malasusa jitu la hovyo kabisa bladidaken
malasusa ni hopeless guy. Eti sikulelewa kutofautiana na serikali, kama serikali haitendi haki? stupid of him!Baadhi ya dondoo kwenye hotuba zake:-
1. Sikulelewa kuipinga serikali.
2. Njooni tusemezane. Tusemezane (dialogue) tukiwa na neno.
3. Kama angetafutwa wa kufaa kuwa Mkuu wa Kanisa basi mimi Malasusa nisingechaguliwa.
4. Rais uchaguzi mdogo 2024 tuufanye ufanikiwe.
5. Amani na mshikamano wa kitaifa.
6. Ninaipenda sana serikali yangu.
7. Rais suala la ndoa za jinsia moja tuachia Kanisa.
8. Amzawadia rais kwa kuhudhuria kwenye ibada iliyomsimika kuwa Mkuu Mpya wa KKKT Tz.
Tathmini.
Hotuba yake imemshushia Askofu Dr. Benson Kalikawe Bagonza wa Dayosisi ya Karagwe kitu kizito utosini.
Aidha, hotuba imempa Bagonza angalizo kutathmini nafasi yake ya criticism kipindi hiki ambacho yeye Malasusa anaenda kuliongoza Kanisa.
Malasusa ni kijana wa mjini Bagonza ni kijana wa shambani, kuvumiliana kunahitajika kwa mustakabali na maslahi mapana ya Kanisa na taifa.
Bagonza alikuwa Askofu Juni 15, 2003. Alikuwa Msemaji Maarufu kwenye Makanisa ya Lutheran Western Illinois kwa miaka 7 alipokuwa akisoma katika chuo cha Wartburg Seminary Dubuque.
2020 aliamua kujiimarishia ulinzi binafsi kufuatia kuhisi hakuwa salama.
Malasusa alikuwa Askofu Aprili 17, 2004 na sasa Mkuu wa Kanisa mara 2. Anajuwa kuchanga karata na kujipatia dume zote. Ni Banker hivyo anajuwa hesabu vizuri.
Asilimia kubwa ya wafuasi wa Kanisa hawakukubaliana na Malasusa kurudi kwenye Ukuu wa Kanisa na ikadhaniwa amefanikiwa kwa mkono wa serikali.
Nijuavyo mimi, Kanisa ni Watchdog wa serikali kama lilivyo mhimili wa Bunge. Kanisa pia limepewa jukumu adhimu na MUNGU la kusahihisha utendaji na mwelekeo wa serikali ili amani idumu kazi ya MUNGU isonge mbele.
Malasusa hakuongelea yafuatayo ambayo Bagonza hasingeyaacha:-
Ugumu wa maisha.
1. Sukari 1kg 5,000/
2. Nyama ya ng'ombe 1kg 12,000/
3. Nyama ya nguruwe 1kg 13,000/
4. Nguruwe na ng'ombe wanachuana mtanange wa bei.
5. Samaki 1kg 10,000/ baada ya Ziwa Victoria na Tanganyika kufungwa.
6. Usalama wa Chakula hususan ugavi na bei kutokuwa himilivu.
7. Pengo kubwa la kipato.
8. Uhaba wa nishati unaohujumu jitihada za wananchi kujikwamua na umaskini.
Maridhiano ya kisiasa.
1. Madai ya Katiba Mpya.
2. Mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi.
3. Misighishano ndani ya vyama iliyosababisha kesi Mahakamani.
4. Changamoto za Siasa za Kanisa (Church Politics).
Nini tathmini yako.