"Kuwa waadilifu ni kitu cha maana. Tunatakiwa kuishi maisha maadilifu kwa wakati wote, tusingoje kutuhumiwa," aliasa Askofu Malasusa.
Wakati huo huo, Muhibu Said anaripoti kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, amesema hatajibu tuhuma za ufisadi wa mabilioni ya fedha za umma, zilizoelekezwa kwake na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa.
Kauli hiyo ambayo ni ya kwanza kutolewa tangu Dk Slaa ambaye pia ni Mbunge wa Karatu awataje vigogo 11, akiwamo Lowassa kwamba, ni mafisadi waliohusika na ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma, ilitolewa kupitia mwandishi wake, Said Nguba juzi.
Kauli hiyo haikufafanua sababu za Waziri Mkuu kuamua kutojibu tuhuma hizo nzito ambazo baadhi ya vigogo, akiwamo Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Gray Mgonja, kutangaza msimamo wa kukusudia kumshtaki mahakamani Dk Slaa kwa madai ya kuchafuliwa majina.
Alisema madai kwamba Waziri Mkuu asipojibu tuhuma ina maana kuwa anakubaliana nazo, ni tafsiri ya Dk Slaa na wenzake na kusisitiza kuwa hana la kujibu juu ya tuhuma hizo.
"Waache wengine wajibu, sisi hatuna cha ku-coment juu ya hilo," alisema Lowassa kupitia mwandishi wake, Nguba.
............
Tayari viongozi sita, akiwamo Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, Karamagi, Mgonja na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Patrick Rutabanzibwa, wameshatoa taarifa kwa waandishi dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwao kwa nyakati tofauti.