Askofu KKKT aitaka serikali kujichunguza kwa madai ya ufisadi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,082
*Asema kiwango kinachodaiwa kufujwa kinatisha
*Lowassa asema yeye hatajibu tuhuma za ufisadi

Na Mwandishi Wetu
Mwananchi

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Alex Malasusa, ameitaka serikali kupitia vyombo vyake kuchunguza tuhuma zilizotolewa na Kambi ya Upinzani dhidi ya viongozi wa serikali ili kujiridhisha kama ni za kweli au ni mchezo wa kisiasa.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili, Askofu Malasusa, alisema uchunguzi wa tuhuma hizo ni muhimu kwa sababu kiwango cha fedha kinachodaiwa kufujwa ni kikubwa kinachoshtua sana katika jamii ya kimaskini.

"Jamii yetu ni ya kimaskini. Katika jamii ya namna hii tunapozungumzia mabilioni yanashtusha sana, ni vizuri uchunguzi ufanyike kama ni kweli sawa na kama si kweli ifahamike," alisema.

Askofu huyo alisema tuhuma hizo zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, zinaweza kuthibitishwa na vyombo vilivyopo kisheria, hivyo akawataka Watanzania kuwa watulivu na kusubiri hadi tuhuma hizo zisithibitike.

"Hizi ni tuhuma tu, zinaonekana kama za kisiasa, maana huyu anasema hili, huyu anasema lile, lakini kinachoweza kuzithibitisha ni vyombo vyetu vya kisheria," alisema Askofu Malasusa.

Askofu huyo aliwataka Watanzania wote kuwa waadilifu, wakati wote bila kungoja tuhuma na kujisafisha.

"Kuwa waadilifu ni kitu cha maana. Tunatakiwa kuishi maisha maadilifu kwa wakati wote, tusingoje kutuhumiwa," aliasa Askofu Malasusa.

Wakati huo huo, Muhibu Said anaripoti kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, amesema hatajibu tuhuma za ufisadi wa mabilioni ya fedha za umma, zilizoelekezwa kwake na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa.

Kauli hiyo ambayo ni ya kwanza kutolewa tangu Dk Slaa ambaye pia ni Mbunge wa Karatu awataje vigogo 11, akiwamo Lowassa kwamba, ni mafisadi waliohusika na ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma, ilitolewa kupitia mwandishi wake, Said Nguba juzi.

Kauli hiyo haikufafanua sababu za Waziri Mkuu kuamua kutojibu tuhuma hizo nzito ambazo baadhi ya vigogo, akiwamo Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Gray Mgonja, kutangaza msimamo wa kukusudia kumshtaki mahakamani Dk Slaa kwa madai ya kuchafuliwa majina.

Alisema madai kwamba Waziri Mkuu asipojibu tuhuma ina maana kuwa anakubaliana nazo, ni tafsiri ya Dk Slaa na wenzake na kusisitiza kuwa hana la kujibu juu ya tuhuma hizo.

"Waache wengine wajibu, sisi hatuna cha ku-coment juu ya hilo," alisema Lowassa kupitia mwandishi wake, Nguba.

Septemba 15, mwaka huu, Dk Slaa kwa kushirikiana na mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu, wakihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mwembeyanga, jijini Dar es Salaam, waliwataja viongozi 11 wa serikali kwamba ni mafisadi waliohusika na ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma.

Tayari viongozi sita, akiwamo Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, Karamagi, Mgonja na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Patrick Rutabanzibwa, wameshatoa taarifa kwa waandishi dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwao kwa nyakati tofauti.

Juzi akisoma tamko la vyama vilivyoko katika ushirikiano wa kisiasa, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Victor Kimesera, alisema baadhi ya viongozi wa serikali waliotajwa wamekaa kimya kwa wiki mbili tangu tuhuma hizo zitolewe dhidi yao na kuwa hiyo ni ishara ya kukubaliana na tuhuma za ufisadi zilizotolewa hadharani dhidi yao.
 
Lowassa mjanja, anajaribu kuangalia upepo unakoelekea. maana wote waliojibu hakuna aliyetoa hoja ya kuridhisha zaidi ya kutishia kwenda mahakamani.
 
Wote mafisadi tu hata taarifa kupitia wizara ya habari waliyotoa leo kwenye vyombo vya habari haijitoshelezi zaidi yakudai eti wao safi! Na mbwembwe kibao za kusifia chama zisizo na maana.
 
"Kuwa waadilifu ni kitu cha maana. Tunatakiwa kuishi maisha maadilifu kwa wakati wote, tusingoje kutuhumiwa," aliasa Askofu Malasusa.

Wakati huo huo, Muhibu Said anaripoti kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, amesema hatajibu tuhuma za ufisadi wa mabilioni ya fedha za umma, zilizoelekezwa kwake na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa.

Kauli hiyo ambayo ni ya kwanza kutolewa tangu Dk Slaa ambaye pia ni Mbunge wa Karatu awataje vigogo 11, akiwamo Lowassa kwamba, ni mafisadi waliohusika na ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma, ilitolewa kupitia mwandishi wake, Said Nguba juzi.

Kauli hiyo haikufafanua sababu za Waziri Mkuu kuamua kutojibu tuhuma hizo nzito ambazo baadhi ya vigogo, akiwamo Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Gray Mgonja, kutangaza msimamo wa kukusudia kumshtaki mahakamani Dk Slaa kwa madai ya kuchafuliwa majina.

Alisema madai kwamba Waziri Mkuu asipojibu tuhuma ina maana kuwa anakubaliana nazo, ni tafsiri ya Dk Slaa na wenzake na kusisitiza kuwa hana la kujibu juu ya tuhuma hizo.

"Waache wengine wajibu, sisi hatuna cha ku-coment juu ya hilo," alisema Lowassa kupitia mwandishi wake, Nguba.

............

Tayari viongozi sita, akiwamo Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, Karamagi, Mgonja na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Patrick Rutabanzibwa, wameshatoa taarifa kwa waandishi dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwao kwa nyakati tofauti.
Tumetoka mbali :)
 
Mbona hata yeye na kanisa lake ameshindwa kurekebisha kero hadi watu wamewabandika hapa kuwa nao ni mafisadi hao KKKT
 
Mbona hata yeye na kanisa lake ameshindwa kurekebisha kero hadi watu wamewabandika hapa kuwa nao ni mafisadi hao KKKT
Ule ni UWONGO wa kutaka kuchafua watu bila ushahidi. Ndo maana topic yenyewe kwa kukosa ushahidi imewekwa kwenye forum hii:

Uzushi?

We do not entertain such posts, aliandika kama anaelekea kuwa na uthibitisho lakini hakuleta uthibitisho wa kauli yake. Si vema kuwachafua watu kwa mtindo ule. Akileta ushahidi Inshallah, tutakubaliana na alichoandika, otherwise, Malasusa alichoongea mwaka 2007 (2yrs ago) ni kitu muhimu SANA kwa taifa letu.
 
Tangu hawa viongozi wa dini wajiingize kwenye siasa, wamejiondolea uhalali wa khionya serikali.
 
Back
Top Bottom