Askofu Malasusa msemaji wa familia ya Lowasa

wapendwa naomba niwakumbushe tu kuwa maaskofu wachungaji n.k. ni binadamu kama mimi na wewe, na taasisi za dini ni taasisi kama ilivyo taasisi zingine mf. benki, viwanda vya bia n.k. kwenye dini pia huhitajika fedha, msisahau hata yuda alimkana YESU kwa vipande vya fedha, kwa hiyo bado hat hawa viongozi wa dini wa leo wanaendeleza hayo yaliyopita. Kwanza ukiliangalia kanisa au taasisi ya dini kwa nje ndio unaweza ukawa muumini mzuri, ukiingia kwa undani wallah lazima utaikana dini yako, kuna mambo meeeeengi sana ya uchafu mkubwa yanafanywa kwa mgongo wa dini, dini dini. so tujue kuwa kanisa/maaskofu ni wakosefu kama wengine na yaliyo mengi wanayafanya kwa manufaa yao na si kwa mujibu wa neno la Mungu
 
nimetapika kabisa.

siamini kama kweli malasusa ameamua kukumbatia jambazi leo.
alipaswa kumhubiria kwanza aache uovu, arudishe alichoiba na riba juu kisha afunguliwe milango ya mbingu. Ukwasi wa matajiri hauwapi uhalali wa kumiliki mbingu, labda wataimiliki dunia na kuzimu pekee.
 
Hivi siyo huyu Malasusa aliyemkemea yule mchungaji wa KKKT Kijito nyama aliemwalika Rostam Azizi kwenye harambee ya kwaya? Wakatangaza kuwa fedha ya kifisadi hawatachukua? Na mchungaji yule akahamishwa/fukuzwa? Sasa inaelekea wanaliona suala la EL kama vile mwana kilutheri anapigwa vita. Jamani viongozi wetu acheni hizo!!!
 
Baada ya Harusi------ Viongozi wengi hawakuuzulia kwenye TISA DISEMBA--- SIKU YA UHURU.
so, wapi priority-- Lowasa and Family walipopanga Harusi walijua kabisa 9/12 hipo na ni siku mhimu kwa taifa la Watanganyika..........ndo maana kama Waziri mkuu wa zamani walitakiwa angalau watie jicho...lakini wapi.......

WHERE BOYZ 2 MEN...... WAMEJITENGA.
 
Mtenganishe siasa na dini. Padre, Mchungaji, Askofu na wanaroho hawaruhusiwi kubagua binadamu kutokana na dhambi au tuhuma, kwani mwenyezi mungu alimtuma mwanae kuwaokoa watenda dhambi. Baba wa kiroho yupo hapa kukusaidia wewe mtenda dhambi, they are not here tu judge...only god does that!
 
malasusa kapozwa na cha juu,ndio maana anakuwa mstari wa mbele kusifia mambo ya kipumbavu katika jamii...tulitegemea awe wa kwanza kukemea mambo ya kishenzi aliyoyafanya lowasa kwa manufaa ya taifa lake(malasusa). badala yake anasifia ujinga mtupu..ndio maana mimi sio muumini wa dini yoyote ile kwani ni upumbavu mtupu unaoendelea kwenye hizi dini
 
Wajemeni, Maaskofu ni Wachungaji, kazi ya wachungaji ni kuwachunga kondoo wa Bwana wasipotee, Masiya alikuja kwa waliopotea na wale walio elemewa na mizigo ili wapumzishwe.

EL amepotea na ameelemewa na mizigo ya tuhuma, shutuma na kila aina ya bezo, dhihaka, kejeli, matukano, ya kila aina mpaka chuki binafsi mumo humo, kwa watu wa Mungu, huu ndio wakati wa kukaa karibu kabisa na EL na sio kumtenga, bali kumkumbatia mpaka aguswe na roho wa Bwana, atakuja mbele ya kadamnasi ya watu, atatubu, atasamehewa, atatakaswa na atangara kama mbalamwezi tayari kwa 2015!.

Amini nawaambieni, 'jiwe walikolikataa waashi, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni'. Kwake Yeye, wa kwanza atakuwa wa mwisho, na wamwisho atakuwa wa kwanza.

Acha Maaskofu watimize mapenzi ya Bwana, ya kuwarudisha kundini kondoo waliopotea.
Mbona huo mchakato ameshaunza mara baada ya kugundua kosa. EL siyo mchezo! Hajapoteza vision yake. Anailinda kama mboni ya jicho. Kwaufundi mkubwa anarekebisha yaliyopita na kuweka sawa pale palipo pinda. Sijui issues za integrity yake zitakuwaje ili 2015 ndoto yake itimie ila namuona ameamua kupigana kufa na kupona!!
 
Ishu sio maaskofu tu, mchangia hoja aseme hata Dk Salim, warioba,Mbatia walikuwepo pia lakini tatizo isiwe kuwepo kwa hao prominent figures, je Watanzania tumefikia zama ambazo hatuwezi kuhudhuria shughuli za kijamii za watanzania wenzetu eti kwa kuwa tu tuna tofauti nao kimitazamo? sioni hoja hapo

kuwepo kwa hao viongozi si tatizo! tatizo ni kumsafisha!
 
Imebidi nijiulize baada ya kusoma kwenye gazeti kuwa Askofu Malasusa alikuwa msemaji wa familia ya Lowasa kwenye harusi ya binti yake,sijui huu urafiki umeanza baada ya Malasusa kuwa Askofu wa Dayosisi ya Mashariki pwani,kwa kiongozi wa dini ambaye anaelewa tuhuma za Lowasa kujifanya anamfagilia kwa kumsifia mambo amabyo wala Lowasa hanayo ni unafiki mkubwa si ntashangaa hapo baadaye tukimsikia Askofu Malsusa akisema Lowasa ni chaguo la Mungu,Si elewi uhusiano uliopo kati ya Lowasa na hawa maaskofu wetu kwanza Askofu Laizer wa Arusha naye akajitoma kumpokea Lowasa pale Arusha baada ya kupima hoja za Richmond hata akajiuzulu,kabla hatujakaa sawa mkewe Lowasa akazindua kitabu kama kawaida Maaskofu akiwemo Kardinali Pengo wakajitoma kwenye hiyo hafla jamani maaskofu kama hamjijui Lowasa anawatumia kwa malengo yake na sisi waumini wenu mnatutia kinyaa kwa hizo tabia zenu !!

kwani kuna ubaya gani askofu akiwa MC au msemaji wa familia???mbona kikwete mlikubali alipoitwa chaguo la mungu!!! umesahau maneno ya waungwana kuwa mwenye nguvu muache apite...he is powerful and he can do anything ..we hujaona sherehe za send off ya mtoto wake ilinoga kuliko sherehe zetu za uhuru pale shamba la bibi
 
malasusa kapozwa na cha juu,ndio maana anakuwa mstari wa mbele kusifia mambo ya kipumbavu katika jamii...tulitegemea awe wa kwanza kukemea mambo ya kishenzi aliyoyafanya lowasa kwa manufaa ya taifa lake(malasusa). badala yake anasifia ujinga mtupu..ndio maana mimi sio muumini wa dini yoyote ile kwani ni upumbavu mtupu unaoendelea kwenye hizi dini

acha kutusi dini ..kwanza wewe umekimbia kwenu unakaa huko SA ya huku yanakuwashia nini...umasikini unawatia hasira sana..EL mnaye mpaka awe rais ndo mtafunga midomo....hahaaaaa
 
Askofu Malasusa ni Askofu wa dayosisi ya mashariki na pwani pia ni Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania [KKKT].Ushiriki wa Askofu Malasusa na Askofu Thomas Laiser kwenye sherehe za kumwaga mtoto wa E N Lowassa kwa mara nyingine umelizalilisha kanisa na viongozi wake jinsi walivyotayari kuwakumbatia matajiri bila kujali njia walizotumia kuupata utajiri.

Mara kadha kanisa limejikuta linajitia doa kwasababu viongozi wake hawataki kufuata maandiko matakatifu.Sikuwepo kwenye sherehe lakini bila shaka kulikuwepo pombe nyingi zilizowafanya wageni kukaa kwenye sherehe hadi usiku wa manane.Fikiria kanisa la KKKT linavyokemea ulevi [unywaji wa pombe] lakini viongozi wake wa juu yaani maaskofu wawili na akili zao wanashiriki kwenye sherehe kwasababu tu Lowassa ana fedha.

Sipendi viongozi wa kanisa kukubali kutumika na wanasiasa wasiokuwa na maadili kama E N Lowassa.

Lakini mtuhumiwa sio mkosaji. Kujiuzuru ilibidi kwa sababu ya wadhifa wake. Amehukumiwa wapi kwamba ni mkosaji Lowasa? Hata kama anayo makosa, hakuna aliyempeleka mahakamani kuthibitisha uhalifu wake. Maneno ya wapinzani sio hukumu ya Lowasa.

Lowasa pia alikuwa mzee wa kanisa pale Azania Front kwa muda mrefu, amefanya kazi kwa karibu sana na wachungaji wengi waliowahi kupitia pale. Kwa hiyo ikiwa mtaani watu wanakutuhumu wewe kuwa mchawi tuamini kwamba wewe umethibitika kuwa mchawi kweli na tukutenge? Jamani tusibebe dhambi za wengine. Ameshindwa nini mtu yeyote kupeleka ushahidi wake mahakamani kuanika ukweli wa tuhuma hizo. Kwa maoni yangu atabaki kuwa na tuhuma mpaka tuhuma hizo zithibitishwe.

leka
 
Mmesahau kuwa chuo cha Tumaini Dar na Iringa vimejitenga?
Hawa wa Dar wanafanya michango kwa hali na mali na wao wajenge chuo kikubwa kama cha Iringa sasa wapi watapata pesa nyingi kama sio kwa mafisadi? Wanajidai wanawasafisha hapo hapo na wao wanatokea na kuponea njaa zao humo humo.
 
Askofu malasusa ni rafiki mkubwa wa lowassa.Nakumbuka hata wakati wa mchakato wa kumtafuta mkuu wa kkkt, lowassa alitia mkono wake ili malasusa achaguliwe. Aidha, baada ya kuchaguliwa malasusa, lowassa alimwandalia sherehe ya kumpongeza pale oysterbay.Sioni jipya hapo, bado Eddo ataendelea kumtumia tu pamoja na viongozi wengine wa dini mufilisi.
 
Ni kawaida kwa kanisa la Lutherani kuongozwa na viongozi wa siasa. Nafikiri Lowasa ana say sana ndani ya kanisa lile. Ndo maaana askofu Laizer alisafiri toka Arusha hadi Dar. Pia ninakumbuka vizuri namna ambavyo David Msuya alivyowahi kuwa na influence kubwa katika doyosisi mojawapo nchini na kusababisha migogoro mikubwa. I guess kanisa la kilutheri linajipendekeza sana kwa wenye pesa. Lichunge sana maana huyo Malasusa, ningemwalika aje abariki harusi yangu angesema nimwone mchungaji wa usharika wangu. lakini kwakuwa aliyemwomba anazo, mmmh hata kazi ya kuhudumia waumini wengine inasitishwa. Kuna haja ya kanisa hili kujiangalia upya, namna ambavyo linawahudumia waumini wake. Naamin waumini wote masikini kwa matajiri ni sawa.

Siku hizi dini zote ni biashsra na ndio maana ukienda kwenye sala zao mambo ni ya sadaka,michango na minada ili kupata fedha na hapo ndipo wenye nazo wanapopata upenyo wa kuwa na influence kubwa!! Sio hivyo tu, siku hizi tofauti na zamani watu wenye fedha na vyeo wana hadhi tofauti katika makanisa na ndio maana ukienda pale Azania front kusali utakuta kuna sehemu za kukaa ambazo ni reserved kwa watu fulani; mfano ni Lowassa ingawa sio waziri mkuu tena lakini kanisa la Malasusa limemtengea sehemu yake maalum, sasa sijui ndio utaratibu wao na kama ni hivyo siku ambayo vigogo wengi wakija kusali sijui itakuwaje? Kanisa lisilete ubaguzi kwa waumini wake wakati wa ibada, kama kuna protocol iwe baada ya misa na sio wapambe kuongozana na Lowassa hata anapokwenda kupokea chakula cha BWANA hapo inakuwa dhihaka madhabahuni!! Anakotoka Malasusa watu hawatumiwi namna hii, haipendezi.
 
Waswahili walisema "Penye njaa penyeza rupia" hii ndio kazi ya rupia za kifisadi. Wataitumia kujisafisha kwa kila gharama na kwakushibisha kila tumbo lenye njaa na lisiloshiba.
Tusisahau pia Malasusa ni binadamu na ni baba wa familia. Pamoja na kuwajibika kwa kanisa anawajibika kwa familia pia hivyo anajaribu kuwajengea watoto wake mtandao maana si lazima wao wajewaelekee mrengo wake aliopo(Uchungaji/ Uaskofu).Na kanchi haka kamekua ka mtandao kila pahala.Naamini roho yake haitaki ajihusishe na hawa mafisadi lakini mwili wake ni dhaifu. Hii hali ya mwili na roho kutofautiana kimatakwa ilimtokea hata masiha pale alipokua anaelekea kusulubiwa, hivyo huu ni udhaifu wa kawaida kikubwa ni uwezo wa kuushinda ambao Malasusa ameshadhihirisha kushindwa kuuhimili udhaifu huu.

Tutoe wito kwa watanzania wenye imani wawaombee viongozi waregevu hawa
\


nADHANI SI PENYE NJAA NI PENYE UDHIA PENYEZA RUPIA
 
imebidi nijiulize baada ya kusoma kwenye gazeti kuwa askofu malasusa alikuwa msemaji wa familia ya lowasa kwenye harusi ya binti yake,sijui huu urafiki umeanza baada ya malasusa kuwa askofu wa dayosisi ya mashariki pwani,kwa kiongozi wa dini ambaye anaelewa tuhuma za lowasa kujifanya anamfagilia kwa kumsifia mambo amabyo wala lowasa hanayo ni unafiki mkubwa si ntashangaa hapo baadaye tukimsikia askofu malsusa akisema lowasa ni chaguo la mungu,si elewi uhusiano uliopo kati ya lowasa na hawa maaskofu wetu kwanza askofu laizer wa arusha naye akajitoma kumpokea lowasa pale arusha baada ya kupima hoja za richmond hata akajiuzulu,kabla hatujakaa sawa mkewe lowasa akazindua kitabu kama kawaida maaskofu akiwemo kardinali pengo wakajitoma kwenye hiyo hafla jamani maaskofu kama hamjijui lowasa anawatumia kwa malengo yake na sisi waumini wenu mnatutia kinyaa kwa hizo tabia zenu !!
  • tuhuma zipi acha kutumika kama kondomu
 
Yule jambazi wa magari UK,alifungishwa harusi na nani hapa bongo?si huyu Malasusa
 
kkkt kwa muda mrefu wamejitahidi kutaka kutoa rais kwa mtazamo wao wanahisi kanisa katoliki wamefanikiwa kwa kuwa wameweza kutoa rais mara mbili ndio maana wako tayari kumbeba mtu yeyote hata awe fisadi ili mradi wampeleke rais mlutheli
 
Mtenganishe siasa na dini. Padre, Mchungaji, Askofu na wanaroho hawaruhusiwi kubagua binadamu kutokana na dhambi au tuhuma, kwani mwenyezi mungu alimtuma mwanae kuwaokoa watenda dhambi. Baba wa kiroho yupo hapa kukusaidia wewe mtenda dhambi, they are not here tu judge...only god does that!

kuwasaidia watenda dhambi ni kukemea wanacho fanya na kuwaelekeza njia sahihi na sio kuwaunga mkono kama wafanyavyo viongoz weng wa hizo dini za wazungu
 
Back
Top Bottom