Askofu Mkude: Hata Mussa alipomwambia Farao alionekana mchochezi, hivi mnafurahia watu kupotea na kufa?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
ASKOFU MKUDE AHOJI UKIMYA KWA WANAOPOTEA.

•Akumbushia upotoshaji wa mitandao ya kijamii
•Ataka barua yake isomwe Tanzania nzima

*************************
Askofu wa jimbo katoliki Morogoro Mhashamu Telesphor Mkude ametahadhalisha uwepo wa hofu Kubwa kutokana na ukimya usio na maelezo juu ya raia wa Tanzania wanaopotea.

Akizungumza katika homilia yake takatifu Mara baada ya kusomwa barua yake ya kichungaji katika misa ya mkesha wa pasaka usiku wa tarehe 31 kuamkia tarehe 1,Askofu Mkude amesema ukimya usio na maelezo unaoendelea juu ya raia wanaopote a unatia mashaka na unajenga hofu Kubwa

Askofu Mkude amesema raia wanaopotea ni raia walio na familia,Ndugu jamaa na marafiki hivyo kupotea kwao kunapotokea na serikali kukaa kimya bila maelezo yoyote kunajenga hofu.

"Ipo huzuni kubwa kumpoteza Jamaa yake,na ni heri baadae ujue kama amefariki ili umuombee,kuliko kutokujua kabisa mahali alipo,inatia hofu" alisema

"Yesu alipotoweka,(kufa)na siku ya tatu alipoonekana tena(kufufuka)wanafunzi wake walifurahi mno,hivyo tunaitumaini furaha hiyo endapo siku moja Ndugu hawa wataonekana"

Vilevile Askofu Mkude aligusia upotoshaji wa habari za mitandao huku akiita ni kama"kilema Mamboleo".

Akisisitiza juu ya upotoshaji wa mitandao,Askofu Mkude alikumbushia kuhusu uzushi ulioibuka miezi mingi iliyopita juu ya kifo chake wakati akiwa katika matibabu nchini India.

"Nyinyi mtakuwa mashahidi wakati nazushiwa kifo,mlihuzunika sana,hata Arusha nasikia walishanisomea Misa,lakini mliponiona tena mlifurahi....japo nilikuwa natembelea fimbo,sasa hata fimbo sina tena,mmefurahi" alisema Askofu Mkude

"Furaha hiyo ndiyo tunayotarajia wataipata Ndugu wa raia waliopotea" alikazia

Lakini Askofu Mkude alisema ameomba barua yake hiyo isomwe Tanzania nzima ili ujumbe huo wa kupotea kwa raia uwafikie watu wote.

Mwisho Askofu Mkude alitaja vile alivyoviita vilema mamboleo ikiwemo suala la "siasa bila kanuni na sheria"

Hata Mussa alipomfata Farao na kutaka kuwato watu wake Utumwani alipingw sana na Farao hata akapigwa mapigo na Mungu hata alipowaachia hakuamini akawafuata nyuma. Kama sisi sio sauti ya Mungu basi anaye mungu wake anayemwamini yeye.
 
Kanisa la shetani, anahubiri ujinga. Huwezi kulinganisha ujinga wake na nchi ilivyokuwa inaibiwa. Natamani watu kama hawa wafe tu ili nchi iendelee. Ni
 
Askofu Mkude alikuwa Kama Askofu Kilaini walikuwa watetezi wakubwa sana wa Jakaya Hata pale Kanisa lilipokuwa linamuandama Mkwere Yule

Ana kweli kupungua Kwa Sadaka kanisani na kufyekwa Kwa Ruzuku za kwenda Makanisani kumesababisha Hata Bubu aongee
 
huyo askofu mkuda ndio nani?
kuna maaskofu wengine unaweza kujiuliza sijui kama hata hiyo biblia yenyewe wamewahi hata kuisoma?

Musa hakuwa kiongozi wa kidini akikuwa kiongozi/mtawala/mwamuzi wa wanaisrael ndio maana kulikuwa na maaskofu/makuhani chini yake ambao waliendesha ibada.

mwambie askofu mkuda Musa aliua ndio akakimbia kwa farao baada ya hapo akatumwa kuwakomboa waisrael misri, kazi yake ililithiwa na joshua waliwaongoza vitani waisrael huyu mkuda vipi? kwanza yeye ni m-kristo au m-musa? sasa kwanini afate ya musa aache ya kirsto

huyu mkuda ni mkuda kweli.
 
Ndugu kwenye maelezo yako umejichanganya zaidi kuliko askofu Mkude ambaye umeamua kwa makusudi kumuita Mkuda.
 
Back
Top Bottom