Askofu Mwamasika apinga maandamano ya DOWANS

Askofu Mwamasika apinga maandamano ya DOWANS

Mwanajamii

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2008
Posts
7,063
Reaction score
71
amka2.gif

na Francis Godwin, Iringa
WAKATI zikiwa zimepita siku mbili tangu Jeshi la Polisi nchini kuzuia maandamano ya wanaharakati wanaopinga hatua ya serikali kutaka kuilipa kampuni ya kufua umeme ya Dowans, Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini Makumira, Iringa, Askofu Dk. Peter Mwamasika ameibuka na kupinga maandamano hayo kwani hayana tija kwa taifa.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mahafali ya 14 ya chuo kikuu hicho jana, Dk. Mwamasika alisema kuwa maandamano ni njia ya mwisho hivyo kinachopaswa ni kuhakikisha wanaharakati hao wanakutana katika meza ya mazungumzo na viongozi au hata ikiwezekana kutumia vyombo halali vya maamuzi na si kuitisha maandamano ambayo mwisho husababisha vurugu .
Alisema kuwa matatizo ya taifa hili hayawezi kutatuliwa na vikundi vya watu wachache wanaochochea wananchi ili wafanye maandamano ya kuipinga serikali bali ni muhimu kukaa katika meza moja ili kutoa ushauri kwa viongozi wa serikali.
Hata hivyo aliwataka wanasheria kuhakikisha wanashiriki katika kutoa msaada kwa Watanzania katika kutafuta suluhu ya kweli juu ya malipo hayo.
Alisema suala la serikali kulipa ama kutolipa malipo kwa kampuni hiyo si suala la kuwadanganya Watanzania ili kushiriki katika kufanya maandamano bali ni suala la kisheria ambalo linahitaji zaidi msaada wa wanasheria katika kupinga ama kuridhia malipo hayo. Katika hatua nyingine, Dk. Mwamasika alipongeza hatua ya serikali ya kuanzisha shule za sekondari za kata ambazo zimesaidia katika kufuta ujinga miongoni mwa Watanzania.

Source. Tanzania Daima

[TD="bgcolor: #ffffff"]


[/TD]
 
Askofu ambaye anahubiri neno la Mwenyanzi Mungu na anaona kulipa dowans ni halali basi ujue yeye mwenyewe amejificha kwenye mwamvuli wa dini kuwachuna kondoo za Mungu sadaka yao.
 
The source justifies the content. When u pick Tz Daima expect nothing else more than cleansing and praising EL.
 
Hawa maaskofu sasa ni kichefuchefu kitupu afadhali hata Bakwata
 
Maaskofu Wanatumiwa vbaya mno,ila waache wataulizwa kwa Mungu
 
huyu nae ni dokta ati maandamano ni vurugu hata kama mimi sio chadema si ungi mkono malipo ya dowans. Mwizi hakubaliani na mwibiwa ila wote wawe wezi. Unatumiwa baba askofu shauri yako . Ukirudia hii pumba utaona
 
Ndio wale wale wanaokurupuka kutoa kauli bila ya kufikiri kwa kina. Mungu atamnusuru kwa kuwa na uwezo finyu wa uelewa.
 
Ni vizruri huyo Askofu akafafanua kama hayo na mawazo yake binafsi au ni msimamo wa kanisa (yaani KKKT). Mwaka 2005 tuliambiwa kuna chagua la mungu lakini sasa waliosema hivyo wanatamani ardhi ipasuke waingie ndani. Hii kauli ya askofu sina shaka itakuja kumjeruhi yeye (kama ni kauli binafsi) au KKKT (kama ni msimamo wa kanisa).
 
!!!!!!!!!!!!???????? Ati nini? Huyu askofu? Huyu si anategemea sadaka zetu? Kulipwa kwa dowans kutatuasili hadi wananchi tuishiwe hizo sadaka, anyway kama ndo anavyoamini mwache amini ila siku mungu atamuuliza alifanya nini kutetez wananchi walipokuwa wanadhurumiwa
 
Maaskofu naona wameanza kupandwa na kichaa cha kulopokalopoka, mi naona wakae chini na wapewe semina ya kuwa makini na wanachozungumza, pia wamwombe Mungu awape cha kuzungumza. Pia wanafunzi wa tumaini wamekosea ilitakiwa wamzomee. Kwani nchi hii nani ambaye hajui sakata la dowans limetoka wapi. Maandamano nikushinikiza kutokuwalipa wezi wanaotuzurumu, hivyo si kuleta vurugu kama akili yake ilipofikia
 
Askofu ambaye anahubiri neno la Mwenyanzi Mungu na anaona kulipa dowans ni halali basi ujue yeye mwenyewe amejificha kwenye mwamvuli wa dini kuwachuna kondoo za Mungu sadaka yao.
Kwa taarifa Askofu huyo ni kada wa CCM na aliwahi kutaka kugombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mafisadi. Huko kanisani kajificha tu, yeye mwenyewe anajua hayupo kwa ajili ya waumini wake ambao wanakufa kwa magonjwa yanayotibika kwan ipesa za madawa zimechukuliwa na mafisadi ambao mwisho wa siku wanatoa sadaka maalumu kanisani kwa askofu huyo. Ebu fuatillia makanisa hayo yanapo itisha harambee utakuta waalikwa wakuu ni mafisadi. Kunawakati waliwahi kumualika mwenyekiti wa mafisadi Rostamu Azizi, baada ya kupigiwa kelele walijifanya kumurudishia mchango wake.
 
Mwamasika hawezi kuongea tofauti na aliyoyasema. Kwanza ni mwanasiasa (Aligombea ubunge kupitia ccm), sio mwadilifu na pia sio mtu mwenye fikra pevu. He is too ordinary kwenye arguments zake. Ni wale wale tu ambao hata wananchi wakifa njaa hakuna shida wakati wao wanakula hadi vyakula vinawauwa. Its a pity kusikia haya
 
Namkumbuka sana huyu mzee enzi zile pale Dodoma. Ni mzee wa pumba sana huyu!
 
Ndio wale wale wanaokurupuka kutoa kauli bila ya kufikiri kwa kina. Mungu atamnusuru kwa kuwa na uwezo finyu wa uelewa.

Huyu mzee Askofu mstaafu asamehewe kwani hajui alisemalo!!Historia ya maisha yake na utumishi wake hapo dayosisi ya Dodoma ni vielelezo tosha kuwa hajui alisemalo.
 
Huyu aligombea ubunge Dodoma mjini kupitia Magamba!
 
Hii nchi itaendelea kuwa masikini hadi pale vimburu kama Fisadi papa na wajukuu zake watakapotokomea kama Gadafi.
 
Huyu fisadi mkubwa tu. Kawaulize waumini wa Dodoma alikokuwa Askofu. Ameifilisi hiyo dayosisi kabla ya kustaafu. Ana kila aina ya uchafu na mkipenda ingieni Yu Tube mtaona maajabu yake.
 
The source justifies the content. When u pick Tz Daima expect nothing else more than cleansing and praising EL.

Bado natafakari tatizo la sasa la Tanzania Daima limesababishwa na nani na kwa nini? Ni Kibanda anayeonekana kuuasi utu wake kwa minajili ya kumtakasa Lowassa ama ni mabadiliko ya sera za mwenye gazeti? I no longer read the paper
 
Back
Top Bottom