Askofu mkuu KKKT jimbo la Kusini: Tungetengeza kizazi cha ajabu sana kwa Taifa kwa kutokuimba wimbo wa Taifa mashuleni

kilagalila

JF-Expert Member
Nov 8, 2018
320
154
1544899007410.jpeg
Askofu mkuu wa kanisa la KKT jimbo la kusini ISAYA JAPHET MENGELE amemshukuru Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk.JOHN POMBE MAGUFURI kwa kutoa marekebisho juu ya matumizi ya wimbo pamoja na rangi za bendera ya Taifa

Askofu huyo mkuu wa jimbo la kusini ametoa shukrani hizo mbele ya mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth msafiri wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo cha tumaini mkoani Njombe na ya saba ya chuo hicho yaliyofanyika katika maeneo ya chuo mkoani Njombehuku akimtaka mkuu huyo wa wilaya kuzipeleka shukrani za kanisa hilo kwa Rais.

“nimpongeze sana mtukufu Raisi kutoa itikio la haraka sana tulianza kufadhaika juzi tulipoletewa elekezo ya kwmaba wimbo wa taifa usiimbwe isipokuwa kwenye dhifa za kitaifa tulitaka kuona tunatengeneza Tanzania isiyokuwa na uzalendo kwasababau wimbo wa Taifa ni mahali pekee ambapo mtoto anaweza kujifunza nini Tanzania na nini utanzania na fahari yake angeipata kupitia yaliyomo katika wimbo wa Taifa sasa tunapoambiwa wimbo ule uimbwe kwenye dhifa za kitaifa maana yake kwenye matukio ya Rais tu, mimi nimshukuru mh.Rais tumesoma tena taarifa za mh alivyo rekebisha ilibradi wimbo ule uimbwe kwa usahihi hilo tutalisimamia maana tulianza kufadhahika moyoni lakini vile vile ametuwekea vizuri juu ya nembo za kitaifa tunashkuru sana mimi tangu nchi inapata uhuru toka 1961 nilikuwepo na tulijifunza rangi hizo sasa kwa kweli nilipoona kizazi hiki kilitaka kubadilisha maana nilitaka kufadhaika”alisema askofu Mengele.

Aidha Askofu huyo ametoa shukrani zake kwa serikali kwa kutambua mchango wa taasisi za kidini kutoa huduma mbali mbali ikiwemo elimu.

“tumshukuru pia Raisi kuruhusu makanisa kushirikiana serikali kutoa huduma tunazoziweza kwakweli kama hizi za elimu ilipaswa serikali ifanye lakini na sisi tumeruhusiwa kutoa huduma tunazoziweza, tunamshukuru sana kwa kuutambua mchango kwa makanisa kwa kupokea vitu na kupewa msamaha wa kodi kwa vitu ambavyo vinatoa huduma kwa jamii hilo utupelekee shukrani za dhati kwa kuwa mchango wetu ni mkubwa sana kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii ambayo tumekabidhiwa”alisema Askofu mkuu

Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth msafiri ametumia nafasi hiyo kuwaomba watanzania na wananchi wa mkoa wa Njombe kuendelea kushiriki katika kazi kwa kumuunga mkono Raisi ili kuleta manufaa kwa taifa.

“haya wanayofanya wenzetu biblia inasema asiyefanya kazi na asile haya wanayofanya wenzetu mmeyasikia wenyewe ni mawazo ya mda mrefu tusiwe wasemaji tushiriki katika kazi kama kiongozi wetu anavyofanya maana yake wewe usipofanya kazi huna haki hili kwetu liwe deni tukatumie maarifa yetu katika kubuni vitu vizuri kwa ajili ya ustawi wa Taifa letu.”alisema Ruth msafiri

Siku chache zilizopita kulikuwa na barua ya maelekezo iliyoandikwa na wizara ya elimu sayansi teknolojia na ufundi juu ya matumizi ya wimbo wa Taifa na rangi katika bendera ya Taifa ambapo kwa sasa kutokana na taarifa kutoka IKULU imeeleza kuwa Rais ameamua kuifuta barua hiyo na endapo kutakuwa na mabadiliko yoyote ni lazima yafanyike kwa kuzingatia taratibu zote kwa kuwa jambo hilo ni la kitaifa na sio la mtu mmoja.

mc.amiri/mr.mtaani

MWISHOO=========================================================
 

Attachments

  • IMG_0018.JPG
    IMG_0018.JPG
    203 KB · Views: 22

Similar Discussions

Back
Top Bottom