Askofu Mkuu Mwamakula: Baada ya CHADEMA ni CCM na wasio kanda yake

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411
SIWEZI KUNYAMAZA KATIKA MAISHA HAYA
WAkati CCM wakiamini ukiukwaji wa sheria na haki za binadamu ni kwa wapinzani peke, yamekuta akina Nappe, Mwigulu, January na wengine huku mzee wa Msoga akidhalilishwa na kivulana cha Iringa pamoja na Kinana.

Waliamini ni kwa wapinzani, sasa inakuja kwao

[Kule] Ujerumani [wafuasi wa Hitler] walianza na [kuwakamata, kuwatesa na kuwaua] Wakomunisti; mimi sikupaza sauti kuwatetea hao [Wakomunisti] kwa kuwa mimi sikuwa Mkomunisti. Kisha wakawaendea Wayahudi. Pia, sikupaza sauti kuwatetea hao [Wayahudi] kwa kuwa mimi sikuwa Myahudi. Kisha wakaanza kuwakamata wafanyakazi na wanachama pamoja na viongozi wa vyama vya wafanyakazi. Mimi sikuweza kupaza sauti yangu kuwatetea hao pia kwa kuwa mimi sikuwa mwanachama [wala kiongozi wa chama cho chote cha wafanyakazi]. Baadaye wakaanza kuwashughulikia [waumini na viongozi wa Madhehebu ya Roman] Katoliki; mimi sikuweza kusema lolote [nikanyamaza] kwa kuwa mimi nilikuwa [Mkristo wa Madhehebu ya] Ki-Protestanti. Hatimaye wakanijia mimi mwenyewe na kunikamata, na hapo sasa hakukuwa na mtu mwingine ye yote aliyebaki ambaye angeweza kupaza sauti...."

Maneno hayo yalisemwa na Mchungaji Niemuller baada ya kukamatwa na kuteswa na kisha kufungwa wakati wa utawala wa kikatili wa Hitler kule Ujerumani. Alipokuwa huru na nafasi ya kupaza sauti, hakuweza kuwatetea wengine kwa kuwa alidhani kuwa yeye kama Mchungaji halikuwa jukumu lake; pia hakuwahi hata siku moja kuwaza kuwa yeye pamoja na familia yake na waumini wenzake nao wangelikuja kukamatwa, kuteswa, kufungwa na hata kuuawa!

Maneno hayo nimeyatafsiri kutoka katika kitabu kilichoandikwa kwa Lugha ya Kiingereza kiitwacho "Church and State" katika ukurasa wa 121, kilichoandikwa mwaka 1984 na Mhashamu Baba Askofu Dkt. John Henry Okullu (marehemu) wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Maseno South, Kenya. Askofu Okullu alimnukuu Mch. Niemuller ili kuwaonyesha Maaskofu wenzake katika Bara la Afrika kuhusu umuhimu wa kuwasemea na kuwatetea watu wengine katika jamii zao.

Mimi pia ninaamini kuwa wito wangu kama Askofu ni pamoja na kuwatetea na kuwasemea wengine katika jamii yangu. Hata kama kuwatetea huko kutanifanya nisieleweke lakini sitaweza kunyamaza hata kama sauti yangu ni nyembamba na hafifu. Siku zote ninamuomba Mungu ili anipe kipaza sauti (Habakuki 2:1) kusudi niseme, nishauri, nionye, nikemee, na nitie moyo (Ezekieli 33:1-20). Ni maombi yangu kuwa Mungu kwa njia zake ataupa kibali ujumbe huu ili umfikie kila mtu katika nchi yetu mkubwa kwa mdogo, tajiri na maskini, mtawala na mtawaliwa, msomi na maamuma, mwanasiasa na asiye mwana siasa, kiongozi wa dini na muumini, mfanyabiashara na mjasiliamali, mfanyakazi na mkulima, mwenye dini na asiye na dini, nk.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula -
 
Shda ya cc watu weusi ni ubinafsi na ujinga mwng... Vyuma vishaanza kulana wacha waonje joto ya jiwe ndo akil ziwakae sawa
 
Askofu Pengo ndo kaharibu nchi hii. Yeye kila uozo alikuwa anatetea. Bora wamelitoa angalau maaskofu waliobaki watampasha. Bado ruwaichi anamvutia pumzi tu
Shda ya cc watu weusi ni ubinafsi na ujinga mwng... Vyuma vishaanza kulana wacha waonje joto ya jiwe ndo akil ziwakae sawa
 
Ukweli siku zote utatuweka huru, ni vyema Urais ukajengwa kama taasisi imara, na wala sio "one man show", sauti zenye busara na hekima siku zote hutoa taadhari juu mabaya yanayolinyemelea taifa letu, lkn wana CCM walio wengi hupuuzia kwa kudhani kuwa wao wapo salama.

Bunge limekosa meno kupitia wingi wa wabunge wa CCM na utiifu kwa chama chao kutokana na upendeleo wanaoupata ktk kulinda maslahi yao binafsi. Mhimili wa mahakama nao imeingiliwa, tunaona utiifu wa makada waliojichimbia ndani yake wakipangwa kuendesha kesi kimkakati, na ukija na maamuzi ya kukipa shavu chama chao.

Lkn jambo moja li dhahiri, "Sikio lisikiao haliwezi kukatwa ktk kichwa".
 
Back
Top Bottom