Askofu Kyando: Watanzania wameanza kusahau utu

Askofu Kyando: Watanzania wameanza kusahau utu

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,438
Reaction score
5,235
Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe, Mhashamu Eusebius Kyando, ametoa wito kwa Watanzania kurejea katika msingi wa kuthamini utu wa binadamu kama nguzo muhimu ya ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.

Akizungumza kwenye mahafali ya 25 ya Taasisi ya Mafunzo ya Afya Lugarawa (LUHET) yaliyofanyika Julai 27, 2025, katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, Askofu Kyando amesema kumekuwa na mwelekeo wa kupungua kwa maadili ya utu jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo ya kijamii.

 
Dah Mungu awasaidie. Maana wanavyofurahi wangejua mtaa ipoje wwngesali. Wanafuraha kwa kweli.
 
Back
Top Bottom