Askofu Kilaini kuendelea kuwa Askofu Msaidizi

Askofu Kilaini kuendelea kuwa Askofu Msaidizi

Mie niulize askofu wa katoriki akisitaafu anaenda wapi maana hawana familia kwamba akae alee wajukuu!
 
umetumwa ?
Hako katoto kana kila dalili ya ushoga. Na kanaonekana hakako vizuri kisaikolojia! Muda wote kanaongelea ulawiti, kutolewa marinda, kubakwa, nk.

Hivyo mnatakiwa mkapuuze, au mkaweke kwenye ignore list, kama nilivyofanya mimi.
 
Mie niulize askofu wa katoriki akisitaafu anaenda wapi maana hawana familia kwamba akae alee wajukuu!
Mapadre na Maaskofu wazee hupelekwa kuishi kwenye nyumba zao maalum za malezi, ambapo huhudumiwa kwa kila kitu na Kanisa. Mfano chakula, malazi, mavazi, mazoezi, nk. Mpaka pale Mwenyezi Mungu atakapo wachukua.
 
Je rulenge na ngara Ni Jimbo kuu au

Kwa hyo mkoa mmoja inaweza kuwa na maaskofu wawili au Zaid na nn kigezo kuwa hvyo

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Jimbo sio Mkoa. Kanisa Katoliki halifuati mipaka ya kijiografia ya mikoa ya Tanzania. Kwa mfano, Zanzibar kwa kanisa katoliki ni jimbo, sawa na kahama, sawa na lindi! Kwahiyo mkoa mmoja wa kijiografia unaweza ukawa na majimbo zaidi ya moja. kwa mfano, mkoa wa Morogoro una majimbo matatu ya katoliki, jimbo la Morogoro, jimbo la Mahenge na jimbo la Ifakara.

Mfano mwingine Bagamoyo ni karibu sana na Dar es Salaam lakini ni jimbo la Morogoro. Wakati Mafia ni mbali sana ni Jimbo la Dar es Salaam. Eneo kubwa la Pwani Jimbo la Dar es Salaam ukiondoa Bagamoyo. Dar es Salaam imetamani kwa muda mrefu kumiliki ili eneo la Bagamoyo bila mafanikio. Mkoa wa Pwani umetamani sana kuwa na jimbo lao bila mafanikio. Kule Moshi, eneo la Rombo wanatamani sana kuwa jimbo bila mafanikio.

Kwanini wengine wanafanikiwa na wengine hawafaniki kuwa majimbo fanyeni utafiti!!!!

Jimbo ni sehemu wa waamini walio chini ya askofu. Hapo sifa kubwa ni askofu. Askofu ni Jimbo na jimbo ni Askofu. Kuna baadhi ya maaskofu katoliki ukimpigia simu anaitikia kwa kusema hallo jimbo linaongea...... na wahusika wanaelewa nini maana yake? Kwa kanisa katoliki askofu ana mamlaka makubwa sana wakati mwingine zaidi ya Mungu.

Jimbo Kuu ni sehemu ya majimbo yaliyo katika kanda moja ama kihistoria au pia kijiografia ukisikia jimbo kuu la Dar es Salaam ndani yake kuna (suffragan dioceses) za Mahenge, Ifakara, Morogoro, Tanga na Zanzibar! Na Askofu anae ongoza Jimbo Kuu lazima awe Askofu Mkuu. Kuwa Askofu Mkuu hakufanyi awe mkuu kwa majimbo yaliyo katika hiyo kanda. Kila askofu ni mkuu katika jimbo lake na anawajibika moja kwa moja na Vatican.

Pia ni muhimu kuzingatia haya majimbo hayapangwi na watanzania wenyewe ni Baba Mt peke yake ndio ana mamlaka ya kutangaza eneo fulani kuwa jimbo.
 
Back
Top Bottom