Kwa kawaida mimi nawaheshimu sana hawa watumishi wa Mungu. Hasa kama ni Maaskofu, na huyu ni Mkuu wa K.K.K.T!!!!!!!!!!!!
Lakini kwa heshima na taadhima, Mheshimiwa Askofu, mahubiri yako yamekosa TIJA. Hujajijulisha kwamba DOWANS ni nini na hujui kwamba inamilikiwa na nani. Hata Rais wetu Jakaya Kikwete amekiri hajui wamiliki wa DOWANS. Wewe nani kakujulisha shareholders wa Dowans?
Wengi wetu tunaamini Dowans na Richmond ni kampuni feki zilizoundwa na mafisadi waliokwapua fedha zetu sisi WaTz. toka BoT (EPA) na kuzitumia kwa madhumuni yao ya kisiasa mwaka wa 2005. Hata Marehemu Daudi Balali alikiri kwamba aliagizwa na Mkuu wake atoe fedha kusaidia uchaguzi. Wakubwa wakazichukua toka EPA. Zilizosalia wakajidai wao ni Wamerikani na kuwapelekea Tanesco mitambo ya umeme wa dharura, wakati huo wakijibandika jina la RICHMOND DEVELOPMENT CORPORATION (P.L.C.).
Kama kawaida katika mashughuli ya haraka haraka ya matumizi ya fedha za wizi, mitambo yao haikukidhi vigezo vilivyotamkwa na Tanesco. Hapo ndipo Bunge letu tukufu lilipoingilia na kugundua, baada ya uchunguzi yakinifu, ulioonyesha uzalendo wa hali ya juu, ufedhuli wa watu tuliodhani ni viongozi wetu ukagundulika. Sasa tumewabatiza ni "MAFISADI"!!!!!!!! Tunakusihi Mheshimiwa Askofu, usali tena na utatambua kuna waumini wako wameku-mislead. Nakuombea Mwenyezi Mungu akusaidie ktk sala hiyo.
Wazalendo jasiri wa Tanzania, ambao wanajali kwa dhati maslahi ya nchi yetu, na watu wanaoona uchungu wa wanyonge wanaotumbukizwa katika lindi la umaskini, unaosababishwa na na hawa wezi wa fedha za umma, wameona njia pekee ni kuhamasisha WaTanzania kuandamana kwa amani na kupinga kwa nguvu zote, malipo kwa hawa wezi na baradhuli. Naamini Dowans hawajajitambulisha kwako. Watakaofaidika na hili tozo la Doawans ni wezi wa mali ya umma.
Hata kama hawa majiizi yatafanikiwa kuwapumbaza Serikali kupinga maandamano ya amani kupinga malipo haya, sisi wanyonge tutaendelea kusali ili hatimae fedha zetu watakazolipwa hatimae zirudishwe kwa kutaifisha mali za hawa baradhuli. Crime does not pay.