Askofu Mwamakula: Mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwenye miaka 13 aswekwa Mahabusu kituo cha Polisi Kirumba

Una hakika kwamba ni kweli aliiba limao tu? Acheni kutoa bila kusikiliza upande wa pili.
Tuache ya limao,jee kwa umri wake ni sawa kuwekwa mahabusu na watu wazima? Na kwa nini wasimpeleke mahakamani waendelee kukaa naye mahabusu huku walezi wake hawajui mtoto alipo? Wacha roho ya kishetani kwa vile aliyeleta hoja humpendi. CCM mna roho mbaya sana.
 
Kuna watu wana roho mbaya kumzidi hata shetani aisee ila Mungu ni mwaminifu malipo hapahapa duniani hata usipolipa wewe kizazi chako kitalipa tu, nimeiona na ninalipia tu kwa sababu ni kizazi cha machifu, waliyoyafanya babu zangu kwenye uchifu wao nalipia big time lakini Mungu ni mwema, nimeshatubu kama kizazi na Mungu anatenda miujiza. Tusitende mabaya jamani.
 
kama tatizo ni limao tu kwanini wananchi mpaka majirani wasimtetee wamuangushie kipigo? jiulize kwanza hapo
Kama sijakosea kusoma ni kwamba huyu mtoto kapigwa na wenye mlimao na amepelekwa polisi hakuna aliyeona hilo tukio
 
Kama sijakosea kusoma ni kwamba huyu mtoto kapigwa na wenye mlimao na amepelekwa polisi hakuna aliyeona hilo tukio
hapanja mkuu walimchangia watu wengi tu wanakijiji mpaka walitaka kumdedisha hivi kweli unaweza kusema ni limao tu?kuna kitu nyuma ya pazia watu wote hawawezi kuwa na akili moja
 
Back
Top Bottom