mfianchi
Platinum Member
- Jul 1, 2009
- 11,855
- 8,253
Imebidi nijiulize baada ya kusoma kwenye gazeti kuwa Askofu Malasusa alikuwa msemaji wa familia ya Lowasa kwenye harusi ya binti yake,sijui huu urafiki umeanza baada ya Malasusa kuwa Askofu wa Dayosisi ya Mashariki pwani,kwa kiongozi wa dini ambaye anaelewa tuhuma za Lowasa kujifanya anamfagilia kwa kumsifia mambo amabyo wala Lowasa hanayo ni unafiki mkubwa si ntashangaa hapo baadaye tukimsikia Askofu Malsusa akisema Lowasa ni chaguo la Mungu,Si elewi uhusiano uliopo kati ya Lowasa na hawa maaskofu wetu kwanza Askofu Laizer wa Arusha naye akajitoma kumpokea Lowasa pale Arusha baada ya kupima hoja za Richmond hata akajiuzulu,kabla hatujakaa sawa mkewe Lowasa akazindua kitabu kama kawaida Maaskofu akiwemo Kardinali Pengo wakajitoma kwenye hiyo hafla jamani maaskofu kama hamjijui Lowasa anawatumia kwa malengo yake na sisi waumini wenu mnatutia kinyaa kwa hizo tabia zenu !!