Askofu Mokiwa: Bunge la Katiba linaloendelea ni uhaini na ubatili mtupu

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,526
Aliyekuwa askofu wa kanisa la Anglikana Tanzania, Askofu MOKIWA amesema kuwa bunge la katiba linaloendelea mijini Dodoma ni ubatili na ukatili kwa Taifa hili. Amesema kuwa wapenda amani wamekwisha sema na kuonya na Jukwaa la kikristo limetoa maonyo sana ila anashangaa kuna watu vichwa ngumu bado wanaendelea kung'ang'ania mambo yao. Ameendelea kutoa maonyo kwa kusema, kama bunge la katiba wanadhani wana haki na sifa za kuendelea na kikao basi wasituletee KATIBA AMBAYO HATUKUIPENDEKEZA.

Source: EATV KURASA LEO SAA MOJA JIONI
 
Watatuletea tu kwa sababu wanajua tunaogopa police,risasi na mabomu.Hizi kelele wao wanaona ni sawa na kelele za mlango.Nilishasema huko nyuma kama wachache hatutakubali kufa kwa ajiri ya Taifa hili basi tukae kimya tu-wafanye watakalo
 
Sitta hamsikilizi mtu,anachoangalia ni Tsh 150 millioni atakazovuna mwisho wa bunge na akijua urais hapati
 
Hongera sana baba askofu, angalau sasa taasisi za dini mmeanza kutekeleza wajibu wenu kwa nchi kuliko yale matamko mliyokuwa mkimezeshwa huko nyuma
Asasi zote za dini na kiraia zipaze sauti kwani katiba mpya ya maridhiano chini ya rasimu ya warioba ndio italiacha taifa letu ni moja na amani.
 
serikali ya ccm ni hawasikii wala kuona hata maono ya viongozi wa dini hawa ccm hawa tofauti na mashetani hawa nawachukia sana Sitta pamoja na wajumbe wa ccm MUNGU atawahukumu wote
 
Angesema sheikh angeambiwa mchochezi na anachanganya dini na siasa ...
 
Sita awepo kwenye ile list ya watu ansarabo, aingizwe kwenye list muda wake utafika tu
 
Hivi mokiwa mwakani anagombea udiwani kwa chama gani wakuu nimemshuhudia akiwa na kadi ya chama cha siasa na anajipanga kugombea udiwani mwakani.
 
HAWA MAASKOFU NDIO WALIOMBEBA SLAA UCHAGUZI 2010 BAADA YA KUTOA WARAKA,SASA WANACHOKITAKA UPANDE WA PILI TUMEKIJUA,SISI WOTE NI WATANZANIA.NCHI UNAZOSIKIA WANACHINJANA INAANZA HIVIHIV?i
 
Back
Top Bottom