Kwa kuwa amekuwa mlei (kisheria) matendo yote anayoyafanya ya daraja takatifu (la kiaskofu) yatakuwa valid kwa sababu ya character ambayo haifutiki LAKINI yatakuwa illegal na yasiyotambulikana na Kanisa. Kumbe akisoma Misa mbele ya Kanisa Misa hiyo haitambuliwi kama Misa halali hata kama katika undani wake itakuwa valid. Akipadirisha au kutoa uaskofu wale waliopewa wanahesabiwa ni walei Tu mbele ya Kanisa (au wenye daraja la nyuma kabla ya huyu jamaa kuwapa hili la sasa) hata kama katika undani wake watakuwa wamepata daraja husika kama alifanya kile ambacho Kanisa hukifanya kwa uhalali wa sakramenti. Kumbe hawatatambuliwa kama ni mapadri au maaskofu, matendo yao watakayoyafanya yatakuwa hayana effect mbele ya Kanisa.
Mkuu, jaribu kuchagua maneno ya kutumia. Kisheria na hata kiteolojia Milingo hawi mlei. Ukinitajia kifungu chochote cha sheria ndani ya kanisa hilo kinachosema sasa Milingo amekuwa mlei Naacha uanachama wa Jamii Forum. Na atakayeniita mimi kilaza Moderator asimzuie kwani nitakuwa nimekuwa kilaza kweli.
Kazi kwako na kwa yeyote anayetaka kunithibitishia hilo kwamba sasa Milingo amekuwa mlei.