Askofu Mokiwa Vs Lowassa Kulikoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu Mokiwa Vs Lowassa Kulikoni?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DSN, Oct 24, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kupitia Dondoo za magazeti ya leo kuna habari inayomuhusu Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania (ACT), Dkt. Valentino Mokiwa,kulikoni wengine tuko mbali na magazeti tujuzeni?

  Manake Askofu Mkuu huyu kwa misimamo ndio mwenyewe, sasa kwa kusikia yuko ndani ya issue na star wa siasa za Bongo kidogo inabidi tu dadavue dadavue kidogo. ebu tumwageni na taarifa hizo. [Bofya Hapa]

   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ungeelezea japo kwa ufupi juu ya mawazo/hisia/maoni yako juu ya hiyo habari ili watu wajue wanachangia nini.
   
 3. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ndio maana nikaiweka jamvini sisi huku polini hatuna magazeti ila kupitia ITV nimeona msoma taarifa za dondoo za magazeti akiongelea habari ya mokiwa na lowasa lakini wakati nataka kuelewa nini kinachoendelea msomaji akawa ameamia kwenye taarifa nyingine.

  Ndio maana nikatumia jamvi kualika wadau watyujuze.Manake kuna wakati Askofu huyu alipiga kelele sana kuhusu Shule za Kata,alilalamika kuwa zimekuwa ni shule za kukaliilisha watoto badala ya kuwaelimisha na kuwapa ufahamu.Na mwisho alisema zilianzishwa bila kujiandaa.Hivyo kwa kupingana na Shule hivyo ni kuwa alikuwa anapingana na muasisi wa shule hizo ambazo ni bomu la Taifa miaka mitano ijayo kuanzia sasa.

  Ila kwa hili la leo la yeye na Lowasa ndio maana nataka kujua kulikoni.
   
 4. Mr.Toyo

  Mr.Toyo JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 9, 2007
  Messages: 433
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HII IMEKAAJE??

  ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk. Valentino Mokiwa amewataka Watanzania kuchangia huduma za kijamii bila kuogopa kuitwa mafisadi.

  Dk. Mokiwa amesema Watanzania wengi wamekuwa waoga kutoa walicho nacho kwa sababu ya kuhofia kuitwa mafisadi na kuongeza kuwa fisadi ni neno na watu wasiogope kuchangia.

  Alisema hayo jana katika harambee ya kanisa hilo iliyoongozwa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ya kuchangia ujenzi wa mabweni na vyoo katika Shule ya Sekondari ya Askofu Mkuu John Sepeku, iliyopo Yombo Buza jijini Dar es Salaam.

  Katika harambee hiyo, michango ilivuka lengo la kukusanya Sh milioni 100 na kufikia Sh milioni 126; fedha taslimu Sh milioni 65.9 na ahadi Sh milioni 60.9.

  Lowassa alichangia Sh milioni 20. Katika hatua nyingine, Dk. Mokiwa ameitaka Serikali kurudisha shule za mashirika ya dini zilizotaifishwa.

  Alisema kwa sasa Kanisa linahitaji kurudishiwa shule hizo pamoja na mali zake ambapo itakuwa mdau katika kutoa elimu nchini, kwani zilizopo hazina ubora kutokana na kuwa na upungufu mbalimbali kama ya kukosa walimu na vitabu.

  Alisema ingekuwa nchi nyingine, Kanisa lingekuwa limeshakwenda mahakamani, lakini jambo la msingi ni Serikali ijue kuwa ina mali ambazo sio zake na sio hadhi kwake kukaa na kitu ambacho sio chake.

  ENDELEA: HabariLeo | Askofu- Watanzania msiogope kuitwa mafisadi

  My ???:
  1-Je Mheshimiwa askofu alimpaka mafuta EL kwa mgongo wa chupa ili atoe mchango zaidi
  2-Au alidhamiria kumpa matumaini kutokana na skendo dhahiri za ufisadi zilizomkabili EL?
  3-Je Mheshimiwa askofu hajui sisi walalahoi tuliowengi tunavyochukulia uzito wa neno fisadi/ufisadi?

  Y
  api maoni yako mwana JF??????????
   
 5. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  watanzania maskini mnatabu sana
   
 6. L

  Losemo Senior Member

  #6
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watumishi wa Mungu walikuwepo zamani. Sasa hivi makanisa yamekuwa ya kijasiria mali zaidi. Hata majambazi yanatafutiwa lugha laini mradi ana hela lakini wakumbuke Tajiri kuuridhi ufalme wa mbinguni ni muujiza tu. Halikuwa tamko la heshima kwa askofu, Watanzania tunajua kwamba fedha kifisadi ni za wizi 2
   
 7. k

  kamakak Member

  #7
  Oct 24, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Yaani askofu Mokiwa kamwambia Lowasa akiingia Ikulu arudishe shule zote za waanglikana.Sasa Lowasa mwenyewe amesha kataa mara nyingi bado hajaamua kugombea.Huyo Askofu Mokiwa kaambiwa na nani?Haya maneno yangesemwa na sheikh hapa jamvini ingekuwa ni matusi matupu.Sasa tuseme huyu askofu kanunuliwa nae.Kweli Mfumo kristo ufanya watu vipofu wa fikra.
   
 8. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hakika message sent.

  Kwanza amnampigia debe na kuuza Lowasa kwa waumini wa Kikristo. Lakini pia kilio cha kurudishiwa shule zao kitapata jibu muafaka.

  Waislam waliambiwa NO. Wakristo je?
   
 9. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
 10. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
Loading...