hii kauli mara ya mwisho nimeisikia jana kama sio juzi kutoka kwa mwenezi wa ccm
 
Hahaha, hata Chura kiziwi kikinuka ana kwea pipa to Oman, Tafuta passport mzee
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
Siasa zao za udini hiyo ndo dawa Yao funga makanisa ili watafute pa kukimbilia,
 
Kiongozi wa aina yake kukimbia na kutuacha waumini wake katika mazingira anayoyakimbia si salama. Wote pamoja na yeye hakuna mwenye uhakika na Kesho yake. Yeye ameweza kukimbia nchi kwasababu anapo pakukimbilia na waumini wake hasa tusio na pakukimbilia tufanyeje?

Ask. Desmond Tutu hakukimbia Afrika Kusini. Lakini pia niliona maaskofu wa DRC wakiongoza maandamano nchini mwao, bila shaka walitaka wafe pamoja na waumini wao.

Ikumbukwe kuwa, kufa ni lazima. Kila mwenye pumzi ikiwa ni pamoja na wauaji ni lazima siku moja atakufa. Tusichokifahamu wote ni kila mmoja wetu hafahamu namna itakavyokuwa siku ya kufa kwake! Hata Askofu wetu huko alikokimbilia kuna siku atakufa kwasababu kifo ni ahadi ya Mungu kwa kila mwenye pumzi.
 
maendeleo na utu, kmmk samia usituone kama sisi ni matako yako
 
Toka vijiwe vyao vifungwe na wakose sadaka watakimbia mmoja mmoja
Hapo ndio unajua walikuwa wachungaji wa Mshahara
Acha roho mbaya,

Taasisi gani ya dini haikusanyi sadaka?
 
Ni ngumu kuamini mdude hatunaye tena.....Mungu amlaze mahala pema peponi
 
Back
Top Bottom